ntamaholo
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 12,906
- 6,909
- Thread starter
- #61
Ndg. zangu
Hoja hii ni kweli ina mambo fulani ya kinafiki;
Matatizo ya mwanza ni ya kurithiwa kutoka enzi za zamani. Jiji hili liliplaniwa vibaya, halina miundo mbinu ya barabara, waloplan jiji hili hawakutegea kama litakuwa na kasi ya ukuaji namna hii. (Inasemekana ni jiji linalokua kwa kasi ya ajabu Afrika Mashariki). Alofanya survey ya jiji hili la mwanza alipal jiji lijengwe Nyamhongolo - hapa lilipo jiji ilikuwa ni sehemu tu ya Bandari. Kutokana na viongozi wa serikali yetu kutothamini mawazo ya wataalam; wakaruhusu ujenzi holela maeneo ya rufiji, uhuru, mabatini, igogo,, bugando n.k.
Wazo langu! Baadhi ya barabara ulozitaja ni matatizo ya Mkurugenzi wa jiji na watendaji wake. Ikumbukwe kuwa Mkurugenzi wa jiji ni Chaguo la Rais wa Magamba - kwa hali hiyo matatizo yote uloyataja hawezi kuyakwepa ila sisi wana CHADEMA tunajitahidi kumulika mapungufu katika jamii ili pale ambapo wenye nchi watakereka watajua la kufanya. CHADEMA wameshika makali ya jiji lakini mpini umeshikiliwa na MAGAMBA ndo maana tukifurukuta tu wanakimbilia kuwataarifu walala nje (Polisi) wenye siraha za kutisha raia.
TUWAPE MOYO WABUNGE WETU VIJANA WAFANYE KAZI KAMA TUTAKAVYOWASHAURI.
Nakusoma ndugu.
Ndo hapo sasa tunapohitaji wabunge/madiwani waje watueleze kuwa mambo hayafanikiwa kwa kuwa WILISONI KABWE Mkurugenzi wa jiji anakwamisha kila juhudi zetu. Na hapo watatoa suluhisho nini wana mwanza wafanye. Wewe unajua hayo, maorirty hawajui. Jukumu langu,, mie ninaye kipenda chama cha CDM kishike hatamu, ni kuwakumbusha wachaguliwa wetu wasiwatelekeze wapiga kura, kwani hawatakuwa wamejitofautisha na magamba