Wenje na Highness wabunge CHADEMA MWANZA, msiidhalilishe CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wenje na Highness wabunge CHADEMA MWANZA, msiidhalilishe CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ntamaholo, Nov 11, 2011.

 1. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #1
  Nov 11, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,150
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Wana Jamvi habarini.

  Jiji la Mwanza, ni jiji ambalo kwa sasa linaheshimika kwa harakati za kisiasa baada ya wabunge tena waliowahi kuwa mawaziri kubwagwa na vijana wado EZEKIEL WENJE-Nyamagana na HIGHNESS KIWIA-Ilemela. Wabunge hawa vijana, walichaguliwa kwa imani kubwa na Mwanza tuliamini wataonesha usimamizi wa rasilimali za umaa kwa manufaa ya umma.

  Hali imekuwa tofauti kwa uchunguzi wangu, kwani wakati mvua zikinyesha, barabara za mitaani zile za vumbi zimekuwa kero hali inayopelekea watu kuhoji, HAWA NDO WABUNGE TULIOWACHAGUA?

  Barabara ya kutoka kona ya BWIRU mpaka Nyasaka, madereva wa daladala wengi wanaikimbia kwa kuwa na mashimo. Magari yanaharibika kwa ubovu wa barabara hiyo. Na road hii ina wapiga kura, na tayari wameanza kulalama.

  Barabara ya NUNDU-NYAKATO MECCO, nayo hali kadhalika. Hofu yangu ni kwamba, iwapo suluhisho halitatafutwa, basi wabunge hawa watakuwa wanawapa nafasi CCM kulitwaa tena JIJI la Mwanza.

  Kulinusuru ni wao japo kuwa karibu na wananchi, kuwaelimisha kwa nini barabara hazitengenezwi na kama jamii ya eneo husika tufanyeje kuepuka hatari ya kukosa huduma ya usafiri inayotokana na uwepo wa barabara isiyopitika.

  Kuendlea kujificha kwa wabunge hawa bila hata kutoa matamko kwa uzembe huu, inaonesha kwamba hawajali kwani kwa habari ya HIGHNESS alishahama na mtaa. Wakati akifanya kampeni alikuwa akilala nyumba moja iliyopo kwa Lema-Munazi, siku hizi hatumuoni pande hizo thus ametutelekeza na barabara yetu inayotutesa.

  Watch out kijana, kwa ustawi wa chama.

   
 2. tujadili TZ

  tujadili TZ New Member

  #2
  Nov 11, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  serikali imefilicka,haina ela..
   
 3. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #3
  Nov 11, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Jiji la mwanza halinaga mwenyewe!! hata CCM wanajua hilo!!
   
 4. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #4
  Nov 11, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,150
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  kwani mbunge hawezi kumkumbusha meya? Nani afuatilie kwa meya, wananchi au mwakilishi wao!!!! tafakari vizuri, kwani iwapo barabara zinakuwa mbovu halafu mbunge kakool, kinachofuata ni kupoteza Imani naye. Na hapa ni yeye na diwani wake, kulala kwao kutatukost wapenda maendeleoa
   
 5. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #5
  Nov 11, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,150
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  kwa hiyo unaridhia 2015 lirudi CCM?
   
 6. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #6
  Nov 11, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,150
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  ni wangapi wanaojua hilo? Siyo lazima ajenge, lakini kuonesha kuwa anakerwa na hali ya barabara hiyo, atakubalika kuwa anajli. Yeye kaamua kuhama mtaa kabisa, kwa gari lake lingeharibika. Wakazi wa eneo hilo ndio tunaoumia yeye kahamia kwenye lami pasiansi
   
 7. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #7
  Nov 11, 2011
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Ulikwishawahi kuhudhuria vikao vya halmashauri na hukuona wabunge hawa wakikemea?Au unadhani ni mpakawaende kwenye vyombo vya habari au bungeni!Fanya utafiti kwanza ndipo uje na kauli kama hizo,pia suala la mtu kuhama ni la mtu binafsi ili mradi anaishi jimboni kwake,au ulitaka akae unapopataka wewe?
   
 8. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #8
  Nov 11, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,150
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Nijuavyo mimi kazi ya Mbunge ni kuwasimamia watumishi wa umma. Ndiye mwakilishi wa wananchi wenye nguvu anayeweza kuongea na mtumishi wa uma kama Mkurugenzi wa jiji ambaye ndiye anayepokea pesa toka serikali kuu.

  Sasa Mbunge anapokuwa zuzu, mwisho wa siku hata pesa zenyewe zinarudishwa serikalini eti kazi iliyokusudiwa haijafanyika. Kwa wabunge waliolala usingizi mzito kama Highness, tutarajie pesa kurudishwa kwa GVT kwa visingizio mbalimbali ikiwemo na madai ya kuchelewesha pesa.

  Mbunge makini lazima awaeleweshe wananchi wake kinachoendelea.
   
 9. Gwallo

  Gwallo JF-Expert Member

  #9
  Nov 11, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 2,322
  Likes Received: 844
  Trophy Points: 280
  Mkwara wote wa nini toa maelekezo nini Mbuge akifuatilie wala siyo matisho. Nawasiwasi na umwanza wako huenda mpitaji tu wewe, tena inaonyesha unazungumzia uharibifu wa magari kuonyehsa uko matawi ya juu, mweleze Mbunge wako afuatilie kuhusu upatikanaji wa elimu bora, dispensary za kutosha na zenye dawa na hiyo barabara unayozungumzia inayotishia ubunge wa Wenje na Highness?

  Toa ushauri kwa Mbunge wako usilalamike!!!!!!
   
 10. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #10
  Nov 11, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,150
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  siyo rahisi kwa kila mwananchi kwenda council kusikiliza vikao vya madiwani, lakini ni wajibu wa mbunge kurudi kwa wananchi na kutoa ufafanuzi wa masuala yaliyozungumziwa council. Barabara ni mbovu, yeye katulia, si wananchi watajitafutia majibu?

  Juzi maeneo ya Kiloreli kwa msuka, wananchi walikerwa na hali ya barabara, waendesha pikipiki wakaamua kuziba eneo lililokuwa korofi, walipofanikiwa, wakataka kila gari linalopita pale wachangie japo 500/=. Watu waovu wakapiga simu polisi-Ilemela, Polisi walikuja na kuwatimua wale wananzengo.

  Mbunge yeye katulia tu. Ataikost CDM huyu, nasema haya kwa uchungu na kwa kuwa sina njia nyingine ya kumfikia
   
 11. M-pesa

  M-pesa JF-Expert Member

  #11
  Nov 11, 2011
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 605
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hapa umesema ukweli, achana na wanaokubeza. Communication ndio uhai na ku survive kwa mwanasiasa.
   
 12. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #12
  Nov 11, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,150
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  siyo kihivyo mkuu, mie kila siku napanda daladala kwetu tuanita express. Ninachokishuhudia ni baadhi ya madereva kuamua kuhama ruti na kutafuta ruti ya buhongwa kwani mwanzo mwisho ni lami. Watumiaji wa barabara hiyo ninayoizungumzia, watapanda gari labda kama mvua inanyesha, lakini kama pako shwari, mwendo wa gari na mwenda kwa miguu, havitofautiani hata kidogo. gari linaeenda kwa speed labda speed 2, hata tano hawafiki. Hivyo kwa mtu anaeishia kwa msuka, bigbite na contena, anaona bora kutembea kuliko kukaa kwenye gari linalotembea kwa speed ya mwenda kwa miguuu
   
 13. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #13
  Nov 11, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,150
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Ushauri ndo kama huu ninaoutoa, madiwani wake na katibu wasilale, wanaweza kuitisha mkutano wa hadhara na kuzungumza kwa niaba ya mbunge, siyo kuaaa kimywa as if KILAMHEWA hawajachagua wawakilshi
   
 14. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #14
  Nov 11, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,959
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  Ujumbe umefika. Ngoja nimpigie simu, ila shida ya barabara ya Kilimahewa ni kwamba 1. Nyembamba sana 2. Huwezi kubomoa nyumba za watu.
   
 15. e

  evoddy JF-Expert Member

  #15
  Nov 11, 2011
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 302
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Wanaharakati kwanza tungemshukuru mtoa taarifa kwa kuwakumbusha wabunge hawa maana hivi ni vitu ambavyo walituhaidi wakati wa kampeni kutatua kero zetu.

  Pili huyu ni mtu ambaye anaipenda sana CHADEMA hivyo kama ilvyokwenye katiba ya chama kila mwanachama anatakiwa kuwa mtetezi ilani na mwangozo wa shughuli za kitaifa

  Tatu unapoona mwananchi anamlalamikia mbunge ujue katika yale maeneo hajafika kuendesha mikutano na wananchi wa maeneo husika.

  Nne tusiwakatishe tamaa wapenda maendeleo ukizingatia eneo la jiji la Mwanza linafikika kwa urahisi zaidi.hivyo wabunge wafahamu tunawapenda sana
   
 16. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #16
  Nov 11, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Uliyoyasema ni kweli, kwanza barabara zote hizo ulizozitaja ziko chini ya JIji (Sio Serikali kuu).
  Mwenye Jukumu la kutengeneza hizo barabara ni Jiji. FYI, Jiji la Mwanza linaongozwa na CDM. Meya
  anatoka CDM. Hivyo kushindwa kutengenezwa kwa barabara hizo it is down to CDM. Hili halina
  mkono wa magamba.

