Wengine wanasema miradi ya gesi na mafuta inachelewa sana kwasababu hatuna wataalamu wa kutosha wa kujadili mikataba ya gesi na mafuta

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,317
8,228
Moja ya tatizo linalokumba taifa letu ni kuchelewa kwa miradi ya gesi na mafuta. Majadiliano yamekua yakichukua muda mrefu sana.

Labda pengine changamoto imekua kwenye kuelewana na kuridhiana vile vifungu vilivyowekwa kwenye mikataba hiyo.

Watu wengi wameweza kusema kuchelewa kwa miradi ya gesi na mafuta kunasababishwa sana sana na upungufu wa wataalamu wa mafuta na gesi nchini.

Wanasema taifa lina upungufu wa wataalamu wa kujadiliana kwenye mikataba ya mafuta na gesi. Pia wanasema eneo la uhandisi na sayansi ya mafuta na gesi lina upungufu wa wawataalamu. Yaani wataalamu waliopo hawana ujuzi na ubobezi wa kutosha kwenye mambo waliyosomea ya mafuta na gesi. Taifa linahitaji wataalamu wenye ujuzi wa kutosha na ubobezi katika fani za sayansi na uhandisi wa mafuta na gesi pamoja na fani za mazingira, sheria na uhasibu zilizojikita upande wa mafuta na gesi.

Kwenye kujadiliana mikataba ya mafuta na gesi tunahitaji wataalamu wa sheria ya mafuta na gesi, wahasibu wa mafuta na gesi, wataalamu wa sayansi na uhandisi wa mafuta na gesi (wahandisi wa petroli au mafuta na gesi, wakemia wa petroli au mafuta na gesi, na wajiorojia wa petroli au mafuta na gesi, wataalamu wa mazingira lakini katika fani ya mafuta na gesi na wengineo.

Nini kifanyike ili kupata wataalamu wa mafuta na gesi wabobezi au wenye ujuzi katika mambo waliyosomea?

A. Je serikali iendelee kusomesha wataalamu zaidi kwenye vyuo vya ndani?

B. Je serikali iendelee kuwatafutia scholarship za kusomea fani za mafuta na gesi nje ya nchi?

C. Je serikali itengeneze utaratibu wa interniship ya lazima ya mwaka mmoja kwa wahitimu wote wa fani za mafuta na gesi? Je mfumo huo wa internship uratibiwe na wizara ya nishati yenyewe kama wanavyofanya wizara ya afya?

D. Je vyuo vitengeneze utaratibu wa interniship ya lazima ya mwaka mmoja kwa wahitimu wote wa fani za mafuta na gesi?

E. Je serikali kupitia wizara ya nishati iandae scholarship ya internship kwenye makampuni ya kimataifa ya mafuta na gesi kwa wahitimu wa fani za mafuta na gesi ili wakapate kujifunza teknolijia nchi za nje. Ili wakirudi warudi na ujuzi wakusaidia taifa letu na sio maarifa ya darasani?

Karibuni kwa majibu yenu na michango.
 
Wasomi wetu ndo hawa wakina Prof.Kabudi,Osoro na mruna pamoja na PhD Kama ya Ya ya ya ya×17 Kama taifa tuna safari ndefu Sana

Tumbocracy
 
Kwa ulichoandika ina maana hata uko vyuoo kuna uhaba wa wahadhiri wabobezi wa hayo masuala

Huu ni mjadala unaotakiwa kajadiliwa kwa upana sana kwenye vyombo vya habari na hata kuwa na midahalo kipi kifanyike waziri na makatibu wakuu wa elimu, na nishati wanajukumu kushiriki hii mijadara na kuja na majibu sahihi wakowa kama watalamu makatibu wakuu wanamsaidiaje mama kuvuka hapa
 
A. Je serikali iendelee kusomesha wataalamu zaidi kwenye vyuo vya ndani?
Hapana, inabidi vyuo vya nje zaidi na wahudumu kwenye makampuni ya nje kwanza kwa miaka isiyo pungua kumi mfano nchi kama U.S.A , China, Russia, Qatar, Saudia Arabia n.k
B. Je serikali iendelee kuwatafutia scholarship za kusomea fani za mafuta na gesi nje ya nchi?
Ndio tena waongeze kiwango cha wasomi kwenda kusoma nje.
C. Je serikali itengeneze utaratibu wa interniship ya lazima ya mwaka mmoja kwa wahitimu wote wa fani za mafuta na gesi? Je mfumo huo wa internship uratibiwe na wizara ya nishati yenyewe kama wanavyofanya wizara ya afya?
Ndio, tena ikiwezekana internship iwe kuanzia mwaka mmoja mpaka miwili. Ndio huo mfumo uratibiwe na wizara ya nishati pamoja na wataalamu kutoka makampuni makubwa ya gas na mafuta kutoka nje yanayo tambulika duniani.
D. Je vyuo vitengeneze utaratibu wa interniship ya lazima ya mwaka mmoja kwa wahitimu wote wa fani za mafuta na gesi?
Ndio hakuna ukakasi juu ya hilo.
E. Je serikali kupitia wizara ya nishati iandae scholarship ya internship kwenye makampuni ya kimataifa ya mafuta na gesi kwa wahitimu wa fani za mafuta na gesi ili wakapate kujifunza teknolijia nchi za nje. Ili wakirudi warudi na ujuzi wakusaidia taifa letu na sio maarifa ya darasani?
Ndio, serikali inapaswa kufanya hivyo.
 
Hapana, inabidi vyuo vya nje zaidi na wahudumu kwenye makampuni ya nje kwanza kwa miaka isiyo pungua kumi mfano nchi kama U.S.A , China, Russia, Qatar, Saudia Arabia n.k

Ndio tena waongeze kiwango cha wasomi kwenda kusoma nje.

Ndio, tena ikiwezekana internship iwe kuanzia mwaka mmoja mpaka miwili. Ndio huo mfumo uratibiwe na wizara ya nishati pamoja na wataalamu kutoka makampuni makubwa ya gas na mafuta kutoka nje yanayo tambulika duniani.

Ndio hakuna ukakasi juu ya hilo.

Ndio, serikali inapaswa kufanya hivyo.
Ahsante sana kwa mchango wako mtaalamu.
 
Back
Top Bottom