Elections 2010 Wengine waliopewa mgao wa mlungula wa rada ni akina nani?

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
0

Haya madudu ya sasa hivi ya CCM – yaani kujichanganya na kwa Mkuu wa kaya kuonekana kukaa kimya bila ya kauli yanaonyesha kwamba kuna vigogo wengine, mbali na Chenge na Dr Rashid waliopata mgao wa zile Dola mil 12 za hongo alizopewa Vithlani na BAE.

Likinukuu ripoti mbali mbali za kuhusu sakata la rada, gazeti la Raia Mwema la jana, ukurasa wa 3 chini ya stori "Ubalozi wa Uingereza wabanwa kuhusu rada" (gazeti lilitoka kabla ya taarifa ya jana ya Ubalozi huo kumkana Hosea) kuna ibara moja inasema:

"Vithlani inadaiwa alipewa dola za Kimarekani milioni 12 (zaidi ya Sh bilioni 12) kama kamisheni ya kufanikisha biashara hiyo na kwamba aligawana kitita hicho cha fedha na maofisa saba wa ngazi za juu katika serikali ya Tanzania."

Sasa tutafakari hao maofisa wengine ni watu gani, maana SFO ilitoa majina ya Chenge na Dr Rashid tu, wengine watano ilimezea, bila shaka ni majina mazito mno yasingeweza kutajwa hadharani.

Na jibu la akina nani wao wengine watano litatoa mwanya kwa nini serikali ya CCM inanikanyaga sana na kutia aibu katika suala zima la kuwafikisha wahusika mahakamani. Hali kadhalika kashfa hii ya sasa hivi ya Hosea kumsafisha Chenge na kwa Ubalozi wa uingereza kukana kumeitia aibu Tanzania mbele ya uso wa ulimwengu – iwapo JK anaelewa ‘aibu' ni nini.

Orodha yangu ya watano hao (mbali na Chenge na Dr Rashid) ina upungufu wa majina mawili:

1.Benjamin Mkapa (kama rais wakati ule)
2.Jakaya Kikwete (akiwa Waziri wa Nje wakati ule).
3.Governor Daudi Balali
4.…………………………..
5.…………………………..

Jee, mwenye kuweza kukamilisha orodha hiyo? (bado wawili).
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom