Wenje na Highness wabunge CHADEMA MWANZA, msiidhalilishe CHADEMA

mimi niko pamoja na mtoa mada.mimi naishi nyakato mahandu tulikuwa hatuna barabara ya kwenda makaburini limekuja katapila kuchonga barabara ile kwa sasa tuna barabara na watu wote wamesifu kuwa diwani na mmbunge wetu wenje wanafanya kazi tulio watuma. ila bado kuna barabara ambazo hazijachongwa zingine zina hitaji marekebisho tumuulize nani? kama sio huyo huyo mmbunge aliyesifiwa. kama kuna mazuri kafanya lazima tuseme na kama kuna matatizo lazima tuseme vilevile.
 
ni sahihi rweyy. unajua watu wamekuwa washabiki kitu ambacho ni hatari. mambo ya maana hawataki kuyazungumzia hata kidogo, kisa yanawahusu viongozi wa CDM. Huku siyo kujenga, ni kuua chama baada ya mda si mrefu. Kiongozi mzuri ni yule anayekubali changamoto, kuzichukua na kuzifanyia kazi, siyo kutetea hata visivyofaa kisa una ushabiki. siyo vizuri wanacdm, kwani hakuna mwenye uwezo wa Mungu. Kama kuna watu wanataitiwa na maisha, wanamlaaumu MUNGU kwa kusema, hivi mimi nimemkosea nini MUNGU?

Si zaidi kwa wanadamu wenye mapungufu kibao?
 
kule kweli bungeni wanajibu tu kama haufutilii na wao wanakausha ila kama ni mfuatiliaji wanatekeleza, mfano mnyika (kwy mkutano wake na wananchi alituambia) aliuliza swali kuhusu viwanja vya wazi vilivyotwaaliwa na ccm na watu wengine ktk jimbo lake, lakini bungeni alijibiwa kisiasa, mnyika hakuishia hapo alimuandikia barua tena waziri ya kumtaka utekelezaji wa swali lake, hivi ninavyozungumza nimepita sinza manispaa matangazo(mabango) ya viwanja vya wazi na kutaka waliojenga waondoe na vibaki wazi kwa shughuli za jamii. na ndivyo kwa wabunge wa mwanza wanawza wakawa wanafuatilia na akafika wakati s/kali ikaja kutengeneza hiyo barabara.

kweli kweli mkuu. tunachohitaji siku zote ni kwenda sambamba na uwajibikaji. siyo kutetea. mtu akiisimamia serikali tutamsifu na akiwa na mazoea ya kurudi kwa wananchi na kuwapa mrejesho, tutamkubali zaidi na kumheshimu na kumwona anafaa zaiidi.
 
ila wenye anajitaidi kugawa pesa elfu mbili mbili na kununulia wazee kahawa pale nyegezi,buhongwa,makoroboi nk.pia anawataka watu wafunge vibanda wacheze mpira muda wa kazi.hawa ndy wabunge wetu,yeye amesha amia dar ata shem naye kamwamishaga afza
 
hizo ni tuhuma zako. Wenje anajua vijiwe vya wazee, thus kujichanganya ili kuchukua maoni yao ni jambo la kujivunia sana
 
Wana Jamvi habarini.

Jiji la Mwanza, ni jiji ambalo kwa sasa linaheshimika kwa harakati za kisiasa baada ya wabunge tena waliowahi kuwa mawaziri kubwagwa na vijana wado EZEKIEL WENJE-Nyamagana na HIGHNESS KIWIA-Ilemela. Wabunge hawa vijana, walichaguliwa kwa imani kubwa na Mwanza tuliamini wataonesha usimamizi wa rasilimali za umaa kwa manufaa ya umma.

Hali imekuwa tofauti kwa uchunguzi wangu, kwani wakati mvua zikinyesha, barabara za mitaani zile za vumbi zimekuwa kero hali inayopelekea watu kuhoji, HAWA NDO WABUNGE TULIOWACHAGUA?

