Wenye Kuhofia Uenyekiti wa Magufuli CCM Wana Hoja za Msingi? Ndiyo!!

Ni
Hii ni ajabu na kweli. Yaani mtu mliyemkabidhi nchi, akawa amiri jeshi mkuu na mkuu wa nchi, leo him mnajuliza kuhusu uwezo wake wa kuongoza? Really? CCM acheni ubinafsi.

Wala sio ajabu, democracy ndani ya chama ni tofauti na democracy ndani ya nchi. Vipo vyama vya kidikteta vinanvyotawala nchi zinazofuata democracy. Kadhalika yawezekana rais wetu ni kiongozi shupavu katika ngazi ya nchi na sio ngazi ya chama ambacho kina misingi tofauti. Ndio maana nchi za wenzetu zimetofautisha uongozi wa chama na uongozi wa nchi na huku nyingine zikimtaka kiongozi wa nchi kupitia kwanza uongozi wa chama kabla ya kuwa kiongozi wa nchi.
 
Nisingependa kujadili watu kwa sana. Nitajadili dhana.Nilipoandika "Magufuli" chukulia mtu yeyote atakayekuwa rais kama Magufuli alivyo sasa.

Niliandika hivi pengine hapa, kwenye suala hili.

Tatizo linakuja:

Itakuwa vipi kama Magufuli anakuwa Mwenyekiti wa CCM halafu his two loyalties (to CCM and to the government) zinapata conflict?

Itakuwa vipi kama Magufuli rais anaona classified infornation kama rais ambazo Magufuli Mwenyekiti wa CCM hatakiwi kuziona?

Itakuwa vipi kama Magufuli Mwenyekiti wa CCM anataka kuwawajibisha wabunge wa CCM directly yeye mwenyewe lakini anafungwa na vifungu vya separation of powers executive kutoingilia bunge kwa sababu ni rais?

Itakuwa vipi kama Magufuli rais anatakiwa kuwepo katika shughuli za serikali kama rais na wakati huo huo kuna shughuli za muhimu za chama Magufuli Mwenyekiti wa CCM anatakiwa awepo muda huo huo? Ataenda wapi? Kwenye shughuli za serikali au za chama? Na kuchagua shughuli yoyote kati ya hizi mbili hakutaipunja nyingine?
Huoni kwamba mtu mmoja ambaye ana masaa 24 tu kwa siku moja na anasema halali mpaka saa nane usiku akifanya kazi ya urais, ukimuongezea kazi ya uenyekiti wa chama utamnyima zaidi muda wa kufanya kazi ya urais?

Itakuwa vipi kama watu wataona kwamba Magufuli Mwenyekiti wa chama anagharamiwa na mfuko wa serikali katika kufanya shughuli za chama? Inevitably atahitaji kutumia gharama za serikali.

Itakuwa vipi kama Magufuli Mwenyekiti wa chama ataambiwa na chama kwamba chama kinahitaji fedha ambazo hakitaweza kuzipata kutoka vyanzo vyake vya fedha na Magufuli akawa na uwezo wa kuagiza fedha hizo zitoke katika mfuko wa serikali? Tumeona hili nyakati za chaguzi CCM wanachukua fedha nyingi kutoka mashirika ya umma nje ya utaratibu. Tukisema hii ni moja ya sababu CCM wanataka rais awe mwenyekiti wao watakataa? Ukimweka Ole Sendeka awe Mwenyekiti, Ole Sendeka si anayeteua Mkurugenzi wa NSSF. Kwa hiyo Ole Sendeka akitaka fedha za NSSF ziende kusaidia uchaguzi wa CCM kunakuwa na msururu wa watu wa kuwapitia na ku approve. Na kama rais ni mwanachama wa kawaida tu, anakosa leadership role kuhakikisha fedha zinapatikana. Especially kama kuna scandalous implications na yeye anastaafu. Hapo utaona moja ya sababu wanataka rais awe Mwenyekiti wa CCM ni kurahisisha wizi wa fedha za umma. Rais akimpigia simu Mkurugenzi wa NSSF kumuomba milioni mia kadhaa zipelekwe kwenye uchaguzi wa CCM, Mkurugenzi wa NSSF kama anaitaka kazi yake hawezi kukataa. You cant say Magufuli ana clean up NSSF kwa sababu naongelea principle zaidi kuliko Magufuli. What if we do not get somebody who is geared in cleaning up?

Itakuwa vipi kama wabunge wa CCM wanataka kumpigia rais kura ya kutokuwa na imani naye lakini wanaogopa kwa sababu wakimtoa urais bado atawapatiliza katika chama? Huoni kwamba hilo linapunguza uhuru wa bunge na checks and balance? Rais badala ya kuongoza executive a deal na legislature na judiciary, anakuwa anaongoza executive na party. This weakens checks and balance.

