Elections 2010 Wenje ashawishiwa ajitoe, shinyanga yadaiwa kuibiwa kura

harrysonful

Member
Oct 27, 2010
34
0
kwa taarifa zinazoendelea kusambaa shinyanga,, mgombea wa chadema bwana shelembi ameibiwa ushindi wake na kusababisha hali ya mchafuko kutokea sasa huko shinyanga..

Pia kwa habari zisizo rasmi mkapa na jk wako mwanza wakimshawishi bwana wenje akubali kushindwa au kujitoa ktk mchakato.. Binafsi naumia sana,, any way nawaachia watanzania.piga simu mwanza na shinyanga wawape habari huko
 
Kwanini ajitoe kwani kuna ulazima gani huyo Masha kushinda hapo hawa CCM wakoje jamani??aagggrrrrrrr.....
 
Atajitoaje na uchaguzi umeshafanyika, is it possible or just a guess work
 
Sasa huko tunakoelekea siko...
Ni kwanini ccm wanang'ang'ania madaraka kiasi hiki? nini siri iliyojificha mpaka waogope kushindwa kiasi hiki..?
Naamini kuna mambo magumu tusiyoyajua yanafichwa na hawa wanaojifanya kondoo kumbe ma-chui..
 
kwa taarifa zinazoendelea kusambaa shinyanga,, mgombea wa chadema bwana shelembi ameibiwa ushindi wake na kusababisha hali ya mchafuko kutokea sasa huko shinyanga..

Pia kwa habari zisizo rasmi mkapa na jk wako mwanza wakimshawishi bwana wenje akubali kushindwa au kujitoa ktk mchakato.. Binafsi naumia sana,, any way nawaachia watanzania.piga simu mwanza na shinyanga wawape habari huko
Kuna haja ya kuwa serious sasa na kuacha majungu.
 
Hakuna kujitoa kwanini ajitoe kwani kuna ulazima wa kujitoa kwani wanang'ang'ania hapo Nyamagana CCM wana nini yaani hapo mpaka kieleweke yaani hadi mzee wa kokoto naye ameenda huko pole sana mtahangahika sana kama vile kuku anataka kutaga mayai lakini ukweli unajulikana
 
unasikia toka shinyanga na mwanza au UNAUHAKIKA NA UNACHOTAMKA NA KUTUANDIKIA?....am sorry to say so
 
Kama hauamini piga simu sasa shinyanga na watakwambia kinachotokea hautaamini.. Chukua simu yako na pata ukweli kwa unaemwamini.
 
Kwanini hawa CCM wanang'ang'ania jimbo la Nyamagana? Waache wananchi waamue wenyewe
 
Ndugu zangu wana jf, hali ya mwanza siyo shwari hata kidogo, ccm wanataka kulazimisha ushindi, ni kweli kikwete yupo mwanza na nia na madhuni ya kwenda ni kulazimisha masha atangazwe mshindi wakati ni kuwa ameshindwa vibaya sana, hivi sasa wananchi wapo tayari kwa lolote kwani hawataki kudhulumiwa haki yao.

Police wameambiwa wawachape na mabomu na virugu lakini wamekataa kuwapiga watu wanaodaia haki yao, piga simu kwa ndugu jamaa na rafiki yako yeyote aliyepo mwanza atakueleza haya, kwanini ccm na kikwete wake wanataka kufanya hilo, kwanini wanalazimisha matokeo, hapo ni ubunge tu, je kwenye urais haki nako imetendeka kweli.

Ccm inabidi wajue kuwa wao ndiyo walikuwa wanapreach about amani, wakati kumbe hawataki hiyo amani, kwa kweli inabidi tuingie sote barabarani kupambana na kitu hiki. Ni sababu zipi zinawafanya wasitangaze kuwa wameshindwa na kuachia jimbo kwa amani.
 
No data no right to speak... tusichanganyane jamani

Ni kweli siyo vizuri kurushana mimi ninachojua ni kuwa Dialo ndiye alimuomba msimamizi wa Uchaguzi bwana Kabwe asitangaze matokeo kwanza ili zungumze na Highess Samson mbunge mpya wa Ilemela akubali kujitoa kwa ujira wa milioni 300 akagoma. Na baada ya hapo Diallo amekubali kusaini na amekamilisha sasa zinahesabiwa kura za Nyamagana wakimaliza watasaini.
 
Wana-Mwanza tunawasihi mkae hapo kwa amani wakla hamna haja ya kufanya fujo.Ila msiondoke hadi kieleweke kama ni kukesha mkeshe peaneni zamu, ila msifanye fujo sisi tulio mbali tunaendeleza maombi tumefunga kwa ajili yenu.Majina yenu yatakumbukwa na watanzania kuwa mlipigania hadi haki ikapatikana.Naamini mungu atawasimamia na pia mkumbuke Rais mtarajiwa yupo nyuma yake anaendelea kusoma matukio muda muafaka ukiwadia tutamsikia, na yeye tunamwanimini ni mamlaka kamili.peopleeeeeeees
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom