Wenje na Mnyika walitikisa Nyamagana-Mwanza Jana jioni...

O

OMUSILANGA

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Messages
384
Points
0
O

OMUSILANGA

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2012
384 0
Ndiyo wakuu, heshima kwenu!

Jana jiji la Mwanza na viunga vyake limezidi kujidhihirisha kuwa bado ni ngome ya CHADEMA baada ya umati mkubwa kuhudhuria mkutano wa cdm ulio ongozwa na Makamanda Wenje na Mnyilka. Katika mkutano huo, vijana wawili ambao ni wahanga wa mashambulizi na uvamizi wa mgambo wa jiji la mwanza i.e. majeruhi na walemavu walijitokeza mbele ya jukwaa.

Mmojawapo alipigwa risasi 3 mwaka jana sehemu za kiunoni ,kwa sasa amekuwa mlemavu wa maisha, hawezi tembea pekee yake mpaka apate msaada wa kubebwa, ana mke na watoto, matibabu yake yana hitaji milioni 16. Mwingine alipigwa risasi mkono wa kulia mwezi uliopita ambapo risasi ilitoka kwa matundu matatu, mkono wake bado umefungwa piopi lakini kwa maelezo ya madaktari ni kuwa uwezekano wa kupona haupo.

Wakati wahanga hao wakitoa maelezo ghafla umati ulio kuwepo ukiongozwa na Wenje ulianza kutoa vilio na machozi kama simanzi kwa vitendo hivi vya kikatili wanavyo fanyiwa watanzania wasio na hatia.

Jumla ya laki kama 6 hivi zilipatikana ndani ya muda mfupi kama pesa ya kuwasaidia wakati utaratibu unafanyika wa kuwasaidia. Vilevile Kamanda Wenje alitoa madawati 400 kama mpango mkakati wa kupunguza tatizo la madawati hapa jijini ambalo ccm kwa muda wote hawa kuthubutu. Pesa ya madawati hayo ni matokeo ya harambee iliyofanyika mwezi wa 4 mwaka huu chini ya Laira Odinga kama mgeni rasmi ambapo jumla takribani milioni 16 zilipatikana.

Pia katika mkutano Kamanda Wenje na wananchi wa jiji la Mwanza wali azimia kumukataa Mkurugenzi wa jiji, Willison Kabwe ambae ameonekana kama mratibu mkuu wa kuihujumu CHADEMA na kuratibu uvamizi kwa wamachinga bila taarifa ambapo hali hii imekuwa ikihatarisha amani, maisha ya watu, mali za watu na ustawi wa jiji. Hivyo Wenje chini ya nguvu ya umma ametoa siku 14 ambapo barua ya kumwomba Waziri mkuu pamoja sahihi /signatures za wananchi itatumwa ili ahamishwe hapa mwanza, kama itashindikana basi wananchi walisema watafanya kama Misiri.

Mwisho, ilitangazwa kuwa 30.11.2012 kutakuwa na uzinduzi wa M4C Mwanza live Gold crest.
 
MNYISANZU

MNYISANZU

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2011
Messages
7,053
Points
1,225
MNYISANZU

MNYISANZU

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2011
7,053 1,225
Well. Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Wilson Kabwe ndiye anayewahujumu Wenje na Kiwia ili waonekane hawafai. Nashukuru wamelishtukia hilo. Glory to God.
 
Naibili

Naibili

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2011
Messages
1,680
Points
1,225
Naibili

Naibili

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2011
1,680 1,225
Mwanza bila magamba imewezekana. viva cdm
 
Filipo

Filipo

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2011
Messages
9,321
Points
1,250
Filipo

Filipo

JF-Expert Member
Joined Jan 6, 2011
9,321 1,250
Mungu ibariki M4C. Mungu ibariki cdm!
 
Arushaone

Arushaone

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2012
Messages
14,741
Points
2,000
Arushaone

Arushaone

JF-Expert Member
Joined Mar 31, 2012
14,741 2,000
Hiyo kanda ya ziwa CCM walikuwa na margin kubwa ya voters na wakawa wanawafanya misukule wa kuwakamua kwenye mauzo ya pamba na kwenye mauzo ya samaki, sasa wameamka na wamekurupuka! CHADEMA kinakutoa gizani na kukuleta mwangani unajiona. VIVA M4C!!
 
M

Mthuya

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2011
Messages
1,415
Points
1,225
M

Mthuya

JF-Expert Member
Joined Jun 9, 2011
1,415 1,225
Furumusha magamba wooooooote
 
Fpam

Fpam

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2011
Messages
290
Points
0
Fpam

Fpam

JF-Expert Member
Joined Apr 28, 2011
290 0
huyu kabwe aliharibu sana alipokuwa mbeya walichofanya baadal ya kumdemote wakampeleka mwanza
 
R

raymg

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2012
Messages
844
Points
195
R

raymg

JF-Expert Member
Joined Jun 30, 2012
844 195
Si ungefanya live coverage jana mjuu!
 
Marire

Marire

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2012
Messages
11,849
Points
2,000
Marire

Marire

JF-Expert Member
Joined May 1, 2012
11,849 2,000
Jana kwenye viwanja vya sahara mwanza ,mbunge Wenje,alikabidhi madawati mia nne zilizotokana na harambee,nampa hongera kwani nilikuwa mmoja wa watu niliokuwa na wasiwasi kuwa alikula pesa hizo.katika mkutano huo mkubwa alikuwepo mbunge John Mnyika na kwa pamoja walimpa siku kumi na nne mkurugenzi wa jiji awe ameachia ngazi kotokana na kulivuruga jiji na tofauti na hapo nguvu ya umma itafanya kazi yake.
 
Marire

Marire

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2012
Messages
11,849
Points
2,000
Marire

Marire

JF-Expert Member
Joined May 1, 2012
11,849 2,000
Ugomvi wenu na meya matata vp?
matata alituma vijana waje wavuruge mkutano kwa kurusha mawe na walifanya hivyo ila kipondo walichokipata hawatakaa wasahau,na matata kuna msg alimtumia wenje ya kumtishia maisha ilisomwa mkutanoni na wenje amepanga kumfungulia mashitaka,hakika watu walikuwa ni wengi sana!
 
KakaJambazi

KakaJambazi

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2009
Messages
16,259
Points
2,000
KakaJambazi

KakaJambazi

JF-Expert Member
Joined Jun 5, 2009
16,259 2,000
Ufunguzi wa M4C "Gold Crest" ndo kwenye walakini. Wamachinga na walalahoi wangapi watahudhuria?
Kwanini wasifanye kwenye viwanja vya furahisha?
 
Kimagege

Kimagege

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2010
Messages
283
Points
195
Kimagege

Kimagege

JF-Expert Member
Joined Oct 28, 2010
283 195
hiyo ndio kazi ya watu makini na si kupita vijiweni na kuanza kutangaza ooh mm ntagombea urais sijui ubunge sijui nmke wa mtu .wajibika majukumu yatakuja kadiri unavyoonyesha kuyamudu uliyopewa sasa.
 
J

jigoku

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2011
Messages
2,397
Points
1,250
J

jigoku

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2011
2,397 1,250
matata alituma vijana waje wavuruge mkutano kwa kurusha mawe na walifanya hivyo ila kipondo walichokipata hawatakaa wasahau,na matata kuna msg alimtumia wenje ya kumtishia maisha ilisomwa mkutanoni na wenje amepanga kumfungulia mashitaka,hakika watu walikuwa ni wengi sana!
Mkuu nimelazimika ku-quote post yako ili niweke msisitizo juu ya utata wa Matata.kwa wakazi wa MWZ wa siku nyingi hakika ni mashuhuda wazuri juu ya tabia tata za Matata tangu enzi hizo,kiukweli nilishangaa sana alipoibukia CDM,nilishituka sana ila nikasema labda kwa kuwa ni binadamu huenda amejirekebisha,kumbe huenda ni kweli jasiri haaschi asli,huyu ni mtu hatari san na dhani pia alikuja CDM kama mamluki,tabia ya huyu ndugu ni tata tangu kioindi cha miaka ya 1985-1991 ningali MWZ naijua,yeye dhuluma ni zake,magendo alikuwa ni mahiri,matumizi ya silaha kupata kitu anachokihitaji haikuwa tatizo kwake,magendo kupitia ziwa victoria-kisumu na Kampala alikuwa ni mahiri kwa smuggling,na huko majini inasadikika alizamisha majini watu wengi tu.anyway sitaki kuwasadikisha ,mlioko mwanza mnaweza kufanya mahojiano na watu wa siku nyingi mwanza watakuambieni huyo alikuwa na tabia za namna gani.
Ila kama anadhani atapambana na nguvu ya umma basi na aendelee,najua analipa watu fedha ili wakivuruge chama lkn hakika atashindwa.
 
Tutor B

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Messages
8,925
Points
2,000
Tutor B

Tutor B

JF-Expert Member
Joined Jun 11, 2011
8,925 2,000

Hujakosea! tabia zake mbaya ndo zilizoifanya Club yake ya Magnum kudorora hadi kuwa kama pagala. Ilikuwa ukienda na kimwana mzuri magnum - anawaagiza mabaunsa wake wanakufanyia fujo then anamchukua huyo kimwana. Mwanza nzima hakuna asiyejua hilo.
 
WABHEJASANA

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2011
Messages
4,225
Points
1,195
Age
40
WABHEJASANA

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Joined Jun 22, 2011
4,225 1,195
Hili si la muhimu sana kwa sasa!!!!!!!
 
J

jigoku

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2011
Messages
2,397
Points
1,250
J

jigoku

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2011
2,397 1,250
Hujakosea! tabia zake mbaya ndo zilizoifanya Club yake ya Magnum kudorora hadi kuwa kama pagala. Ilikuwa ukienda na kimwana mzuri magnum - anawaagiza mabaunsa wake wanakufanyia fujo then anamchukua huyo kimwana. Mwanza nzima hakuna asiyejua hilo.
Tutor hapo umenena ukweli,ana historia hiyo ya kudandia vimwana wa watu.alishawahi kufukuzana kwenye gari akiwa na bastola akimkimbiza marehemu(D) mtoto wa tajiri mmoja wa enzi hizo wakapita mitaa ya isamilo huko akapotezwa njia.fuatilieni kwa mlioko huko mwaulize wenyeji watawaambia,nadhani alipata udiwani kwa upepo wa CDM.
 
W

wauwau

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Messages
705
Points
170
W

wauwau

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2012
705 170
Hayo ya Matata yamekuja hapa na siku zote alipokuwa cdm damu mbona hamkusuma, cdm wa Tanganyika wanafiki, kesho na kesho kutwa slaa akirudi alikotoka au pengine atakosa pa kutokea, maana nyie siwaelewi siju mkoje. People Always Told Me Be Careful Of What They Do and Talk And Don't Go Around Breaking others peoples Hearts like fuuls And Mother Always Told Me Be Careful Of Who I'm Talking to. Maana si ajabu naongea au nawaambia misukule humu ndani
 
B

Bobuk

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2010
Messages
5,875
Points
1,500
B

Bobuk

JF-Expert Member
Joined Oct 8, 2010
5,875 1,500
Tutor hapo umenena ukweli,ana historia hiyo ya kudandia vimwana wa watu.alishawahi kufukuzana kwenye gari akiwa na bastola akimkimbiza marehemu(D) mtoto wa tajiri mmoja wa enzi hizo wakapita mitaa ya isamilo huko akapotezwa njia.fuatilieni kwa mlioko huko mwaulize wenyeji watawaambia,nadhani alipata udiwani kwa upepo wa CDM.
Niliwahi kuandika tabia za Matata hapa JF. BTW Mwanza anajulikana kama MAGNUM. Kwamba Matata ni EX-Jambawazi amefanya sana mauaji ziwa Victoria wakati huo akifanya biashara ya magendo ya bia kutoka Kisumu Kenya. Enzi hizo za Majani beach Pansisia (around 1985?) ikifika saa sita usiku bia tunauziwa nusu bei, kumbe wakati huo ndiyo bia za magendo zinateremshwa ziwani.

Kuhusu kuchukua wasichana/wake za watu kwenye bar yake ya magnum ndiyo ulikuwa mchezo wako. Alipata huo udiwani baada ya kushindwa kura za maoni CCM na kukimbilia CDM. Mwanza hata ukiweka KICHAA CDM vs Mgombea wa CCM amini usiamini kichaa atashinda. MZA hakuna kabisa CCM.

Hiyo Bar na Guest yake ya Magnum ameijenga kwenye eneo la wazi maeneo ya Ghana. Mpaka leo iko kwenye mgogoro wa kuvunjwa. Nafikiri sasa Kabwe amempatia kazi ya kuivuruga CDM in exchange ya ku-spare hiyo Guest/Bar yake ya Magnum.
 
Forum statistics

Threads 1,285,555
Members 494,670
Posts 30,866,692
Top