Vivyo hivyo, kwa upande mwingine, Itakuwa vipi kama rais kakosea chamani wanachama wanataka kumtoa lakini wanaogopa wakimtoa bado atawashughulikia kama rais? Huoni kwamba kuwa na vyeo hivi viwili kunatengeneza ka mungu mtu fulani hivi?

Itakuwa vipi kama rais hatekelezi ilani ya chama na anajitungia mwenyewe vitu vya kufuata na mtu wa kwanza anayetakiwa kumsimamia kurudi kwenye ilani ya chama ni mwenyekiti wa chama, na mtu huyo hawezi kufanya hivyo kwa sababu mwenyekiti wa chama ni rais huyo huyo? Huoni kwamba hapa tunatengeneza kitu kinachoitwa "a single point of failure"?

Talking about a single point of failure, pishia mbali isitokee, lakini sote ni watu, tuna uwezekano wa kupigwa daflao na kuanguka. Kwa nini tunataka likitokea hilo kwa mtu mmoja liwe na impact kubwa sana kwa chama na serikali?

Kwa leo point hizi kumi zinatosha kukufanya uchambue hoja kwa kina zaidi.
 
Kabla ya mengine, mimi nataka kujua huko Dodoma kunaenda kufanyika uchaguzi au uteuzi? Ni kipi kati ya hivyo viwili kipo kikatiba? Kama ni uchaguzi, mbona sioni faida au/na hasara za mgombea mwingine zaidi ya JPM zikichambuliwa hadharani?

sio uchaguzi wala uteuzi bali ni 'makabidhiano!' bado hujaelewa tu?
 
Kabla ya mengine, mimi nataka kujua huko Dodoma kunaenda kufanyika uchaguzi au uteuzi? Ni kipi kati ya hivyo viwili kipo kikatiba? Kama ni uchaguzi, mbona sioni faida au/na hasara za mgombea mwingine zaidi ya JPM zikichambuliwa hadharani?
Usiwe mvivu, ratiba ipo, soma ujue nini kitafanyika
 
JPM lazima awe mwenyekiti,mlizoea vya kunyonga.
Hakuna anaye pinga hilo kwa sabb limo nda ya katiba ya ccm kwahiyo kitakachofanyika Ddm ni kukamilisha utaratibu wa kupokea kijiti sema safari hii mambo yameharakishwa tofauti na ilivokuwa imezoeleka kiasi cha kuibua mijadala ya kulikoni uharaka huu.
 
Kabla ya mengine, mimi nataka kujua huko Dodoma kunaenda kufanyika uchaguzi au uteuzi? Ni kipi kati ya hivyo viwili kipo kikatiba? Kama ni uchaguzi, mbona sioni faida au/na hasara za mgombea mwingine zaidi ya JPM zikichambuliwa hadharani?

Mbona ni vizuri kusubiri tu kuona; kinachofanyika ni formality. Ni uchaguzi wa Mwenyekiti na kura zitapigwa.
 
Naomba utuelezee pia kwanini kwa mara ya kwanza katika historia ya vyama vingi tunashuhudia hofu ya "rais kuwa mwenyekiti wa Ccm" imefika hadi upinzani?

Nimejaribu kudokeza mwishoni; sababu kubwa ni kwamba endapo Magufuli atafanikiwa kuisafisha CCM, na kuleta nidhamu, uwajibikaji na mwelekeo mpya wenye kusimama katika kulitumikia taifa kuna uwezekano hoja ya mwisho ya upinzani ikafa kifo cha asilia -- kwamba CCM ni ile ile. Hili linaweza kurudisha upinzani Tanzania hadi mwaka 1965.
 
Kuna wale walikuwa wakishangilia Lowassa akikatwa, safari hii Magufuli akikabidhiwa uenyekiti huenda tukawaona wakilia na kusaga meno huku wakimkumbuka Lowassa

Wale ambao wanammiss Lowassa inabidi wamfuate; walimuuza mwenzao kwa kumwambia "ulipo tupo" halafu alivyoondoka wao wakabaki wakisema "Ukiondoka Tunakusubiri". Matokeo yake sasa hawana amani na hawajui waogelee au wapige mbizi!
 
Rudi darasani @mwanakijiji kasome upya role ya chama cha siasa. Political mobilization is not synonymous to political bullying as per Pombe jp. CCM wakimpa jpm uenyekiti kuna mambo mawili yanaweza kutokea. Moja kutazaliwa chama kipya ambacho sio CCM. Mbili, wahafidhina wa CCM wanaweza waka-sabotage CCM. Huwezi kuacha nje watu kama wakina Emanuel Nchimbi halafu utegemee kubaki salama.