Barabara ya kutoka kona ya BWIRU mpaka Nyasaka, madereva wa daladala wengi wanaikimbia kwa kuwa na mashimo. Magari yanaharibika kwa ubovu wa barabara hiyo. Na road hii ina wapiga kura, na tayari wameanza kulalama.

Barabara ya NUNDU-NYAKATO MECCO, nayo hali kadhalika. Hofu yangu ni kwamba, iwapo suluhisho halitatafutwa, basi wabunge hawa watakuwa wanawapa nafasi CCM kulitwaa tena JIJI la Mwanza.

Kulinusuru ni wao japo kuwa karibu na wananchi, kuwaelimisha kwa nini barabara hazitengenezwi na kama jamii ya eneo husika tufanyeje kuepuka hatari ya kukosa huduma ya usafiri inayotokana na uwepo wa barabara isiyopitika.

Kuendlea kujificha kwa wabunge hawa bila hata kutoa matamko kwa uzembe huu, inaonesha kwamba hawajali kwani kwa habari ya HIGHNESS alishahama na mtaa. Wakati akifanya kampeni alikuwa akilala nyumba moja iliyopo kwa Lema-Munazi, siku hizi hatumuoni pande hizo thus ametutelekeza na barabara yetu inayotutesa.

Watch out kijana, kwa ustawi wa chama.

Leo daladala zimegoma, zimesitisha huduma
 
Uliyoyasema ni kweli, kwanza barabara zote hizo ulizozitaja ziko chini ya JIji (Sio Serikali kuu).
Mwenye Jukumu la kutengeneza hizo barabara ni Jiji. FYI, Jiji la Mwanza linaongozwa na CDM. Meya
anatoka CDM. Hivyo kushindwa kutengenezwa kwa barabara hizo it is down to CDM. Hili halina
mkono wa magamba.

Kama kweli CDM wanataka waonekane wako tofauti na Magamba na wako tayari kushika dola 2015
haya matatizo yaliyomo ndani ya uwezo wao LAZIMA wayatatue bila visingizio. Kama tatizo ni
MKURUNGEZI basi wamukatae apelekwe sehemu nyingine aletwe mwingine atayekwenda na
kasi ya CDM.

Afterall moja ya maazimio ya Wana-Mwanza ilikuwa kumfukuza Mkurungezo Willison Kabwe
mara CDM watakapotwaa uongozi wa JIji, kwani alionekana dhahiri kumbemba Lau Masha
hata pale ilipoonekana dhahiri ameshindwa uchaguzi.

Swali Je ni kwanini Wenje na Highness wame compromise na Willison Kabwe?! Wametusaliti wana MZA.
Uzuri ni kwamba Wana MZA huwa hatusahau kama hawajui wawaulize marehemu Bomani, Masha, Diallo
the list goes on, Mwanza tunafahamu kutumia kura zetu vizuri.
Jamani tuelewe taratibu. Mbunge sio accounting officer, hana pesa mfukoni za kutengeneza barabara. Katika majiji yetu accounting officers ni wakurugenzi hao ndio kama makatibu wakuu wa wizara, ndio wanaoshikiria pesa zote. Hivyo wa kuwalalamikia kuhusu barabara mbovu ni hao wakurugenzi. Wenje hata apige kelele kama mkurugenzi hataki hakitatengenezwa kitu!!!!
 
HAWA WABUNGE MBONA WALISHASHINDWA KAZI HATA KABLA YA KUCHAGULIWA KUWA WABUNGE....??!!!???!!!!

HASA HUYO HIGHNESS UKIANGALIA BARABARA ZA JIMBONI KWAKE ZOTE UTAZIMIA, BARABARA ZA ISAMILO KUZUNGUKA MEDIKO RISECHI NA ISAMILO INTANESHENO SKUU, BARABARA ZA KILIMAHEWA KUELEKEA KILOLELI, MITAA YA IBUNGILO, NYAMANORO, BARABARA YA KUELEKEA PPF, KISEKE, BUSWELU MAJENGO MAPYA JILANI NA OFISI ZA MKUU WA WILAYA YA ILEMELA ZOTE HOVYO NA YEYE YUPO TU ANANG'AA NA KUKODOA MACHO.

AFADHALI KIDOGO RAFIKI YANGU WENJE ALIJARIBU KUPARUA BAADHI BARABARA ZA KATA YA BUTIMBA INGAWAJE NA YEYE BADO ANASUASUA SANA.

MNADHANI HAPO TUNA WABUNGE...!!!??? AU TUNA WA...??? :behindsofa::behindsofa: UKIZINGATIA KUWA NA HUYO HIGHNESS KAWATELEKEZA NA HIZO BARABARA ZENU ZILIZOJAA MASHIMO KAMA KIKAANGIO CHA VITUMBUA
.......!!!
 
:photo:Wana jamii,naomba ufafanuzi. WANIDHALILISHA CDM KIVIP?

CDM ni chama kinachoheshimika kwa utendaji na uwajibikaji wa viongozi wake. Watu wanawakubali kwa sababu ya kazi nzuri wanayoifanya. Sasa iwapo mtu mmoja atashindwa kutekeleza majukumu yake kwa kasi ileile ya chama, wapenzi wengi wa chama wanaweza kukichukia.

Siasa n mapambano ya kuonesha nani anaweza, nani hawezi. Hivyo iwapo ukionesha kuwa huwezi, usitegemee kufanikiwa kisiasa
 
HAWA WABUNGE MBONA WALISHASHINDWA KAZI HATA KABLA YA KUCHAGULIWA KUWA WABUNGE....??!!!???!!!!

HASA HUYO HIGHNESS UKIANGALIA BARABARA ZA JIMBONI KWAKE ZOTE UTAZIMIA, BARABARA ZA ISAMILO KUZUNGUKA MEDIKO RISECHI NA ISAMILO INTANESHENO SKUU, BARABARA ZA KILIMAHEWA KUELEKEA KILOLELI, MITAA YA IBUNGILO, NYAMANORO, BARABARA YA KUELEKEA PPF, KISEKE, BUSWELU MAJENGO MAPYA JILANI NA OFISI ZA MKUU WA WILAYA YA ILEMELA ZOTE HOVYO NA YEYE YUPO TU ANANG'AA NA KUKODOA MACHO.

AFADHALI KIDOGO RAFIKI YANGU WENJE ALIJARIBU KUPARUA BAADHI BARABARA ZA KATA YA BUTIMBA INGAWAJE NA YEYE BADO ANASUASUA SANA.

MNADHANI HAPO TUNA WABUNGE...!!!??? AU TUNA WA...??? :behindsofa::behindsofa: UKIZINGATIA KUWA NA HUYO HIGHNESS KAWATELEKEZA NA HIZO BARABARA ZENU ZILIZOJAA MASHIMO KAMA KIKAANGIO CHA VITUMBUA
.......!!!

Wemje amejitahidi sana, na anjichanganya na watu hivyo atleast watu wanaweza kujua what is going on
 
Wana Jamvi habarini.

Jiji la Mwanza, ni jiji ambalo kwa sasa linaheshimika kwa harakati za kisiasa baada ya wabunge tena waliowahi kuwa mawaziri kubwagwa na vijana wado EZEKIEL WENJE-Nyamagana na HIGHNESS KIWIA-Ilemela. Wabunge hawa vijana, walichaguliwa kwa imani kubwa na Mwanza tuliamini wataonesha usimamizi wa rasilimali za umaa kwa manufaa ya umma.

Hali imekuwa tofauti kwa uchunguzi wangu, kwani wakati mvua zikinyesha, barabara za mitaani zile za vumbi zimekuwa kero hali inayopelekea watu kuhoji, HAWA NDO WABUNGE TULIOWACHAGUA?

