Elections 2010 Wenje amemaliza kazi Nyamagana

Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
261
Nimetazama vimbwenga vya wenje kupitia TBC1. Umati unatisha! Hakuwa anaomba kura kwa sababu ni wazi kashapata. Alikuwa anahamasisha ulinzi wa kura.

Hivi hadi sasa tuna uhakika wa majimbo mangapi?
 
Kwa habari za nadani ya chama kuna uhakika wa Majimbo 30,kati ya majimbo hayo yapo majimbo ya Arusha mjini,Maswa mashariki,Moshi Mjini,Singida Mashariki,Tarime,Ubungo,Sumbawanga Mjini,Bukoba mjini,Busanda,Bukombe,Nyamagana,Iringa mjini,Hai,Njombe Kaskazini,Kigoma kaskazini,Busega,Mbeya Vijijini,Mbulu na Kawe.
 
kumekucha!mtashangazwa na matokeo ya moshi vijijini, Anton komu wa chadema amemkalia kooni dr cyril chami wa ccm
 
hayo 30 ni according to Mwawado. Ila kwa taarifa nilizozipata ni zaidi ya majimbo 80 kama mambo yatakuwa kama ilivyopangwa na hila hazitafanyika.
 
nilisema tagu kurejeshwa kwa Wenje, pale Nyamagana, kua tutafanya kazi ya kusisimua, hatuta waangusha waTz, Masha anaujua Ukweli, anaandaa Polisi kuiba kura, wananchi wameapa kuzilinda.
 
Kwa habari za nadani ya chama kuna uhakika wa Majimbo 30,kati ya majimbo hayo yapo majimbo ya Arusha mjini,Maswa mashariki,Moshi Mjini,Singida Mashariki,Tarime,Ubungo,Sumbawanga Mjini,Bukoba mjini,Busanda,Bukombe,Nyamagana,Iringa mjini,Hai,Njombe Kaskazini,Kigoma kaskazini,Busega,Mbeya Vijijini,Mbulu na Kawe.

Ongeza:
Biharamulo, Ngorongoro, Kiteto, Muhambwe, Geita, Mwibara, Musoma mjini, Iringa Vijijini etc

Njombe magharibi kwa mhe. nyimbo msisahau. chichiem inahenywesha kisawasawa.

Pipooooooooooooooooooooooooooooooooooooz ......................
 
Nimetazama vimbwenga vya wenje kupitia TBC1. Umati unatisha! Hakuwa anaomba kura kwa sababu ni wazi kashapata. Alikuwa anahamasisha ulinzi wa kura.

Hivi hadi sasa tuna uhakika wa majimbo mangapi?

Wakibaatika majimbo matano wana bahati.

Kwani kuwa na umati mkubwa kwenye kampeni si kura zile. Mjue wapiga kura ni wachache sana. na mlivyo banwa kura hazipigwi kanisani. Poleni chadema, Pole Slaa
 
CCM inakiri kuna utata kwenye majimbo 74 (soma gazeti la Uhuru la leo Uk 9), tafsiri yangu ni kuwa upinzani una nafasi ya kushinda katika majimbo hayo kama wananchi watapiga na kulinda kura !!!
 
Jamani ngoja niwape!! Kigoma--majimbo 4,
Mbeya--majimbo 3,
Kagera --- majimbo 3,
Mwanza ---majimbo 3,
shinyanga ---4,
Mara ---majimbo 4,
Arusha ----3,
Moshi ----3,
Morogoro ---2,
Dodoma ---1,
Singida --2,
Iringa ----4,
sumbawanga ---3,
Tabora --2,
Dar es salaam ---3
Pwani ---1
Tanga ----2
sehemu nyingine sijapata kwa undani.
 
Kwa habari za nadani ya chama kuna uhakika wa Majimbo 30,kati ya majimbo hayo yapo majimbo ya Arusha mjini,Maswa mashariki,Moshi Mjini,Singida Mashariki,Tarime,Ubungo,Sumbawanga Mjini,Bukoba mjini,Busanda,Bukombe,Nyamagana,Iringa mjini,Hai,Njombe Kaskazini,Kigoma kaskazini,Busega,Mbeya Vijijini,Mbulu na Kawe.
P/se !!!!!!!!!!!!!!Karatu since 1995

Wakibaatika majimbo matano wana bahati.

Kwani kuwa na umati mkubwa kwenye kampeni si kura zile. Mjue wapiga kura ni wachache sana. na mlivyo banwa kura hazipigwi kanisani. Poleni chadema, Pole Slaa

Udini..... udini.... udini hatutaki udini hapa, lete hoja tutakusikiliza sio mpaka uguse imani za watu. Kwa mtazamo wako mwepesi unadhani neno kanisani umelitumia dhidi ya chadema tu kumbe umewagusa na wale unaowasiliana nao hapa JF. Tumesema mambo ya msikiti/ kanisa au uislamu na ukrisito usitumike katika jukwaa hili. Tunahitaji umoja wa kitaifa kuliko jambo lolote.

hata kama hamjanichagua nitajivika uongozi wa kukemea udini hadi mwisho wa jasho langu. Nitatumia nendo yangu kuwaasa wote wanafikiri udini ni jambo jema kwa taifa letu.

Bila ubaguzi nitaendelea kuwalinda wote Waislamu na wakristo sitakubari mtu kutuharibia undugu wetu.
 
Wakibaatika majimbo matano wana bahati.

Kwani kuwa na umati mkubwa kwenye kampeni si kura zile. Mjue wapiga kura ni wachache sana. na mlivyo banwa kura hazipigwi kanisani. Poleni chadema, Pole Slaa

Moja ya kazi zangu kubwa nitakazozifanya hapa JF ni kuwasaka wapenda udini na kuwakaripia kwa nguvu zangu zote. Ni makosa kudhani kwamba weredi unapimwa kwa kigezo cha udini. Hata usiposhambulia dini ya mtu, tutakuelewa tu usihofu hapa JF kuna vichwa.
 
sijaona mikakati ya kutumia media kurusha hotuba za Slaa ili ziwafikie wananchi katika maeneo ambayo hakubahatika kufika. Hii itawapa support sana wagombea wa chadema maeneo husika. lazima hotuba hizo zitawabadilisha wapiga kura wachache mawazo na kupigia chadema.
 
Wakibaatika majimbo matano wana bahati.

Kwani kuwa na umati mkubwa kwenye kampeni si kura zile. Mjue wapiga kura ni wachache sana. na mlivyo banwa kura hazipigwi kanisani. Poleni chadema, Pole Slaa
.

Watu wengine ni wa ajabu sana, neno kanisani umelitumia mahala si pake. Udini ni jambo baya na linapunguza uwezo wa mtu kufikiri kwa sababu linakwenda kubomoa upendo kati ya dini na dini. kwa kuwa umelewa udini umeshindwa kutambua kuwa unalitukana kanisa hapo juu lakini wagombea wa ubunge katika jimbo la nyamagana (Lawrence Masha wa CCM na Wenje wa chadema) ni wakristo.

Usipende kuchanganya dini na siasa kwa wakati mmoja. kila sekta ipe nafasi yake,kwa wakati wake na mahala pake. hapo ulipotumia neno kanisa sio pake.
 
Back
Top Bottom