moto2012
JF-Expert Member
- Jul 3, 2012
- 2,271
- 1,491
Wanaitwa Madaktari Wasaidizi, lakini pamoja na yote tunachojali ni huduma zao maana ndio wengi wamekuwa wakitutibu tangu nchi imepata uhuru mpaka sasa hivyo kwa kuwaita madaktari nadhani ni sawa tu katika mazingira ya kawaida ila wao pia taasisi wanazofanyia kazi wanajulikana kama AMO, wengine wapo makini kuliko hao tunaowaona ma-graduate kutokana na kujituma hasa ukizingatia magonjwa ambayo wengi huugua ni malaria, typhoid, kifua, kichwa, kuhara (magonjwa ambayo ni business as usual ambayo wana uzoefu nayo hata kabla ya kuwa AMO)
Tuwatie moyo tu kwani mtu mpaka anafikia kuwa Assistant Medical Officer ni mtu ambae amefaulu kiwango cha juu masomo ya sayansi ya O-level na A-level pia ila si katika kiwango cha juu sana, hivyo kwa kupitia hapo ni sehemu tu ya kuelekea elimu ya juu zaidi na wengi wao huwa wapo vizuri sana pindi wanapoamua kujiendeleza. Hii inanikumbusha miaka ya nyuma, kuna wanafunzi walikuwa wanatoka shule za ufundi kama Mazengo, Tanga, Ifunda na walikuwa wanafaulu kiwango cha juu kiasi cha kwenda A-level lakini wengi wao walikuwa hawapendi kwenda A-level badala yake wanakwenda vyuo vya ufundi na kutoka na FTC (Full Technician Certificate) na kiukweli wamefanya kazi nzuri sana kutokana na elimu waliyoipata kule chuoni na tulikuwa tunawaita Engineers though ni Technician
In this case, kibongobongo ni madaktari hawa kwa jinsi wanavyotusaidia kwani mwisho wa siku wataenda kuchukua full course ya udaktari
Kitanda usicho kilalia huwajui kunguni wake, kutokana na uhaba wa madaktari ni kweli wanafanya kazi, ila kazi zao nyingi ni za mazoea, suala la ufaulu usidanganye, fuatilia profile zao kwa karibu, wapo ambao hata kuandika majina yao ni ishu.
Kwanini wanadharaulika? Hilo ni kosa la kimfumo wa mafunzo ya udaktari kwa Tanzania, kwa nchi za wenzetu advanced diploma ya medicine haipo, tunayo sisi tu Tz, hivyo kimataifa hawatambuliki!