MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Kwa kuzingatia historia na taratibu za uendeshaji wa mabunge yote ya nchi zote chini ya jumuiya za madola hasa kwa nchi zinazoheshimu siasa zenye misingi ya demokrasia ya vyama vingi, adhabu walizopewa wabunge wote wa upinzani hazikubaliki na si utaratibu wa kiungwana, haiwezekani na haitowezekana huu uonevu kuendelea kwa kuzingatia wabunge hao ni wawakilishi wa wananchi kwahiyo hapa ni kuwaonea wananchi, maamuzi ya kamati ya maadili sio maamuzi ya Mungu yanaweza kutenguliwa inapowezekana kwa kuzingatia maslahi mapana ya taifa.
Wabunge wote wanazo haki za kuzidai haki zao mahali popote kwani maamuzi ya Naibu spika ndiyo sababu ya haya yote, kutaka kuziba midomo ya wabunge wanaoibua madudu ya serikali ndio chanzo cha haya yote! Bunge ni taasisi ya umma ambapo ni mahali pa kutatua na kuziwakilisha kero za wananchi, nasema wabunge wote waliosimamishwa bahati nzuri ni wasomi wazuri wanao uwezo wa kuchukua uamuzi wowote watakaoona unafaa kuhakikisha kua huu udhalimu unatokomezwa mapema kabla haujajiotea mizizi, ni haki yao kutokukubaliana na maamuzi ya kamati ya maadili ya bunge kutumia ubabe kufanya maamuzi tena yasiyozingatia taratibu na ustaarabu kutokana hali halisi ya wakati uliopo.Wasidhani kua hizi adhabu ni fundisho kwa wabunge waliowasimamisha zaidi ya kuibua hisia na hasira za wananchi wanaowawakilisha.
Ni wakati wa kamati kutafakari upya kupima kama uamuzi iliouchukua una faida kwa wananchi nje na njama za kutaka kuziba midomo ya watetetezi wa wanyonge, kamati inatakiwa kuzingatia katiba ya nchi katika kufanya maamuzi kwa kutazama wakati,mazingira na aina ya bunge lililopo! Wabunge waliofukuzwa wanaweze kurejeshwa Mara moja, hiyo sio adhabu ni uonevu.
Wabunge hawa waliosimamishwa ambao walikuwepo mambunge yaliyotangulia kama ni watovu wa nidhamu ilikuaje hawakuwahi kuadhibiwa adhabu kama hizi miaka yote iliyopita? Kama ni watovu wa nidhamu ilikuaje wananchi wakawapa ridhaa ya kurudi tena bungeni? Kwanini waadhibiwe wabunge wa upinzani tu? CCM hakuna wabunge watovu wa nidhamu?
Mfano kusimamishwa vikao 10 kwa mbunge wa Tarime vijijini John Heche eti kwa kosa moja tu sio sahihi kabisa na ni uamuzi mbovu kuliko uamuzi wowote ule,Hii adhabu ni kubwa mno iliyopitiliza na kuvuka mipaka kutaka kumkomoa mbunge. Kamati lazima itengue uamuzi wake haraka kwani hawa wabunge ni wengi na kwa kuzingatia michango yao ndani ya bunge tena yenye maslahi kwa umma! Huwezi kusimamisha mbunge vikao 10 kwa kosa moja tu ilihali kuna wabunge wanaotukana na kufanya udhslilishaji wa kijinsia ndani ya bunge unawaacha tu.
Hatujengi nchi kwa kuziba midomo ya watu kwa sababu tu kuna upande unajiona uko sahihi kuliko upande mwingine kwa kukosa mizania inayoakisi misingi ya kidemokrasia. Ninaamini wabunge wote waliosimamishwa kutokukubaliana na adhabu hizo, uamuzi wa kamati lazima utenguliwe! nchi ni yetu sote,bunge ni letu sote na wananchi ni wetu sote! Ubabe hautalifikisha taifa mahali sahihi, haki itendeke mahali pote.