Elections 2010 Wengi wa wanafunzi wa vyuo vikuu kutopiga kura 2010

Kuna uthibitiisho kuwa mwaka huu vyuo vikuu vyote vitaanza mwaka wa masomo mpya mwezi wa kumi na moja soon after uchaguzi. wachambuzi wanasema hi ni janja ya CCM kuzuia wanachuo wasipige kura kwani wengi si wana CCM, na wengi wangepigia upinzani. wanajua fika wengi wamejiandikisha maeneo ya chuoni. jamani mbona wanawanyima watu haki ya kupiga kura? I hate being tanzanian and live here, am strugling to go and live abroad where life there make sense.

nasikitishwa na kauli ya kuchukia kuwa mtanzania na kufikiria kuwa mkimbizi katika mataifa ya wenzako.tambua hata mataifa ya unayotaka kwenda nao walikuwa na matatizo yao wakatafuta ufumbuzi na si kukimbia , mzalendo hawezi kukubali kuwa mkimbizi katika mataifa ya wengine. jawabu si kukimbia bali kutafuta ufumbuzi wa tatizo
 
Masa naomba ukumbuke wengi wetu tunatoka familia za aina gani hata niwe na hiyo nauli ya nenda rudi nenda rudi!!!

kuna watu hata kwenda September Conference ni tabu jamani ije kuwa kwenda kupiga kura??

Najua ila kila kitu kina gharama zake!

if education is expensive, try ignorance

Kuliko kuacha hali kama ilivyo nmetoa option kama hawawezi safiri watoe elimu ya uraia
 
Democracy kwenye nchi ya watu inakufaidia nini?bado ni utumwa ule ule..Asikudanganye mtu eti kwa kuwa unadhani Marekani kuna Demokrsai absi ukienda huko ndio itakusaidia,hakuna kitu kama hicho..Believe me kama sio mzawa shida iko pale pale..waulize wenzako,wanaishi kama watumwa vile wakati wangekuwa nchi zao wangekuwa mbali sana..Tatizo hukabiliwa na sio kukimbiwa..Wote tukikimbia nani sasa atakuwa mkombozi?

Umezidisha mkuu wangu. Mara nyingi tu nchi za wenzetu unaweza kuwa huru kuliko huku nyumbani. Kuna jamaa yangu huwa anasema anasumbuliwa karibu na kila mtu akiwa TZ wakati nje hana pressure hizo. Ila bado anapenda nyumbani na kwamba TZ kuna more opportunities kama mwenye nchi kuliko zile ambazo anazipata ugenini. TZ siku moja anaweza kuwa rais wakati ughaibuni uwezekano ni zero.

Ila tu si vizuri kukimbia tatizo na ni kweli ukiwa nchi za watu utaendelea kuwa mgeni mpaka unakufa hata kama maisha yako hayatakuwa na shida zozote.

Niliwahi kutembelea UK japo ni kwa miezi mitatu tu lakini niliona maisha poa ukiachia kimbia kimbia ya kwenye kazi. Lakini ni bora uchape kazi kuliko kunyanyaswa kila siku na wenye nchi yao huku nyumbani TZ. Mimi tutabanana nao hapa hapa.
 
Nimezidisha au nimejumlisha..Uhuru upi huo unaozungumzia wewe?ambao ni mzuri kwenye nchi za watu kuliko home sweet home..Utakuwa na matatizo tu wewe,yaani kwenu hakuna hauko huru kuliko kwa watu.Duu!
 
Hivi jamani hawa wanaosoma vyuo vikuu na walijiandikishia kwenye vyuo vyao, Je watapikaje kura wakati vyuo vinafunguliwa mwezi wa kumi na moja........................
Je hizi haziwezi kuwa ni njama za CCM kwa kuwa inajua kuwa upinzani unaungwa mkono na vyuo vikuu????
Jamani naomba tulijadili kwa kina
 
DEVIDE AND RULE.....! wapiga kura ni wa vyuo vikuu pekee? AU UNAMAANISHA WALE WANAOFADHILIWA NA CHAMA CHA VIDOLE VIWILI KUANZISHA MIGOMO NA HALI TETE VYUONI KWA MANUFAA YA KISIASA?
 
DEVIDE AND RULE.....! wapiga kura ni wa vyuo vikuu pekee? AU UNAMAANISHA WALE WANAOFADHILIWA NA CHAMA CHA VIDOLE VIWILI KUANZISHA MIGOMO NA HALI TETE VYUONI KWA MANUFAA YA KISIASA?
Namuunga mkono aliyekwambia uiondoe avatar ya Mwalimu Nyerere kwenye jina lako kwa sababu kwa kweli unamdhalilisha sana Mwalimu ambaye alikuwa akitetea haki ya kila mtu including wasomi. Asingelikubali ujinga huu wa mbinu za kipumbavu za kutaka kuwaengua wanachuo katika kupiga kura kwa kuogopa kwamba kura zao zitaende kwa vyama vya upinzani. It is a shame kwa CCM chama ambacho kinajidai kinatetea Demokrasia na Utawala wa sheria.
 
