Wengine wananunua laptop, sisi hatujaweza kutosheleza vitabu


W

Wa Busiya

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Messages
326
Likes
0
Points
0
W

Wa Busiya

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2012
326 0 0
Mambo mengine yakitokea huibua hisia za kusononesha miongoni mwa jamii badala ya kufurahisha kutokana na taathira yake kwa jamii. Hivi wenzetu wanaposema wananunua laptop 1,300,000 kwa mwaka huu wa fedha mtanzania anayejua kushabikia vyama tu anajisikiaje! Tanzania bado tunazo shule ambazo wanafunzi wanakalia mawe na bado walimu hawatoshi. Uko wapi ulinganifu wa elimu tunapoelekea shirikisho la Afrika Mashariki! Mungu wangu! Hivi ni kweli hatuwezi kuweka mikakati inayoonekana kama walivyofanya wenzetu wa Kenya? Mbona kagame anasomesha wanafunzi wengi katika vyuo vyetu na duniani kote bure hasa masomo ya sayansi? Sisi wadangayika tunafanya nini? Je, Vision 2025 inatekelezeka? Mkukuta je? Maisha bora ule wimbo wa kuombea kura uko wapi? Amani na utulivu uko wapi? Muungano uko wapi?
Wa kulaumiwa si serikali hata kidogo, Maana tumeridhika nayo! Raia ndio mabosi wa serikali iliyoko madarakani wenye uwezo wa kuitoa (kwa njia ya kura) au kibakiza. Sasa kama tumeridhika acha nauli ipande, bidhaa kama nafaka zipande, umeme, nyumba za kuanga, elimu vipande maana ndio mkakati wetu.
 

Forum statistics

Threads 1,273,433
Members 490,382
Posts 30,481,458