Wenye Bima ya Afya(NHIF) tunanyanyasika sana kwenye hospitali za private na Pharmacy;Serikali ipo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wenye Bima ya Afya(NHIF) tunanyanyasika sana kwenye hospitali za private na Pharmacy;Serikali ipo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Maega, Jun 25, 2012.

 1. M

  Maega Senior Member

  #1
  Jun 25, 2012
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 152
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ni jana jioni baada ya kujisikia vibaya nikaamua niende kupata matibabu kwenye hospitali ya binafsi(Private) ambayo ipo jirani na ninapoishi maeneo ya Mbezi Beach. Daktari aliniandikia dawa na nilipokwenda kuchukua dawa nikaambiwa hizo dawa zimekwisha hivyo nikajaziwa form ya kuniwezesha kuchukua dawa hzo kwenye maduka ya dawa(pharmacy). Wakati nikirudi sehemu ya kuchukulia dawa baada ya kuipeleka ile form kwa daktari hamadi Mungu si Athumani nikakuta mtu mwingine ambaye ana bima ya AAR akipewa dawa zile zile ambazo nimeambiwa zimekwisha. Nikawa mstaarabu sikuhoji nikachukua zile form nikaondoka na kwa vile ilikuwa usiku sikuweza kwenda pharmacy usiku ule.

  Leo nimezunguka kwenye pharmacy kubwa na ndogo kote wananiambia hawana mpaka kwenye duka moja nilipomuuliza muuzaji na akaniambia kuwa kwa bima ya afya(NHIF) utazunguka sana wala hakuna atakayekuuzia ila kama una cash au ungekuwa na bima nyingine kama AAR ningekuuzia kwa madai kuwa bima ya afya wanawalipa hela kidogo.

  Sasa pamoja na zile hela nyingi tunazokatwa kila mwezi kwa ajili ya NHIF ambazyo ni lazima bado tunanyanyasika kiasi hiki!!!!! Hivi serikali au hao wakuu wa NHIF wanaokula hela zetu kila mwezi hili nalo wameshindwa kulitatua? Yaani ukiwa na kadi ya NHIF ni mateso, unanyanyasika na kudharauliwa why?
   
 2. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Pole sana mtanzania mwenzangu. Hii NHIF ni tatizo, ni mateso makubwa sana. Bado imekumbatia uendeshaji mbovu wa kiserikaliserikali. Unakatwa hela nyingi hasa kama una ile green kadi na kwa hakika si kwamba unaugua kila siku but huduma zao ni mbovu sana. Nakumbuka siku walipofika ofisini kwetu ili tujiunge waliongea kwa mbwembwe ila mtumishiwe mwenzetu mmoja aliyejua huduma zao mbovu aliwaponda pale pale. Majibu yao yao yalikuwa kuwa kwa sasa huduma zimeboreshwa sana hakuna tabu, waongo na dhaifu!!! Wewe unafikiri ni kwa nini binadamu anafikia mahali anatumia misamiati kama DHAIFU? Ni mambo na uozo kama huu. Sasa basi baada ya NHIF kuanza kutoa huduma tena after 3 months tulikatwa bila huduma basi huduma kwa wale wa brown kadi ni mbovu sana na hata kwa green kadi ni mbovu kwa kuwa eti si kila huduma unatakiwa upate. Kwa mfano nimalipia over laki mbili kwa mwezi lakini kwa pesa hii kila mwezi ambapo kwa mwaka ni over 2 million na huku sina watoto wadogo wanaougua kila siku but eti siwezi kupata huduma ya miwani. Nilitaka waangalie mchango wa mtu ili niweze kupatiwa angalao miwani ya laki mbili na si kila siku kwa kuwa nachanga nyingi. Sitakubali kupewa miwani na sh, 20,000 ambayo hata frem yake ni matatizo. Matokeo yake nalazimika kununua!!! Hawana mpango mzuri wa kazi atu tusema basi kuna namna hao wahusika wanashirikiana na madaktari kula michango yetu bila huduma bora. Huko mliko NHIF msikie au ni mpaka tuanze kuandika magazetini? But mtasikia wakati mko kiserikali, you are not responsible, very irresponsible to our health and life.
   
 3. msnajo

  msnajo JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 2,464
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  Serikali ipi unaulizia kama ipo?? Hawa magoigoi ndo unaita serikali??
   
 4. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,972
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  Bima ya afya ni kimeo,hakunaga kwanza bima ya afya duniani yenye matabaka.Pia aiji hakilini mpaka leo hii Bima ya afya inatumia technologia ya mwaka 47.Mimi binafsi kadi yao nimeifanya mapambo,yupo mwanaseheria mmoja alikuwa anataka kwenda mahakamani kuprotest uwepo wake,akidai kuwa walimu wengi wanaibiwa tu michango yao,iweje mwalimu aliyeko let say Mbinga vijijini akatwe pesa kila mwezi wakati hospital yake ya karibu ipo 150 KM toka kituo chake cha kazi
   
 5. KANYIMBI

  KANYIMBI JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 312
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Kweli bro hayo manyanyaso yapo na sio tunapoenda kutibiwa hospitali za private tu, hata kwenye hizi za serekali nao hali ni hiyohiyo. Nilichogundua mimi ni kwamba bei ya hizi dawa huko kwenye pharmas zetu zimekuwa zikipanda kila mwezi, na hawa watu wa bima wa NHIF hawana utaratibu wa kubadilisha mapema viwango vyao vya malipo ya dawa. Hali hii ndiyo inayowafanya wakati huu wawe hawana inshu. Wanaouza dawa huwa wanaangalia faida na sio hasara. Nawashauri wahusika wa huu mfuko wawe wepesi kwenda na wakati, rekebisheni viwango vya malipo yenu ili wafanyakazi waone faida ya hayo makato yenu.
   
Loading...