Ninachowaomba hawa vijana walionyimwa haki yao. watumie wakati huu wakiwa majumbani kuwaelezea wazazi ndugu jamaa a marafiki juu ya yote haya.
ili wazazi wachambue mchele na chuya
 
Nchi imeoza.ninasoma huko.ila uwezo wetu kuchambua mdogo.hakuna aliyewahi kufikiria jambo hilo.labda ingekuwa wamenyimwa mikopo
 
Kufuatia vyuo kufunguliwa baada ya uchaguzi wanafunzi wengi wameachwa njia panda maana walijiiandikisha wakiwa vyuoni na hwajui vipi watafanya na wanaona kama haki yao ya msingi inaondolewa. Sijui hii huwa inakuwaje?
 
Hii tulishaiongelea hapa jamvini na wengi walisema kuwa ilikuwa ni janja ya mafisadi kujaribu kupunguza kasi ya wanafunzi. Lakini nashukuru SAUT wengi watapiga kwani watakuwa washarudi chuo. Kwa upande mwingine naona sawa tu manake kama wasomi wenyewe ndo walewale tulowaona UDOM wamedanganywa kwa kuvalishwa jezi za njano na kijani na kupewa juice na maji wakiimba masifu ya sera ambazo wao wenyewe wanajua wazi kuwa hazikutekelezeka bora wasipige!
 
hii ni janja yao kwani wanajua vyuoni hawadanganyiki ovyo, nakumbuka uchaguzi uliopita nilikua hapo mlimani na kikwete na keenja waliona chamoto, kwa iyo wamejifunza kutoka uchaguzi uliopita!
 
Nasikia SAUT ni mwiba kwa Masha, maana nasikia alishaenda akawaambia mapadri mapato yao kwa mwezi ni tsh ngapi ili chuo kisifunguliwe jamaa wakasema hawahitaji pesa wanahitaji vijana wawahi shule kusoma. Akakimbilia kwenye kumwekea pingamizi kipenzi cha wana SAUT nako amefeli. Bora ajitoe tu sasa mwenyewe.
 
Masha SAUT haingii wala nini!
 
Hii tulishaiongelea hapa jamvini na wengi walisema kuwa ilikuwa ni janja ya mafisadi kujaribu kupunguza kasi ya wanafunzi. Lakini nashukuru SAUT wengi watapiga kwani watakuwa washarudi chuo. Kwa upande mwingine naona sawa tu manake kama wasomi wenyewe ndo walewale tulowaona UDOM wamedanganywa kwa kuvalishwa jezi za njano na kijani na kupewa juice na maji wakiimba masifu ya sera ambazo wao wenyewe wanajua wazi kuwa hazikutekelezeka bora wasipige!

UDOM ni jamvi la wahuni na watoto wa wakulima wamekusanywa pale hawajui hatima yao! Wanshabikia wasichokijua kama majuha....! Nyerere aliwaita jina zuri san watu wa aina hii: "M-A-Z-U-Z-U". Na ndivyo UDOM walivyo...!

Mimi nimeshajitolea, kwa mwanachuo yeyote aliye mkoani anayedhania anaweza kuja kupiga kura October 31 na aje mimi nita-mhost ilimuradi ajilipie usafiri wa kuja na kurudi.

Wananikera sana genge hili la mafisadi!
 
UDOM si wanafunzi si watawala, hawajashtuka kuwa wanatumika kama mabango ya kampeni. Ngoja hao madogo wamalize shule halafu hakuna kazi ndio wataelewa maana ya kutumiwa. Wenzao wa UDSM walishazoea kutendwa sasa wamejifunza kugangamala na maisha na si kusubiri kubebwa
 
ni wanafunzi wachache waliojiandikisha wakiwa chuo kwa sababu wengi wao hupenda kushiriki uchaguzi wakiwa nyumbani kwa vile wana uelewa wa umuhimu wa kura.
 
kura za udsm ndio zinauma zaidi lakini watumwa wa udom haina shida?pia mnatamka udom kuna makundi tofauti kundi la social science wengi ni makada wa chadema ila infomatics pamoja na education ndio sisiemu damudamu
 
Ccm inajua kuwa katika taasisi za vyuo vikuu hawana mtaji. Wameamua kuwatawanya ili kwamba kama wanafunzi walijiandikisha wakiwa chuoni basi hawatapiga kura.hii yote ni janja ya ccm tu.
Lakini nafikiri ni vyema sasa wasomi hawa wakapeleka elimu kwa wanakijiji kuhusiana na hali halisi ya maisha ya mtanzania wa leo.fikra pevu na zenye kuzaa matunda,fikra endelevu.ni wajibu wetu kufanya haya.
 
Back
Top Bottom