Ushawahi kusikia neno "mkwara Mbuzi"? E.N ana nafasi gani; tayari ameonesha si mtu wa kupima mambo kwa hekima inayostahili. Na watu wasichokiua ni kuwa chama kipya inawezekana kabisa kilizaliwa siku Magufuli aliposhindaa Urais. Akipewa Uenyekiti chama hicho kipya kinaweza kuthibitika. We subiria uone ni wangapi na kina nani wanaamua kustaafu siasa ndani ya CCM.
 
Talking about a single point of failure, pishia mbali isitokee, lakini sote ni watu, tuna uwezekano wa kupigwa daflao na kuanguka. Kwa nini tunataka likitokea hilo kwa mtu mmoja liwe na impact kubwa sana kwa chama na serikali?

Impact gani kubwa sana wakati kuna line of succession?

Hakuna makamu wa rais?

Hakuna makamu mwenyekiti wa chama?
 
DPia wana kila sababu ya kujiuliza kwanini wakati wanachama wenyewe wakijiuliza juu ya uongozi unaoandaliwa kwanini wapinzani wanaushabikia sana uongozi unaokuja! Kuna nini la manufaa kwao? Kama alivyosema JPM mwenyewe ukiona adui anakushangilia jiulize!!

Sidhani kama wapo viongozi wa upinzani ambao wanafurahia Magufuli kupewa Uenyekiti; kwa wananchi wa kawaida ambao wameunga mkono upinzani (kama mimi) suala la Magufuli kupewa Uenyekiti ni zuri kwani tunajua atafanya nini huko. Serikali ya Tanzania ilikuwa inaugua kwa muda mrefu; sasa tangu aingie amekuwa akishughulikia dalili (symptoms) akipewa Uenyekiti ataenda kushughulikia chanzo (cause). Kwa wapenda mabadiliko wa kweli kama mimi hili ni jambo jema kwa Taifa.
 
Kwani wewe humjui Mzee Mwanakijiji kuwa ni mwandishi mkubwa wa makala?

Pia alikuwa ni miongoni ya waliokuwa wanaipinga CCM kwa nguvu zao zote....
Ila mwaka jana baada ya jina la Dr wa mihogo kukatwa kule CDM akaamua kuingia msituni......

Huku ni kurahisisha mambo; inawezekana umejiambia hivyo lakini bila ya shaka hujawahi kutafakari sababu hasa za sisi wengine kukataa mabadiliko feki ni nini hasa.
 
Mwanakiji anajipendekeza kwa Magu...ongeza kasi bro utafikiriwa.

Tatizo lako inawezekana unaamini kabisa kuwa mtu akiandika jambo fulani basi ni lazima awe anajipendekeza; sasa wewe utakuwa unajipendekeza kwa nani?
 
Impact gani kubwa sana wakati kuna line of succession?

Hakuna makamu wa rais?

Hakuna makamu mwenyekiti wa chama?
Whatever the intrigue involved in the succession is doubled if the CCM president is also the president.

Why put all your eggs in the same basket if you could hedge against that?

I generally think creating a single point of failure unnecessarily is inadvisable.

Rais akienda likizo maana yake kuna mambo fulani yatamsubiri serikalini na chamani.

Why do we need to make a demigod out of a man?
 
Ni vema bro Magu akiwa mwenyekiti....ccm walizoea sana kulindana hata kama wakiwa na makosa, sasa kwa Bro Magu hilo hana ndio maana wanahaha...waache wafu wawazike wafu wao...
 
Kwa kifupi hoja zote ulizozielezea ni za msingi sana lakini hazina mashiko hata kidogo katika hali ya kiuchumi, kisiasa na kijamii tuliyo nayo kwa sasa, nasikitika kusema kwamba hao "political deadwoods" wanatumia sababu nzuri kuhalalisha nia OVU, agenda yao ni inaongozwa na "self defence mechanism" ili kulinda maslahi yao binafsi na sio taifa katika ujumla wake! Predictability ndio imejenga na kulea "culture ya impunity na business as usual" katika utumishi wa umma, si wanajua jamaa atachekacheka na kuishia kupiga vijembe na mipasho tu akiacha nchi ikiteketea na watu wanaiba hovyo hovyo left right, top bottom and centre! Nchi inahitaji attributes za Magufuli ili kuizindua kwenye mdororo wa
muda mrefu uliosababishwa na ccm na
makada hao hao wanaosema leo JPM
asipewe Uenyekiti! nchi inahitaji shock therapy ili kuuzindua moyo wa nchi isife kabisa. Go go JPM.
 
Back
Top Bottom