Wenye elimu ndogo ndio wanapenda kuvaa-vaa vizuri na kupendeza

Nichumu Nibebike

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
8,658
15,784
Wasomi wala hawaangaikagi sana na kupendeza pendeza, labda ni kwa sababu kulingana na Maslow's hierarchical of needs, hilo sio tena suala la kipaumbele kwao..

Ila sasa wenzangu na mimi wale wenye elimu ya tia maji tia maji, ndio huwa wanapenda kupiga pamba mwanzo mwisho ili kuboost reputation zao... Wengine huenda mbali zaidi na kuweka staili za ajabu ajabu za nywele. Kama unabishana na utafiti huu angalia watu wenye elimu ndogo kama Ali Kiba, Diamond, Ray Kigosi, Hemed PhD, Geemodel and the like...

Ukitoka hapo waangalie wasomi nguli kama Prof Lipumba, Dr... Mapad Lock, yule baba wa watu yeye yuko bize na hapa kazi tu, wala hanaga muda wa kujiremba remba sana... :D:D:D
=====

Tazama mjadala kuhusu mada hii ukisomwa JamiiLeo
 
Hao waliosoma ungejua ndiyo wanaringishiana vya USA, Italy na UK huko maofisini, tena wakitoka mikutanoni.
 
Hauna ukweli huo utafiti wako.labda kwa wasomi wa bongo tu ndio hawapendi kuvaa vizuri.kwasabu niwabahil,wanapokea mshahara mdogo usiokidhi mahitaji yao.watu wenye elimu ndogo ni watu wa madili.Mshiko wao hausubiri mwisho wa mwezi.Mshiko kwao wakati wowote wanaukamata.
 
Sio suala la elimu tu ila mtu yeyote mwenye IQ kubwa huwa anavaa kawaida sana. Sio mtu waku mind kujipodoa. wapo ambao hawana elimu kubwa ila IQ ni Kubwa.

Kuna msanii mmoja wa movie amekuwa mweupe sababu ya kunywa maji mengi, ona jinsi alivyo mtanashati/very smart, mwisho zaidi katoboa masikio.

Hata mliopo mashuleni na vyuo utakuta wanafunzi wenye dress code za kawaida ndio wanaofanya vizuri academically na masharobaro wao nikunukia perfume tu.

Hata makazini utakuta wakawaida ndio wenye ufanisi mzuri zaidi na hata kwenye vikao wanatoa hoja zenye mashiko, ila wazee wa kupiga pamba na scrabble usoni hata aambiwe achangie mada yeye atasema " naona alichosema Jerald ni sahihi", kiukweli watanashati wengi sio smart kichwani
 
umefanya comparison ya watu ambao sio
Wanamuziki wanavaa flashy sababu ya kazi yao, wanaangaliwa kila mara, so wanajiweka kitofauti tofauti ili kuwa na muonekano wa tofauti na kuvutia kila mara kwa mashabiki wao

Ila nakubali kwa watu kwenye kada mbili zinazofanana, mfano wote ni wafanyakazi wa kawaida ukiwapa kiasi sawa cha fedha wenye elimu kidogo wataitumia kwenye consumption ya vyakula, vinywaji, mavazi, na accessories nyingine ila wenye elimu kubwa huwa sio social sana hivyo consumption yao itakuwa less kwenye hayo mambo
 
Sio suala la elimu tu ila mtu yeyote mwenye IQ kubwa huwa anavaa kawaida sana. Sio mtu waku mind kujipodoa. wapo ambao hawana elimu kubwa ila IQ ni Kubwa.

Kuna msanii mmoja wa movie amekuwa mweupe sababu ya kunywa maji mengi, ona jinsi alivyo mtanashati/very smart, mwisho zaidi katoboa masikio.
Mao na IQ yake kubwa lakini suti zake zimekuwa dress code ya wengi.
 
Wasomi wala hawaangaikagi sana na kupendeza pendeza, labda ni kwa sababu kulingana na Maslow's hierarchical of needs, hilo sio tena suala la kipaumbele kwao..

Ila sasa wenzangu na mimi wale wenye elimu ya tia maji tia maji, ndio huwa wanapenda kupiga pamba mwanzo mwisho ili kuboost reputation zao... Wengine huenda mbali zaidi na kuweka staili za ajabu ajabu za nywele. Kama unabishana na utafiti huu angalia watu wenye elimu ndogo kama Ali Kiba, Diamond, Ray Kigosi, Hemed PhD, Geemodel and the like...

Ukitoka hapo waangalie wasomi nguli kama Prof Lipumba, Dr... Mapad Lock, yule baba wa watu yeye yuko bize na hapa kazi tu, wala hanaga muda wa kujiremba remba sana... :D:D:D
Unapo linganisha kitu Ni lazima uwe Na benchmark, hao wasanii ambao ww unaona hawana elimu ungewalinganisha Na wale wenye elimu., hali kadhalika Na kwa wana siasa vilevile. Pia kuwe Na cut off point Kati ya wenye elimu Na sifa zao Na wasio Na elimu Na sifa zao.
 
Nguo nzuri zinatambulikaje? Kama ni gharama,umewahi uliza mashati wanayovaa hao waheshimiwa uliowataja...
 
Wasomi wengi ni wachafu unaweza mkuta profesa amevaa suti na ndala
 
Hauna ukweli huo utafiti wako.labda kwa wasomi wa bongo tu ndio hawapendi kuvaa vizuri.kwasabu niwabahil,wanapokea mshahara mdogo usiokidhi mahitaji yao.watu wenye elimu ndogo ni watu wa madili.Mshiko wao hausubiri mwisho wa mwezi.Mshiko kwao wakati wowote wanaukamata.
wapo watanashati ambao wana elimu kubwa na IQ kubwa ila ni wachache sana.
Tuna uzoefu wa USA, Europe na hata Uarabuni. Kuna mtu ukiambiwa ni CEO wa idara fulani huwezi amini. Wengine wanakuwa smart kutokana na taratibu za kazini kwake tu.
 
Back
Top Bottom