Wenye busara CCM fanyeni mahesabu Nape soma hii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wenye busara CCM fanyeni mahesabu Nape soma hii

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtaka Haki, Apr 20, 2012.

 1. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndani ya CCM wapo watu wengi tu wanaojua na kuona kuwa serikali yetu inaenda vibaya hasa kwenye suala zima la uwajibikaji au kuwajibishwa kwa watendaji wabovu, wezi, wala rushwa na wasiosimamia raslimali za nchi.
  Wako wengi wanakubaliana na hali hiyo kwa kuwa maslahi yao binafsi hayawezi kutimizwa nje na CCM.
  Wako wasiokubaliana na hali hiyo lakini pia malengo yao ya kisiasa hawaamini yanaweza kutimizwa nje na CCM, zikiwemo nafasi walizo nazo sasa.

  UKWELI

  Karibu kila mwenye ufahamu wa kawaida anaona na kushangaa jinsi ambavyo hata ahadi ndogo ya kawaida kwa mtawala yeyote ya kuwawajibisha wanaofanya maovu mbalimbali ndani ya serikali na ndani ya chama imekwama na haitekelezeki.
  Wimbo wa gamba umekuwa aibu na hatimaye hakuna mwenye ujasiri wa kuuimba tena. Mama au baba anayeishia kumtishia mtoto "nitakuchapa" huku hatimizi, basi mtoto hujua kuwa sio kweli na huendelea na tabia au alifanyalo.
  RADA, MEREMETA, KAGODA, KIWIRA, EPA, RICHMOND, BOT, TANESCO, NA MENGINE MENGI yamebakia kuwa kiini macho.
  UMASKINI UMEONGEZEKA NA DENI LIMEKUWA KUBWA.

  Maisha bora yamekuwa ni kwa kila fisadi, kila mwenye nafasi ya kutia sahihi mkataba uwao wowote na kila mwenye dhamana ya kuiwakilisha serikali katika jambo lihusulo fedha akiamua ana maisha bora na ana uhakika wa kuendelea.
  VIJANA vijijini na mijini hawana ajira na hawashawishiki kwa lolote kuwa maisha yao yanaweza kuwa bora bila kubadilisha chochote. Kila mtu anajua kuwa " HUWEZI KUTARAJIA MATOKEO TOFAUTI KWA KUENDELEA KUFANYA ULIVYOKUWA UKIFANYA. People who keep on doing things the same way will always get the same results they have always got."

  Ili kulinda heshima nawashauri wale wanaouchukia ufisadi kwa moyo wa kweli au wale wanaochukizwa na mwenendo mzima wa serikali basi wakati wa kuondoka ni sasa kwani ndio sauti pekee inayoeleweka katika jamii.
  Ushujaa wa pekee ni wakati huu. Kubakia kwenye Chama tawala kunapaswa kuwa ni kwa wale ambao mwisho wa harakati zao za siasa yenye nia ya kuijenga nchi yao wanakomea 2014 .
  Maamuzi yatakayofanywa huko mbele yatakuwa ya faida za kibinafsi zaidi kuliko ya nchi na wananchi.
  Pamoja na kwamba Fred Mpendazoe sio mbunge lakini historia na future yake kisiasa ni bora mara nyingi kuliko hata mawaziri wqalioko serikalini kwa sasa. MASHUJAA WALISIMAMIA NA KUAMUA KUFUATANA NA IMANI YAO HATA KAMA WALISIMAMA WENYEWE. Kusimamia haki unaweza usiwe na mfuasi, lakini kama utadumu katika lililo haki wafuasi watakufuata na kukupongeza.

  Nape kwa kuwa wewe ni Kijana nakushauri pima maji, chukua hatua Dunia itakuheshimu. Mke watoto wanaweza wasikubali, lakini historia itakuheshimu. Wewe ni kijana bado usiijibu hii kisiasa angalia moyo wako na kwa dhati ufanye maamuzi.

