Wengi wasiojua au wachache wenye hoja:Nyerere | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wengi wasiojua au wachache wenye hoja:Nyerere

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by fige, Jan 22, 2011.

 1. fige

  fige JF-Expert Member

  #1
  Jan 22, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 376
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  katika uongozi sifa mojawapo kuu ya kiongozi ni kuamua. Maamuzi ya kiongozi yanaweza tokana na namna kadhaa ,mojawapo ya hizo ni kutokana na ushauri,kura, au visheni binafsi ya kiongozi.

  Katika mfumo wa kidemokrasia watu tulio wengi tunaamini zaidi uwingi katika kufikia maamuzi.Mfumo huu hutumia zaidi mtindo wa kura kupata maamuzi hata kuchagua nani au nini kinafaa.

  Mtindo huu umejijenga zaidi katika nguvu ya ushawishi ,mtindo huu ni hatari sana hasa pale ambapo wengi si waelewa wazuri wa mambo.

  Mara nyingi mtindo huu kwa watu wasioelewa au wavivu wa kufikiri huangalia nani aliyetoa hoja ,anatoka wapi,ana sura gani na pengine anaamini nini.


  Kukubali kwa mfumo wa vyama vingi TZ ni mfano wa mambo magumu ambayo mwal. NYERERE aliyowahi amua bila kujali wingi wa kura.
  Binafsi nilijiuliza sana kwa nini hoja ya wachache ipewe kipaumbele tena kwa kura chache ?

  Leo hii nimepata jibu kwamba katika maamuzi afadhali uwe na wanaojua ishirini wanaosema ndio kuliko themanini wasiojua wanaosema hapana.Na hapo ndipo nionapo upotofu wa kura.

  Maana ya kusema hayo ni juu ya mambo yanayo endelea TZ hivi sasa kuhusu mjadala wa katiba mpya.


  Je umuhimu wa katiba utegemee watu wengi wasioijua au wachache wanaoielewa ?

  Naomba kuwasilisha wakuu.
   
Loading...