Wenye elimu watabaki kuwa 'superior class' kwenye jamii na wasio na elimu watabaki kuwa 'inferior class'

zagarinojo

JF-Expert Member
Jul 26, 2020
2,622
2,835
Habari wanajamii Forums!

Jamii imegawanyika kwa makundi na matabaka tuchulie kwa kama mfano

Walio na elimu na wale wasio na elimu.

Kwenye jamii ya sasa hakuna uwiano uliopo katika maisha ya watu (Walio na elimu na wasio na elimu).

Jamii yetu ya leo inawaheshimu na kuwapa thamani watu walio na elimu huku ikiwatenga wale wasio na elimu pasi kujua wao nao ni sehemu kubwa ya maisha na maendeleo ya jamii.

Wenye elimu hupata kazi nzuri zenye mishahara mikubwa na husikilizwa pale wanapotoa hoja na mijadala katika nyanja tofauti za maisha.

Tuchukulie mfano kilimo ambayo ni sekta ambayo inachangia sehemu kubwa ya pato la taifa.

Wakulima wengi wanaiwezesha serikali kupata fedha ambazo nyingine hutumika katika wizara ya elimu kutoa mikopo kwa wanavyuo
Lakini wakulima hao wengi wao hawana elimu.

Wenye elimu wataendelea kuwa superior class kwasababu hata company yao na watu wao wa karibu pia wanaelimu hivyo mnyororo utaendelea mpaka mwisho.

Lakini wasio na elimu company yao ni ya watu wenye hadhi kama yao hivyo mnyororo wa ujinga utaendelea kuwepo kwao.

Nafasi ya watu wenye elimu ni kubwa kwenye jamii kuliko ya wale wasio na elimu kwasababu mazingira na mfumo wa maisha Una wa favor walio na elimu.

Hivyo, wenye elimu watabaki kuwa SUPERIOR CLASS na wasio na elimu watabaki kuwa INFERIOR CLASS.
 
Unazungumzia wenye elimu gani au ni hawa hawa wanaotumwa kazi kwa mshahara usiofika hata milioni kwa mwezi, Binafsi mtu mwenye hela ndo ninamhesabu kuwa mwenye elimu ila mwenye elimu asiye na pesa namuona kama kilaza wengine tu, maana elimu yake kashindwa kuibadili kuwa pesa.
 
Mkifika 40+ wenye elimu na wasio na elimu wote wanakua level sawa.

Superior class inakua mwenye pesa ndio ataheshimika katika jamii.
 
Kuna tofauti kati ya elimu na akili. Samahani wewe mleta hii hoja ni nshomile aka Muhaya?
 
Superiority mpaka rohoni na kwenye utu wa kimàadili?

Maana Wasomi wengi tu Ni matapeli wa kalamu ...wamejaa mpaka kwenye "siasa zetu"

Mimi pia Msomi na role model wangu ni Aina ya watu Kama Nyerere.

Karibu hapa Kijiweni tunywe Al kasus,nimezungukwa na WASOMI Wasio na MIKARATASI MIVYETI.

#Mpiga Spana Ujinga
 
Akili zinatofautiana kutokana na mazingira ndo maana hata shule wapo wanaoweza maths,wengi bios wengine geography
Unachanganya mambo akili siyo lazima uwe na elimu lakini elimu ni lazima uwe na akili sasa kwa kiwango gani ndio inategemea na kiasi cha akili ulichojaaliwa katika ubongo wako.
 
Back
Top Bottom