OMUSILANGA
JF-Expert Member
- Jan 25, 2012
- 384
- 227
Ndiyo wakuu, heshima kwenu!
Jana jiji la Mwanza na viunga vyake limezidi kujidhihirisha kuwa bado ni ngome ya CHADEMA baada ya umati mkubwa kuhudhuria mkutano wa cdm ulio ongozwa na Makamanda Wenje na Mnyilka. Katika mkutano huo, vijana wawili ambao ni wahanga wa mashambulizi na uvamizi wa mgambo wa jiji la mwanza i.e. majeruhi na walemavu walijitokeza mbele ya jukwaa.
Mmojawapo alipigwa risasi 3 mwaka jana sehemu za kiunoni ,kwa sasa amekuwa mlemavu wa maisha, hawezi tembea pekee yake mpaka apate msaada wa kubebwa, ana mke na watoto, matibabu yake yana hitaji milioni 16. Mwingine alipigwa risasi mkono wa kulia mwezi uliopita ambapo risasi ilitoka kwa matundu matatu, mkono wake bado umefungwa piopi lakini kwa maelezo ya madaktari ni kuwa uwezekano wa kupona haupo.
Wakati wahanga hao wakitoa maelezo ghafla umati ulio kuwepo ukiongozwa na Wenje ulianza kutoa vilio na machozi kama simanzi kwa vitendo hivi vya kikatili wanavyo fanyiwa watanzania wasio na hatia.
Jumla ya laki kama 6 hivi zilipatikana ndani ya muda mfupi kama pesa ya kuwasaidia wakati utaratibu unafanyika wa kuwasaidia. Vilevile Kamanda Wenje alitoa madawati 400 kama mpango mkakati wa kupunguza tatizo la madawati hapa jijini ambalo ccm kwa muda wote hawa kuthubutu. Pesa ya madawati hayo ni matokeo ya harambee iliyofanyika mwezi wa 4 mwaka huu chini ya Laira Odinga kama mgeni rasmi ambapo jumla takribani milioni 16 zilipatikana.
Pia katika mkutano Kamanda Wenje na wananchi wa jiji la Mwanza wali azimia kumukataa Mkurugenzi wa jiji, Willison Kabwe ambae ameonekana kama mratibu mkuu wa kuihujumu CHADEMA na kuratibu uvamizi kwa wamachinga bila taarifa ambapo hali hii imekuwa ikihatarisha amani, maisha ya watu, mali za watu na ustawi wa jiji. Hivyo Wenje chini ya nguvu ya umma ametoa siku 14 ambapo barua ya kumwomba Waziri mkuu pamoja sahihi /signatures za wananchi itatumwa ili ahamishwe hapa mwanza, kama itashindikana basi wananchi walisema watafanya kama Misiri.
Mwisho, ilitangazwa kuwa 30.11.2012 kutakuwa na uzinduzi wa M4C Mwanza live Gold crest.