  UCHAGUZI ARUMERU, SONGEA , MWANZA na kwingineko tuichukue kama ni sauti ya MUNGU.
  Mh Lowasa anajulikana nguvu zake, Mkapa na wengineo wengi walioenda Arumeru Mashariki , sauti inasema nguvu yoyote huko mbele haitazidi nguvu ya uma na chuki ya maovu. Siku zote wanaochukia maovu watakuwa wengi.
  Kilango na Sitta mlishiriki kampeni za madiwani. Mnakubalika na kupendwa lakini ujumbe unasema haiwezekani tena mkiwa ndani ya CCM.
  Upepo unaonyesha wakati muafaka ni huu. Kwa kuwa maandishi haya ninaandika hapa basi nami historia itaamua kama nilikuwa sahihi au la. Mawaziri waadilifu ni wakati wa kuachia ngazi na kujiondoa hata kama mngeshindwa kwenye uchaguzi ukirudiwa lakini mtashinda moyoni kuwa mliamini na kuusimamia uadilifu. WAKO WAPI WAADILIFU WA LEO?
   
 2. g

  glojos88 Member

  #2
  Apr 20, 2012
  Joined: Jul 31, 2010
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanaotafuta heshima ya kweli ni wachache, wengi wanatafuta chakula cha leo na akiba ya baadae.
  Wenye uchungu ni wachache sana. Mashujaa wa kweli ni wachache sana. Hata baadhi ya wapinzani sio mashujaa wa kweli.
   
 3. m

  mayengo Member

  #3
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  that true kbsa mda ndio huu wa kujiunga na M4C
   
 4. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Umelonga mwuungwana ni vitendo, may our Almighty God bless you, now and forever. Amen.
   
 5. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kuna hoja hapo
   
 6. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Je unadhani ni njia gani uchukuliwe ktk kukabiliana na hili wakati ikitokea bungeni wabunge wa ccm wamekubaliana jambo na upinzani na kuanza kulipiga vita spika anaahairisha bunge na kuitisha kikao cha gafla cha magamba na pindi wanaporudi kuendelea na bunge wanarudi wakiwa wamoja kwa kutetea maovu yasiyokubalika na hata wao wenyewe ila inakuwa ni kwa shinikizo?
   
 7. M

  Manyonyo Member

  #7
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 18, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tumekusoma mzee,asiyeelewa hapa ana yake.
  Nape asome hayo na ayafanyie kazi haraka.
   
 8. j

  jjjj Senior Member

  #8
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  MTAKA YOTE.
  UMEONGEA YA MSINGI LAITI WANGEKUWA WANAYASOMA NA KUYAWEKEA MAANANI,Hii Nchi ingekuwa ya maziwa na asali
   
 9. g

  glojos88 Member

  #9
  Apr 20, 2012
  Joined: Jul 31, 2010
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nape JIBU HII. Umeombwa usijibu kisiasa hivyo ni sawa usipojibu haraka. Ila usiache kujibu
   
 10. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #10
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135


  Je Pongezi apewe Nape Nnauye?
   
 11. DCONSCIOUS

  DCONSCIOUS JF-Expert Member

  #11
  Apr 20, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,272
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Wakifukuzwa na ubunge ntampongeza lakini i ikiishia kwnye uwaziri sifa zote chadema
   
 12. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #12
  Apr 20, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hakuna hatua ya kuchukua kwani hatua yao ni kuhukumiwa na wapiga kura wao. Mbunge atakayepona ni yule ambaye atakuwa na msimamo tofauti na wenzake. Hata kama sio mwaka huu lakini huko mbeleni. Kila kipindi cha historia kuna mashujaa wake. Uamuzi wa kuwa shujaa au msaliti hufanywa na walioko katika kipindi cha historia yenyewe.
   
 13. U

  Ukombozitz Member

  #13
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Open Group mpya imefunguliwa facebook kwa jina la Ukombozi Tanzania. Unaruhusiwa kujoin pamoja na kuinvite watu mbalimbali kwenye group. Aim ni kuwa na kila mtanzania anayetumia mtandao wa internet awe kwenye hili group tayari kupashana habari pamoja na Kuikomboa nchi yetu. Ndio kwanza tumeanza kuchukua hatua sio kila siku maneno.. Jiunge na hiyo group sasa na unganisha na wenzako.


