Wengi wanamkubali Bob Marley ila Mfalme wa Reggae duniani ni Lucky Dube

Zack Snyder

Member
Apr 13, 2020
83
296
Dunia yote inamtukuza na kumuhusudu Bob Marley (Culture?) kama mfalme wa muziki rege, sijui wanatumia vigezo gani hasa. Wanamshusha na kumchukulia poa Lucky Dube sijui kwakua Bob aliuawa ndio wanakua na sympathy naye.

Kwa upande wangu japo Dube alimuheshimu Bob ila kwangu dube ndio mfalme wa muziki wa rege duniani. Nyimbo safi zenye ujumbe mwanana, beats zilizoenda shule performance za hadhi ya nyota 15 alizofanya! Nina uhakika Bob angekuwepo wakati Dube Anatoa Album zake 3 za mwanazo (hasa Slave) angempigia magoti Dube na kumsujudu kwa nyimbo bora alizotoa.

Huyu jamaa anajua hasa sikiliza nyimbo zake zote 80% lazima uzipende tu, ukutaka ujue ukali wa huyu mtu angalia Live performance zake utadata.

Najua mtanipinga humu na kunipopoa ila kwangu huyu ndio nishampitisha kua Mfalme wa Rege Duniani, hakuna mwingine.

Ninauhakika huko alipo kapumzika kwa amani maana katimiza kile kilichomleta duniani (Kuhamasisha watu waamke) japo alikua na mapungufu yake kama mtu yoyote yule ila naamini huyu mtu mbingu ni yake na tunaweza mwita mtakatifu kwa kazi yake nzuri.

Sikiliza hizi


 
Bob Marley One Love ilikuwa nyimbo Bora ya millenium

Sent using Jamii Forums mobile app
1. Paragraph ya kwanza tu unaonekana hujui mambo ya kidunia. Aliyeuwawa ni Lucky Dube (kwa risasi) Bob alikufa tu kawaida kwa kansa iliyoanzia kwenye kidole chake cha mguu.
2. Huwezi mlinganisha Lucky Dube na mkongwe Bob. Lucky anaimba na vinanda sana (huwa tunasema nyimbo zake ni kama kwaya) Bob anaimba ile "Roots Rocky Reggae" yenyewe.
3. Kasikilize nyimbo za Bob kama "Jah live" "Jump Nyabinghi" "Roots Rock Reggae" "Chant Down Babylon" "Them Belly Fully" "Bad card" "Concrete Jungle" "Kaya" najua kwa uelewa wako umeishia zile nyimbo common kama "No woman no cry" "Africa Unite" "Zimbabwe"
4. Fanya hayo hapo juu No. 3 halafu uje ufute huu uzi wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ungekua msikilizaji mzuri wa reggae ungefahamu Bob Nesta Marley na Luck Dube wanapiga aina tofauti ya reggae nikiwa na maana Bob Marley alipiga Roots Reggae na Lucky Dube alipiga Sweet Reggae.

Katika tasnia ya muziki wa reggae inaonyesha tayari hivyo ni vionjo tofauti vya muziki.

Usifananishe Bob Marley na vitu vya kijinga kabisa

Nasisitiza Bob Marley mfananishe na kina Peter Tosh, Joseph hill, Israel Vibration ana Alpha Blondy halafu huyo Luck Dube mfananishe na kina kin Senzo.


Full Stop
 
UMEUA MKUU...
Ungekua msikilizaji mzuri wa reggae ungefahamu Bob Nesta Marley na Luck Dube wanapiga aina tofauti ya reggae nikiwa na maana Bob Marley alipiga Roots Reggae na Lucky Dube alipiga Sweet Reggae.

Katika tasnia ya muziki wa reggae inaonyesha tayari hivyo ni vionjo tofauti vya muziki.

Usifananishe Bob Marley na vitu vya kijinga kabisa

Nasisitiza Bob Marley mfananishe na kina Peter Tosh, Joseph hill, Israel Vibration ana Alpha Blondy halafu huyo Luck Dube mfananishe na kina kin Senzo.


Full Stop

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sjawai ona reggae ya lucky dube ni orijino hata sku1 ,,naonaga ni kama nyimbo za kwaya,..yaan hana tofaut na waimba bongo fleva wa bongo wanaojidai wanaimba RnB..hiv RnB wanaijua,hyo waachie kina Usher,rkely na chris brown

Sasa ndo lucky dube,yaan kabisa unafananisha regae ya jamieka na ya africa...

We lazima ni mchaga tuu
 
Wazee acheni kumzodoa mwenzenu ashakosea basi inatosha.

Sent using Jamii Forums mobile app
Haitoshi lazima aelekezwe ukweli, uwezi kumfananisha Dube na Marley kila mtu aliwika kwa zama zake na kila mtu ana vibes zake Bob ni mkubwa na Lucky ni mkubwa pia wote walifanya kazi nzuri kwenye ulimwengu wa reggae,
Lucky aliinogesha reggae na vionjo vya Africa, nampenda zaidi Dube ila ukweli Bob Marley ndo Mfalme wa reggae worldwid.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom