Wengi watarajiwa kumuaga Dk Remmy leo


kilimasera

kilimasera

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Messages
3,073
Likes
23
Points
135
Age
42
kilimasera

kilimasera

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2009
3,073 23 135
WASANII mbalimbali wa kitaifa na kimataifa, viongozi wa serikali leo watauaga rasmi mwili wa mwanamuziki Ramadhan Mtoro Ongala, maarufu Dk Remmy Ongala.

Shughuli hiyo inatarajiwa kufanyika kwenye viwanja vya Biafra, Kinondoni jijini Dar es Salaam kuanzia saa 4.00 asubuhi.

Akizungumza na Mwananchi jana, msemaji wa familia hiyo, Kitenzugo Makassy alisema Dk Remmy anatarajiwa kuagwa pia na wasanii wa muziki wa Injili, fani ambayo alikuwa amegeukia siku za mwisho za maisha yake.

“Mwili wa marehemu utaagwa kesho katika viwanja vya Biafra na viongozi wa serikali pamoja na waimbaji wa kimataifa na wale wa nyimbo za Injili,” alisema Makassy.

Makassy ambaye ni mkongwe wa muziki alisema wameamua kufanya hivyo kutokana na Dk Remmy kuwa alikuwa msanii wa kimataifa aliyeitambulisha Tanzania nje ya mipaka yake.
 

Forum statistics

Threads 1,235,745
Members 474,742
Posts 29,233,599