Barabara ya kutoka kona ya BWIRU mpaka Nyasaka, madereva wa daladala wengi wanaikimbia kwa kuwa na mashimo. Magari yanaharibika kwa ubovu wa barabara hiyo. Na road hii ina wapiga kura, na tayari wameanza kulalama.

Barabara ya NUNDU-NYAKATO MECCO, nayo hali kadhalika. Hofu yangu ni kwamba, iwapo suluhisho halitatafutwa, basi wabunge hawa watakuwa wanawapa nafasi CCM kulitwaa tena JIJI la Mwanza.

Kulinusuru ni wao japo kuwa karibu na wananchi, kuwaelimisha kwa nini barabara hazitengenezwi na kama jamii ya eneo husika tufanyeje kuepuka hatari ya kukosa huduma ya usafiri inayotokana na uwepo wa barabara isiyopitika.

Kuendlea kujificha kwa wabunge hawa bila hata kutoa matamko kwa uzembe huu, inaonesha kwamba hawajali kwani kwa habari ya HIGHNESS alishahama na mtaa. Wakati akifanya kampeni alikuwa akilala nyumba moja iliyopo kwa Lema-Munazi, siku hizi hatumuoni pande hizo thus ametutelekeza na barabara yetu inayotutesa.

Watch out kijana, kwa ustawi wa chama.

Umetoa dukuduku zako kwa ustadi mkubwa sana, nakupongeza sana kwa hilo. Binafsi nachukulia maoni yako kama mwendelezo wa Post Mortem ya mwaka mmoja wa CHADEMA kama chama chenye wabunge 45 bungeni na chama kikuu cha upinzani. Awali ya yote ni lazima tukiri kuwa kwa muda mrefu wengi wananchma na wapenzi wa CDM tulizoea kukosoa tu, hii inatokana na ukweli kuwa tulikuwa hatujakabidhiwa jukumu lolote kitaifa ili tuweze kupimwa. Kwa kuanzia watanzania wameikabidhi CDM jukmu la kuongoza nafasi za ubunge katika majimbo 23, ambayo ukichanganya na kura za urais CDM iliweza kupata wabunge 22 wa viti maalum na hivyo kufikisha jumla ya wabunge 45.

Tatizo linaloikabili CDM kucheza muziki unaopigwa na bendi iitwayo CCM, Kwa muda mrefu sana CCM imefanikiwa kuwaaaminisha wananchi kuwa jukumu kubwa la Mbunge ni kuwa tarishi wa kuleta maendeleo jimboni toka Serikali kuu. Hivyo kwa muda mrefu sasa watanzania wamekuwa wakipima ufanisi wa mbunge kwa kiwango gani cha maendeleo yaliyopatikana katika jimbo atokalo k.m barabara, maji, shule, zahanati, hospitali n.k. Kwa lugha nyingine ili mbunge aweze kukubalika na kuchaguliwa tena ni lazima awe na uwezo wa kuwahonga wananchi miradi ya maendeleo iliyotajwa.

Ghana hii potofu iliyohasisiwa kwa ustadi mkubwa na wasomi wa CCM ililenga kuwageuza wabunge (Mhimili wa Bunge) kuwa omba omba wa miradi ya maendeleo toka kwa mawaziri (Mhimili wa Serikali). Ibara ya 63 (2) inatamka kuwa "Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii".

Hivyo basi mkakati wa CCM wa kuwageuza wabunge omba omba wa maendekleo toka kwa mawaziri waioko katika (Mhimili wa Serikali) ulilenga kuwadhoofisha kutimiza majukumu yao kw amujibu wa ibara 63 (2) hapo juu, Kwani haiwezekani mbunge ampigie magoti waziri, hala fu wakati huo huo aweze kutimiza jukumu la kumsimamia ipasavyo. Athari za makakati huu wa siri wa CCM ni Seikali ya Tanzania iliyoko chini ya CCM kukosa usimamizi toka kwa wabunge ambao walipaswa kuismamia kwa niaba ya wananchi kama inavyoelekezwa na ibara 63 (2). Matokeo yake viongozi na watendaji wa serikali wamekuwa wakijiamulia kufuja fedha, mali na raslimali za taifa kwa kuwaziba midomo wabunge (walipaswa kuhakikisha fedha, mali na raslimali za watanzania vinalindwa) kwa kuwapatia marupurupu, posho n.k.

Hadi sasa hakuna mtu yeyote ambaye amewahi kunionyesha ibara yeyote ya Katiba au Sheria inayoelekeza kuwa mbunge anawajibuka na maendeleo katika jimbo lake. Kama mtu yeyote anafahamu kifungu hicho cha Katiba au sheria naomba anielimishe.

Hivyo mchawi wa watanzania ni watanzania wenyewe ambao hutumia vigezo visvyo sahihi kuwapima askari waliopaswa kuisimamia serikali ili itekeleze wajibu wake ipasavyo, kwa ufanisi, gharama ndogo n.k. Hivyo kwa maoni yangu mbunge mzuri ni yule anayweza kufahamu ni wapi Serikali itapata mapato na kiasi gani, anayeweza kusimamia mapato yaliypksanywa yatumike vizuri ili kidogo kilichopatikana kiweze kuleta maendeleo makubwa zaidi kwa watanzania waote na sio wa jimbo moja moja. Mbunge mzuri ni yule anayeweza kukagua utekelezaji wa serikali kama unakwenda samabamba na viwangi vya fedha vilivyoidhinishwa katika bajeti iliyopitishwa na bunge; na kama zipo kasoro hatua za kufa zichukuliwe ili kurekebisha kasoro hizo haraka iwezekanavyo.

kazi hiyo ni kubwa na inayohitaji masaa mengi ya utafiti, kusoma na kufuatilia hivyo kutokumuwezesha mbunge kumudu jukumu la kutafuta maendeleo ya jimbo moja moja. Aidha kansa hii ya maendeleo ya jimbo jimbo moja ndio husababisha viongozi wakuu na mawaziri kusukumia manendelko katika majimbo watakayo baada ya kukamata nyadhifa hizo.

Laiti kama wananchi wangekuwa na elimu ya uraia ya kutisha kubaini kuipongeza Serikali nzima kwa maendeleo yaliyopatikananchi nzima na kuwazawadia wabunge kwa michango na utendaji wake wenye mweleko wa kuisimamia serikali itekeleze wajibu wake kwa kuwachagua tena; kansa hii ya maendeleo ya jimbo jimbo moja moja ingefutika.

kwa kuwa CCM wanatambua mkakati huu waliouasisi muda mrefu ndio maan hung'anga;nia Tume ya Uchaguzi ili kushinda kiti cha uraiis na kuwazawadia wapinzani nafasi chache za ubunge wakiwa na uhakika kuwa kwa kuwa hawna Serikali ya kusukuma maendeleo katika majimbo waliyoshinda wapinzani hawatarejea bungeni uchaguzi ujao. Huu ndio mtegao ambao CDM wanapaswa kuutgua kwa kuwaelimisha watanzania nia aina gani ya mbunge bora kwa lengo ya kuua kansa ya maendelleo ya jimbo moja iliyoasisiwa na CCM
 
nakushukuru kwa ufafanuzi wako makini. nakubaliana na wewe. Tatizo lipo kwa wabunge pia kuamu kudanganya wananchi, mkinichagua, nitahakikisha barabara zinapitika, maji yanapatikana watoto wanaenda shule. Huu ndi msingi wa wabunge kudaiwa na wananchi kwenda kuwawakilisha kwa watendaji wa serikali ili vitu hivyo vipatikane, maisha yasonge mbele.