  Kama kweli CDM wanataka waonekane wako tofauti na Magamba na wako tayari kushika dola 2015
  haya matatizo yaliyomo ndani ya uwezo wao LAZIMA wayatatue bila visingizio. Kama tatizo ni
  MKURUNGEZI basi wamukatae apelekwe sehemu nyingine aletwe mwingine atayekwenda na
  kasi ya CDM.

  Afterall moja ya maazimio ya Wana-Mwanza ilikuwa kumfukuza Mkurungezo Willison Kabwe
  mara CDM watakapotwaa uongozi wa JIji, kwani alionekana dhahiri kumbemba Lau Masha
  hata pale ilipoonekana dhahiri ameshindwa uchaguzi.

  Swali Je ni kwanini Wenje na Highness wame compromise na Willison Kabwe?! Wametusaliti wana MZA.
  Uzuri ni kwamba Wana MZA huwa hatusahau kama hawajui wawaulize marehemu Bomani, Masha, Diallo
  the list goes on, Mwanza tunafahamu kutumia kura zetu vizuri.
   
 17. K

  Kifimbocheza JF-Expert Member

  #17
  Nov 11, 2011
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 496
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Serikali yako ya CCM Haina Hela unategemea nn?

  Soma Mgazeti na sikilia Redio na TV Serikali haina hela na haijawalipa Makadarasi toka 2006

  Sasa unataka WENJE afanyaje Atoe Fedha zake Mfukoni

  Tumia Akili Kidogo ww Ulyeleta Mada acha kutumia Masaburi kufikiri

  Si ulichagua CCM ww na Bado
   
 18. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #18
  Nov 11, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,150
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  nakushukuru kwa kuliona hilo, lakini naamin techonolojia haishindwai
   
 19. Mwanagandila

  Mwanagandila Senior Member

  #19
  Nov 11, 2011
  Joined: Oct 9, 2011
  Messages: 182
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  siyo kihivyo mkuu, mie kila siku napanda daladala kwetu tuanita express. Ninachokishuhudia ni baadhi ya madereva kuamua kuhama ruti na kutafuta ruti ya buhongwa kwani mwanzo mwisho ni lami. Watumiaji wa barabara hiyo ninayoizungumzia, watapanda gari labda kama mvua inanyesha, lakini kama pako shwari, mwendo wa gari na mwenda kwa miguu, havitofautiani hata kidogo. gari linaeenda kwa speed labda speed 2, hata tano hawafiki. Hivyo kwa mtu anaeishia kwa msuka, bigbite na contena, anaona bora kutembea kuliko kukaa kwenye gari linalotembea kwa speed ya mwenda kwa miguuu

  hapo kwenye kijani sijui wamaanisha nini?
  ww utakuwa umetumwa na wana CCM huna lolote,la sivyo ww mgeni na jiji la mwanza, unasema barabara ya kiloleli fupi tu ambayo haina ht km 3 toka kona ya bwiru, wasemeje raia wanaoishi kiseke ppf, km 5 toka njia panda pale 7 7, barabara mbovu haipitiki mvua ikinyesha ndio balaa, tunashuka na kwenda home kwa miguu..
  kifupi ni kwamba viongozi wa jiji wanambinu ya kuidhoofisha chadema na wabunge wake katika kutekeleza malengo yao, madiwani ndio wanaokaa na kupitisha maadhimio ya bajeti ya jiji mmbunge yy anashiriki tu bt wenye maamuzi ya mwisho ni madiwani,
  pia daladala kuhama route sio coz barabara mbovu, mbona kwenda furahisha, kirumba mpk bwiru ni lami mwanzo mwisho lakini gari zinazoenda huko hazifai, mbovu kupitliza??
  kiseke road mbovu ila mbona daladala zinafika, kikubwa ni abiria ndio wanachokiangalia

   
 20. e

  evoddy JF-Expert Member

  #20
  Nov 11, 2011
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 302
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Niwajibu wa mbunge kufanya mikutano na kutoa taarifa kuhusu mambo mbalimbali yanayotakiwa kufanyika katika maeneo husika kama hawaitishi mikutana basi ni lazima walaumiwe.

  Sisi kama wanamwanza lazima tutoe malalamiko ili waamke maana ni wajibu wetu kufanya hivyo.Kama kunatatizo la kisera basi hawa wabunge wetu watueleze tunahitaji kwenda na kasi kubwa kuliko iliyokuwapo hapo nyuma
  Hihi ndiyo kazi ya NGUVU YA UMMA(PEOPLES POWER)
   
Loading...