  Ukombozi Tanzania Admin
   
 14. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #14
  Apr 20, 2012
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mpaka sasa sifa zote Chadema, CCm ni mabingwa wa kudaka hoja za CDM wangejivuaje gamba kama hawakutajwa kwenye list of shame ?
  Wangefukuzaje na kuwajibisha mawaziri kama sio tishio la vote of no confidence?
  Kesho ndio waanze kuringa ni hoja yao? Hoja inakuwa yao wakati wa kutapatapa...
  Uliona tweets za makamba na Zitto ? He was openly saying ni cheap politics...

  Sasa hivi atatweet nini mnafiki huyu?
   
 15. l

  london JF-Expert Member

  #15
  Apr 20, 2012
  Joined: Sep 12, 2010
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nape dunia yote inawaangalia sasa tunataka kuona hii nadharia ya kujivua gamba mbona inawasubiri akina Chenge na Lowassa tu? Na huu ukosefu wa meno dhidi ya Chenge na Lowassa umewafanya mawaziri wawe na kiburi kuwa chama hakiwezi kuwavua gamba! Na kwa hili la kushindwa kuwang'oa gamba mawaziri wabadhirifu ndo linawachimbia kabisa kaburi ccm kuwa chama cha upinzani 2015.
   
 16. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #16
  Apr 20, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  Kule kwetu tunasema kuku ana akili kuliko nape!

  "kuku giza likianza kuingia naye anaingia ndani na si vinginenyo"
   
 17. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #17
  Apr 20, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  mama bhundala ananiambia opena iko juu ya fridge. ngoja nipige hii Kili yangu bariid ndo nikalale.
   
 18. w

  warea JF-Expert Member

  #18
  Apr 21, 2012
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waacheni watoto wa magamba, CCM ni ya babu zao, baba zao na watoto wao. Wenye akili kama Nyerere wanaondoka - maana CCM sio mama yao.
   
 19. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #19
  Apr 21, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Bado ninamsubiri Nape, angalao aseme neno moja tu. Yeye ni kijana na yeye alitangaza kuwa watavua magamba. Kama imeshindikana ni kweli na sio kumkebehi namhimiza kutoka CCM. Sekretariet iliyojiuzulu haikuwa watuhumiwa wa ufisadi.
  Wale wapacha watatu je chama chote hakuna mwenye uwezo wa kusema kitu? RADA. EPA, MEREMETA, KIWIRA, BOT, TANGOLD, RICHMOND, sasa TBS, UDA, TANESCO, Madudu wizara ya Fedha, Viwanda na Biashara, MADINI, Nk, NK.
  Kweli nakuomba uamue kuondoka kwenye chama hicho kulinda heshima ya ujana wako. Usikubali kubadilisha msimamo wako.
  Amua kuwa shujaa bila kujali cheo, sifa nk. Utavuka ukiwa shujaa. Vinginevyo utakuwa unamalizia safari yako ya kisiasa ukiwa bado mdogo na historia haitakuwa na neno jema juu yako.
   
 20. J

  JAPHETtumpa Senior Member

  #20
  Apr 21, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ana nafasi ndogo sana ya kuamua kwa sababu kwake ccm ni ni kama ukoo na kama ni zaidi ya ukoo basi ni umoja wa kifamilia.kuhama ccm ni rahisi kwa baadhi ya wana ccm sio rahisi kwa watu kama NAPE na J MAKAMBA hawa wanaamini ccm ni mali yao na nchi ni ya ccm kwa hiyo nchi ni yao ,hili jambo lipo kwenye damu zao kama sio kwenye akili zao
  zungumzia kuhusu ccm kupoteza uhalali wa kutawala hawaamini
  zungumzia kuhusu wizi wa mali za umma hawaoni hivyo maana kwao wizi huu ni wizi wa mali zao
   
Loading...