Kitu kingine, wabunge wetu ambao ndio wawakilishi, wanajisahau mno. mara wanapochaguliwa, wengi huhama makazi yao na kuhamia DSM, na hivyo kusimamia miradi ya maendeleo kwa remot.

wengi wao hata kurdi kwa wananchi kuwapa mrejesho wa kilichotokea mjengoni au vikao vya halimashauri, hawarudi, wako kimya. Hii nayo ni kansa. Mbunge ambaye anaamua kuwa karibu na wananchi, atayafahamu matatizo ya wananchi na kwa kuwa ni lobying and advocacy agency, atafikisha mawazo ya wananchi mahali panahusika.

Lakini pia, tungependa wabunge wetu hawa tunao wachagua kuprove kuwa wako tofauti na CCM. Uwakilishi wao uonekane, na sio uonekane wakati wa kuja kuomba kura.

Kwa pamoja, tutaweza kuwasimami wabunge/madiwani wetu. kwani ndo watu pekee waliobeba dhana ya utumishi wa umma kwa kuwa wanawajibika moja kwa moja kwa umma uliowachagua.

kwani mbunge hawezi kumkumbusha meya? Nani afuatilie kwa meya, wananchi au mwakilishi wao!!!! tafakari vizuri, kwani iwapo barabara zinakuwa mbovu halafu mbunge kakool, kinachofuata ni kupoteza Imani naye. Na hapa ni yeye na diwani wake, kulala kwao kutatukost wapenda maendeleoa

Kama Meya na Mkurugenzi wa jji wanafanya hujuma mbunge anafanyaje? Hukumbuki mgao wa umeme ulivyokuwa ''special'' kwa Mwanza na Arusha?
 
wewe unajua kazi ya mbunge ni ipi kama hawezi kusimamia mawasiliano jimboni kwake? au un azani ubunge ni uanaharakati? hawa jamaa tunawapenda ila hawajui kwa nini waliomba ubunge.
 
Wana Jamvi habarini.

Jiji la Mwanza, ni jiji ambalo kwa sasa linaheshimika kwa harakati za kisiasa baada ya wabunge tena waliowahi kuwa mawaziri kubwagwa na vijana wado EZEKIEL WENJE-Nyamagana na HIGHNESS KIWIA-Ilemela. Wabunge hawa vijana, walichaguliwa kwa imani kubwa na Mwanza tuliamini wataonesha usimamizi wa rasilimali za umaa kwa manufaa ya umma.

Hali imekuwa tofauti kwa uchunguzi wangu, kwani wakati mvua zikinyesha, barabara za mitaani zile za vumbi zimekuwa kero hali inayopelekea watu kuhoji, HAWA NDO WABUNGE TULIOWACHAGUA?

Barabara ya kutoka kona ya BWIRU mpaka Nyasaka, madereva wa daladala wengi wanaikimbia kwa kuwa na mashimo. Magari yanaharibika kwa ubovu wa barabara hiyo. Na road hii ina wapiga kura, na tayari wameanza kulalama.

Barabara ya NUNDU-NYAKATO MECCO, nayo hali kadhalika. Hofu yangu ni kwamba, iwapo suluhisho halitatafutwa, basi wabunge hawa watakuwa wanawapa nafasi CCM kulitwaa tena JIJI la Mwanza.

Kulinusuru ni wao japo kuwa karibu na wananchi, kuwaelimisha kwa nini barabara hazitengenezwi na kama jamii ya eneo husika tufanyeje kuepuka hatari ya kukosa huduma ya usafiri inayotokana na uwepo wa barabara isiyopitika.

Kuendlea kujificha kwa wabunge hawa bila hata kutoa matamko kwa uzembe huu, inaonesha kwamba hawajali kwani kwa habari ya HIGHNESS alishahama na mtaa. Wakati akifanya kampeni alikuwa akilala nyumba moja iliyopo kwa Lema-Munazi, siku hizi hatumuoni pande hizo thus ametutelekeza na barabara yetu inayotutesa.

Watch out kijana, kwa ustawi wa chama.

