Wenye bar acheni kuweka vyoo vichache wakati wateja ni wengi

Afisa Mteule Drj 2

JF-Expert Member
Mar 21, 2017
3,586
3,935
Habari watanzania wenzangu,

Hoja yangu ya msingi ni kuhusu hawa wenye bar. Unakuta bar nzuri ina wateja wengi kuna kila aina ya chakula kipo hapo.

Tatizo lipo kwenye uchache wa vyoo unakuta bar ina vyoo viwili tu kwa ajili ya wale wa haja kubwa.

Ukiingia tu chooni hujaanza kutumia mtu kagonga mlango unakuta watu kama kumi wanakusubiri utoke waingie.

Wenye bar tafadhalini mtusaidie kwa hilo tunapata sana shida wateja.
Mamlaka mnazotoa vibali tusaidieni kwa hilo. Nahitaja bar moja ambayo ina wateja wengi lakini vyoo vya kwa ajili ya haja kubwa ni viwili tu.

Bar hii inaitwa yenu bar ipo Ubungo ipo karibu na mataa pale opposite na kituo cha mwendokasi kilichopo TANESCO.

Hapa unoko unoko tu
 
Naunga mkono hoja..!inauzi sana..!umetoka kula mdudu kilo,upo bia ya 6..wasikia gogo linakuja..!unategemea nin?bar nyingi wana vyoo vichache kama sio kimoja!?ni viwili vya kukata gogo..!ili pia ni jibu.
 
usiwe na wasiwasi, hii bar karibu itavunjwa kupidha interjection, ila jitahidi kuacha mizigo yako nyumbani kwako

Hivi mbona huelewi,uko bar tuseme bar iko ubungo umekula chakula pale ukabanwa na haja kubwa halafu kwako tuseme kwako ni mbagala ina maana utasubiri ukanye mbagala wakati mzigo unagonga marinda?,ndio nyie mnajinyeaga kwenye madaladala mnaanza kusumbua watu na harufu za ajabuajabu wakati ingiwezekana kunya hukohuko bar aseee
 
Nakunywa pombe huu ni mwaka wa 21 sasa lakini sijawahi kukata Gogo bar. Namaliza kabisa kabla sijaondoka. Hebu jaribu hiyo tuone.

Wengine si mnamalizaga humo humo kwenye suruali,kuna kesi nyingi za watu kuwa na harufu zisizoeleweka mzoga si mzoga,itakuwa ndio nyie
 
Hujawahi kupatwa na tumbo la kuhara ghafla dogo ndo maana unayasema haya.uumwe tumbo ghafla nyumbani kwako km2 nakuhakikishia kwako hufiki na hiko choo cha bar utakiona kisafi kama choo cha Kilimanjaro Hotel au Sheraton.

Nisaidie mkuu kumuelimisha huyo mkuu maana itakuwa ubongo wake utakuwa umelowa
 
Habari watanzania wenzangu.Hoja yangu ya msingi ni kuhusu hawa wenye bar.Unakuta bar nzuri ina wateja wengi kuna kila aina ya chakula kipo hapo.Tatizo lipo kwenye uchache wa vyoo unakuta bar ina vyoo viwili tu kwa ajili ya wale wanaoshusha mizigo mikubwa(haja kubwa).Ukiingia tu chooni hujaanza kushusha mzigo mtu kagonga mlango unakuta watu kama kumi wanakusubiri utoke waingie.Wenye bar tafadhalini mtusaidi kwa hilo tunapata sana shida wateja.
Mamlaka mnazotoa vibali tusaidieni kwa hilo.Naitaja bar moja ambayo ina wateja wengi lakini vyoo vya kushusha mizigo mikubwa ni viwili tu.Bar hii inaitwa Yenu bar ipo ubungo ipo karibu na mataa pale opposite na kituo cha mwendokasi kilichopo tannesco.Hapa unoko unoko tu
kanye kwako mkuu,maana watu wengine unakuta anakunywa maji tu lakini kila dakika anaenda kukata gogo!
 
Kuna bar nilienda masasi mjini.ni bar nzuri verey executive.ebwana pahala pa haja ndogo inaangaliana na pahaja kubwa na hakuna mlango.nilichoka ikabidi niende stand kujistil.kweli kuna shida
 
Habari watanzania wenzangu.Hoja yangu ya msingi ni kuhusu hawa wenye bar.Unakuta bar nzuri ina wateja wengi kuna kila aina ya chakula kipo hapo.Tatizo lipo kwenye uchache wa vyoo unakuta bar ina vyoo viwili tu kwa ajili ya wale wanaoshusha mizigo mikubwa(haja kubwa).Ukiingia tu chooni hujaanza kushusha mzigo mtu kagonga mlango unakuta watu kama kumi wanakusubiri utoke waingie.Wenye bar tafadhalini mtusaidi kwa hilo tunapata sana shida wateja.
Mamlaka mnazotoa vibali tusaidieni kwa hilo.Naitaja bar moja ambayo ina wateja wengi lakini vyoo vya kushusha mizigo mikubwa ni viwili tu.Bar hii inaitwa Yenu bar ipo ubungo ipo karibu na mataa pale opposite na kituo cha mwendokasi kilichopo tannesco.Hapa unoko unoko tu

Duh..Mkuu umenikumbusha mbali sana. Kitambo! Hiyo bar tulikuwa kila tukipata boom tunapita tunagonga vyombo tukitoka lecture za jioni! Bado ipo? Na ile ya Sisimizi kulikuwa na kitimoto moja matata sana! Jamani kweli siku hazigandi.....
 
Back
Top Bottom