Kabla hujaandika umejiuliza vizuri kwamba kwa nini barabara hizo ni za vumbi toka tupate Uhuru? Kwa miaka mingapi barabara hizo hazikuangaliwa na haikuwa hoja isipokuwa walipoingia Chadema ndio zinatazamwa na kuwa sababu ya uwakilishi mbaya wa Wabunge hawa?.

Barabara zote hutegenezwa kutokana na mipango ya miji ama toka mfuko wa serikali za mitaa ama serikali kuu hatuna mfumo wa madaraka mikoanikusema kwamba mbunge anawajibika moja kwa moja. Kama barabara hizo zipo chini ya manispaa ya jiji nadhani hoja hii ungeipeleka kwa wahusika yawezekana kuwa uzembe uko huko ama serikali kuu.. Labda ungefuatilia hansard za bunge na kutazama uwakilishi wa wabunge hawa kuhusiana na barabara hizo kama wamewakilisha..
 
Uliyoyasema ni kweli, kwanza barabara zote hizo ulizozitaja ziko chini ya JIji (Sio Serikali kuu).
Mwenye Jukumu la kutengeneza hizo barabara ni Jiji. FYI, Jiji la Mwanza linaongozwa na CDM. Meya
anatoka CDM. Hivyo kushindwa kutengenezwa kwa barabara hizo it is down to CDM. Hili halina
mkono wa magamba.

Kama kweli CDM wanataka waonekane wako tofauti na Magamba na wako tayari kushika dola 2015
haya matatizo yaliyomo ndani ya uwezo wao LAZIMA wayatatue bila visingizio. Kama tatizo ni
MKURUNGEZI basi wamukatae apelekwe sehemu nyingine aletwe mwingine atayekwenda na
kasi ya CDM.

Afterall moja ya maazimio ya Wana-Mwanza ilikuwa kumfukuza Mkurungezo Willison Kabwe
mara CDM watakapotwaa uongozi wa JIji, kwani alionekana dhahiri kumbemba Lau Masha
hata pale ilipoonekana dhahiri ameshindwa uchaguzi.

Swali Je ni kwanini Wenje na Highness wame compromise na Willison Kabwe?! Wametusaliti wana MZA.
Uzuri ni kwamba Wana MZA huwa hatusahau kama hawajui wawaulize marehemu Bomani, Masha, Diallo
the list goes on, Mwanza tunafahamu kutumia kura zetu vizuri.
Huyu si nilisikia alihamishwa toka Mwanza baada ya kushindwa kumrudisha rafiki ya Kikwete kwa nguvu??
 
Kama Meya na Mkurugenzi wa jji wanafanya hujuma mbunge anafanyaje? Hukumbuki mgao wa umeme ulivyokuwa ''special'' kwa Mwanza na Arusha?

Meya wa Mwanza CDM, baraza la madiwani wengi ni CDM. kama Mkurugenzi hatoai ushirikiano kufanya shughuli za watu, wana nguvu ya kumtengenezea zengwe, wakamwondosha
 
Huyu si nilisikia alihamishwa toka Mwanza baada ya kushindwa kumrudisha rafiki ya Kikwete kwa nguvu??
Willison Kabwe bado yupo, na anasumbua kweli, jana tu ameanza kutangaza wajasiria mali wote waondoke kwenye maeneo ambayo hawaruhusiwi. Aliwalenga mafundi seremala, mechanics, wauza matunda na wengine wa aina hiyo. Sasa sijui yeye kalitoa wapi wakati inatakiwa lipitie kwenye baraza la madiwani
 
wewe unajua kazi ya mbunge ni ipi kama hawezi kusimamia mawasiliano jimboni kwake? au un azani ubunge ni uanaharakati? hawa jamaa tunawapenda ila hawajui kwa nini waliomba ubunge.

Kanyasu, rudi kido ufafanue, uweke wazi. sijaua kama ni swali au ni nyongeza kwa yaliyokwisha jadiliwa. Hata hivyo niungane na wewe kwenye bolded. Wana saliti ilani zao za uchaguzi
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom