Wengi wa wanafunzi wa vyuo vikuu kutopiga kura 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wengi wa wanafunzi wa vyuo vikuu kutopiga kura 2010

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by kmp, May 20, 2010.

 1. kmp

  kmp Member

  #1
  May 20, 2010
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wednesday, 19 May 2010

  SERIKALI imetoa waraka unaovielekeza vyuo vikuu vyote nchini, kuchelewa kuanza muhula wa masomo kwa mwezi mmoja, ili kupisha uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.

  Kwa mujibu wa waraka huo, badala ya kuanza Oktoba kama ilivyozoeleka, muhula kwa vyuo vikuu vyote katika mwaka huu, utaanza juma la kwanza la Novemba, baada ya kumalizika uchaguzi huo wa madiwani, wabunge na rais.

  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe, alisema vyuo hivyo vitafunguliwa kati ya Novemba 4 na 5.

  Hata hivyo alisema hatua hiyo haitokani na uchaguzi na kwamba inatokana na mabadiliko yanayotarajiwa kufanywa na serikali katika utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini.


  "Fedha zinazohitajika kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi mwaka huu ni nyingi sana, zinafikia Sh250 bilioni ni pesa nyingi, kwa hiyo tunaandaa utaratibu mpya ambao tunatarajia utakuwa umekamilika ifikapo Novemba 3,"alisema Waziri.


  Profesa Maghembe alisema hata mwaka wa masomo uliopita, vyuo vikuu vilifunguliwa Oktoba 25 na kwamba kuwa tarehe hiyo haipishani sana na ya kufunguliwa kwa vyuo hivgo katika mwaka huu.


  "Tatizo kila kitu kinachofanywa sasa na serikali kinahusishwa na uchaguzi kwa sababu tu tunaelekea kwenye uchaguzi lakini hili la kufunguliwa kwa vyuo Novemba, halina uhusiano kabisa na uchaguzi,"alisisitiza Profesa Maghembe.


  Waziri Maghembe alisema utaratibu wa mpya wa utoaji wa mikopo ambao hakuwa tayari kuuweka wazi, utasaidia kuharakisha ulipwaji wa mikopo hiyo ili wanafunzi watakaporejea vyuoni, wakute mikopo hiyo ikiwa tayari.


  Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU), Profesa Mayunga Nkunya, alithibitisha kupata taarifa kuhusu hatua hiyo.

  Profesa Nkunya alisema, katika kipindi cha Oktoba, wanafunzi wengi watakuwa wakishughulia mikopo kutoka bodi ya mikopo na kwamba halitakuwa jambo zuri kazi hiyo isiingiliane na uchaguzi mkuu.

  mwisho

  Source: Vyuo vikuu sasa kufunguliwa Novemba
   
 2. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,477
  Likes Received: 1,429
  Trophy Points: 280
  CCM bana wajanja sana, wale wote waliojiandikisha vyuoni ina maana hawatapiga kura kwa kuwa watakuwa nyumbani, na tasmini inaonyesha wanavyuo wengi hawana mpango na CCM
   
 3. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  siasa na elimu wapi na wapi?
   
 4. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #4
  May 20, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Ndio mpango wao wameshaona mambo yao hayaendi vizuri.
   
 5. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #5
  May 20, 2010
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  duh!
   
 6. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #6
  May 20, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,060
  Likes Received: 24,064
  Trophy Points: 280
  Kama mafuta na maji.
   
 7. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #7
  May 20, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Uzandiki sana huu
   
 8. kmp

  kmp Member

  #8
  May 20, 2010
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna wakati nilisikia siasa zimepigwa marufuku katika taasisi za elimu, mimi najiuliza hv mbona hawa SISIEM wanaendelea kufungua matawi katika taasisi hizo? Juzujuzi hapa niliona wamefungua tawi la wanafunzi wa UDOM, hii inakuwaje?
   
 9. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #9
  May 20, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Huu mpango sio Mzuri kabisaa CCCM NA SERIKALI YAKE WAZANDIKI
   
 10. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #10
  May 20, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  kama kuna anayetoka chama cha upinzani hapa, tunaomba apeleke habari kwenye makao yake makuu waende kupinga haraka iwezekanavyo hii change ya kisigino, au kama inakaa hivyo, basi wanafunzi wote waliojiandikisha kupiga kura sehemu za vyuo vyao wapewe nafasi ya kujiandikisha tena ili wasikose opportunity ya kupiga kura zao....kama mtu alijiandikisha pale mlimani muda huo atakuwa mwanza atapigaje kura sasa, mwingine ata kuwa songea, mwingine atakuwa tanga mwingine zenji, watapigaje kura au watasafiri? hapa haiwezekani kabisa...itabidi hili lipigiwe kelele hadi waweke utaratibu mzuri kufanya hawa wanafunzi wote wanapata haki ya kupiga kura.
   
 11. Magpie

  Magpie Member

  #11
  May 20, 2010
  Joined: Aug 26, 2009
  Messages: 70
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii habari inachanganya sana mwanzoni inasema kua serikali imesogeza mbele ufunguaji wa vyuo ilikupisha uchaguzi mkuu, waziri anasema wanasogeza mbele kwasababu wanaanza kutumia mfumo mpya wa utoaji mikopo,...kazi kweli kweli.....

  na nivizuri tume ya uchaguzi ikatoa tamko nini hatma ya wanafunzi na baadhi ya wafanyakazi wa vyuo ambao wamejiandikisha kupiga kura wakiwa vyuoni na niwazi hawatakuepo vyuoni wakata wa zoezi la kupiga kura likiendelea...watawezaji kupata fursa ya kupiga kura...?!!
   
 12. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #12
  May 20, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Kuna uhusiano gani kati ya uchaguzi na masomo?.,kwani wakiwa vyuoni uchaguzi hautofanikiwa.,hapa serikali imechemka au ndio mikopo ya wanafunzi imeingizwa kwenye bajeti ya Kampeni sasa wanaogopa zahma la wanafunzi pale watakapofungua chuo na kukuta hakuna ankara zao?
   
 13. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #13
  May 20, 2010
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Ikiwezekana vifunguliwe mpaka Rais atakayechaguliwa akishaapishwa!..Agrrrrr!!Kero za ccm!
   
 14. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #14
  May 20, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  This shame to government hata vyuo vyetu unaweza kusikia wanakubali, SHAME ON THEM
   
 15. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #15
  May 20, 2010
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kwa kuwa wale waliojiandikisha watachagua wabunge wa sehemu waliojiandikishia, na kwa kuwa wanachuo wengi walijiandikishia katika vituo vilivyopo ndani ya shule zao. Je kuvifungua vyuo baada ya uchaguzi, sio kuwazuia wanaelimu ya juu kuwachagua wawakilishi, haswa wabunge na madiwani? Je si hofu ya ccm kuwa itapoteza majimbo yaliyo na vyuo hivi endapo wanachuo watashiriki uchaguzi huu wakiwa vyuoni. Kama haya ni kweli, nini kifanyike? Je, vyama vya siasa vimechukua jukumu gani kupingana na suala hili kama linaashiria mbinu mpya za ccm kushinda kwa mbinu?
  Fuatilia hapo chini!

  ++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

  Wednesday, 19 May 2010

  Fredy Azzah


  SERIKALI imetoa waraka unaovielekeza vyuo vikuu vyote nchini, kuchelewa kuanza muhula wa masomo kwa mwezi mmoja, ili kupisha uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.

  Kwa mujibu wa waraka huo, badala ya kuanza Oktoba kama ilivyozoeleka, muhula kwa vyuo vikuu vyote katika mwaka huu, utaanza juma la kwanza la Novemba, baada ya kumalizika uchaguzi huo wa madiwani, wabunge na rais.

  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe, alisema vyuo hivyo vitafunguliwa kati ya Novemba 4 na 5.


  Hata hivyo alisema hatua hiyo haitokani na uchaguzi na kwamba inatokana na mabadiliko yanayotarajiwa kufanywa na serikali katika utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini.


  "Fedha zinazohitajika kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi mwaka huu ni nyingi sana, zinafikia Sh250 bilioni ni pesa nyingi, kwa hiyo tunaandaa utaratibu mpya ambao tunatarajia utakuwa umekamilika ifikapo Novemba 3,"alisema Waziri.


  Profesa Maghembe alisema hata mwaka wa masomo uliopita, vyuo vikuu vilifunguliwa Oktoba 25 na kwamba kuwa tarehe hiyo haipishani sana na ya kufunguliwa kwa vyuo hivgo katika mwaka huu.


  "Tatizo kila kitu kinachofanywa sasa na serikali kinahusishwa na uchaguzi kwa sababu tu tunaelekea kwenye uchaguzi lakini hili la kufunguliwa kwa vyuo Novemba, halina uhusiano kabisa na uchaguzi,"alisisitiza Profesa Maghembe.


  Waziri Maghembe alisema utaratibu wa mpya wa utoaji wa mikopo ambao hakuwa tayari kuuweka wazi, utasaidia kuharakisha ulipwaji wa mikopo hiyo ili wanafunzi watakaporejea vyuoni, wakute mikopo hiyo ikiwa tayari.


  Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU), Profesa Mayunga Nkunya, alithibitisha kupata taarifa kuhusu hatua hiyo.

  Profesa Nkunya alisema, katika kipindi cha Oktoba, wanafunzi wengi watakuwa wakishughulia mikopo kutoka bodi ya mikopo na kwamba halitakuwa jambo zuri kazi hiyo isiingiliane na uchaguzi mkuu.
  mwisho
   
 16. K

  Keil JF-Expert Member

  #16
  May 20, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Prof. Maghembe juzi katangaza kwamba vyuo vya elimu ya juu vitafunguliwa Novemba baada ya Uchaguzi Mkuu. Sababu ya kusogeza mbele tarehe ya kufungua vyuo ni kwamba Bodi ya Mikopo watakuwa wana process mikopo ili wanafunzi wakifungua vyuo wasianze kuhangaika kufuatilia mambo ya mikopo.

  Hapa ninaona kuna siasa imeingizwa kwenye hili swala. Kuna mambo ambayo mimi ninajiuliza na ninayatilia mashaka sana.

  1. Je, Bodi ya Mikopo ambayo inafanya hayo marekebisho ya utoaji mikopo wanahitaji muda gani kufanya hayo marekebisho mapya? Kwa muda wote ambao wamekuwa ofisini ina maana walikuwa hawajui kama kuna marekebisho?

  2. Mwaka jana vyuo vilifunguliwa Oktoba 25, hizo wiki mbili walizoongeza mwaka huu zitasaidia nini katika kufanya marekebisho ambayo Waziri hayasemi? Hata kama idadi ya wanafunzi ambao wanaingia kwenye vyuo vya elimu ya juu imeongezeka, lakini wana miezi 3 ya kushughulikia hilo swala la mikopo, hizo wiki 2 walizoongeza ni za nini?

  Katika kutafakari kwangu haraka haraka, nimehisi yafuatayo:

  1. Kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi kwenye vyuo vya elimu ya juu, serikali imeanza kuhofia kwamba kwenye majimbo ambayo vyuo vya elimu ya juu vipo, kunaweza kuwa na ushindani mkubwa sana na hivyo CCM inaweza kupoteza viti.

  2. Serikali imekuwa kwenye msuguano na wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu kutokana na tatizo la mikopo, kwa hiyo CCM inahisi kwamba wanafunzi wanaweza kujitokeza kwa wingi ili kupiga kura ya chuki kwenye maeneo yao na matokeo yake CCM itagalagazwa.

  Kutokana na hizo hisia hapo juu, serikali imeamua kwa makusudi kuwanyima haki wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu ili wasipige kura.

  Inaeleweka wazi kwamba mpiga kura, hupiga kura yake mahali alipojiandikisha. Kama hao wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu wamejiandikisha kwenye vituo ambako wanasoma, je wataruhusiwa kupiga kura huko makwao ambako hawakujiandikisha??? If YES, nani ata-verify kwamba huyu hajajiandikisha mara mbili? Hapa ndipo ninapohisi kunaweza kuwa na mchezo mchafu wa shahada za kupigia kura.

  Ukichukua UD main campus peke yake inawezekana ikawa na wanafunzi zaidi ya 10,000, hao ni wengi sana kama wapiga kura ndani ya jimbo, lakini ukiwasambaza wakapigie kura mikoani/makwao, impact ya hizo kura inapungua na hivyo kupunguza ushindani kwenye majimbo ambayo yana taasisi za elimu ya juu.

  Vyama vya upinzani wanatakiwa kulichunguza hili na kulifanyia kazi kwa kuwa linaweza ku-work against upinzani. Hapa ndipo Mnyika na CHADEMA wanatakiwa kuwa makini na wale waliojiandikisha kama wapiga kura pale UD.

  Huu usanii mwingine haufai kabisa, tukianza kuchanganya academics na siasa hii nchi haitakuja kusonga mbele. Hapa ni sawa na kucheza na elimu ya watu. Mabadiliko ya wiki mbili ni makubwa na yanaharibu schedule ya semester na mwaka mzima wa masomo.
   
 17. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #17
  May 21, 2010
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,844
  Likes Received: 1,110
  Trophy Points: 280
  Aise hapa kweli, kikubwa hapa wanaogopa sana majimbo ya Kawe na Ubungo. CCM wahuni sana, hii haiwezekani yaani wapiga kura wote hao wakose kupiga kura? Kwanini woga huo wameupata sasa? mwaka 2000 tulikuwa na mgomo pale UDSM, hawakutufukuza mpaka tulipomaliza kupiga kura ndiyo wakatufukuza tukarudi vyuoni Jan. 2001.

  CCM wanahali ngumu sana kipindi hiki.

  Naungana nawe kuwaomba viongozi wa vyama vya upinzani kulipigia kelele suala hili mpaka kieleweke. Bila kura za wanachuo Mnyika hawezi kupita pale Ubungo.
   
 18. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #18
  May 21, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Profesa Maghembe alisoma wapi hadi akawa profesa? Yaani yeye bado anataka kuendesha elimu ya juu kama jeshi la mgambo bila kuangalia nafasi ya vyuo vyetu katika dunia ya leo? Hajui kuwa baadhi ya wanafunzi hao wanatakiwa kwenda kusoma nchi za nje, na vile vile kutakuwa na wanafunzi wa kutoka nchi za nje wanaotaka kusoma Tanzania?
   
 19. Bob

  Bob JF-Expert Member

  #19
  May 21, 2010
  Joined: Sep 10, 2007
  Messages: 277
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Council ya chuo ndiyo anayopanga au kupitisha almanac ya chuo. Hii sio kazi ya wizara hivyo Prof. Magembe hahusiki. Hii ipo wazi kwenye University Charter.
  Kwa upande mwingine Tanzania Commission for University (TCU) has coordinated the selection process and made it simple. For that matter the Loan Board can have all information about the selections before mid-June, as the application deadline is at the end of May.
  For that reasons, Prof. Magembe narrations lacks reasonable justification.
   
 20. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #20
  May 21, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135

  MKuu huu ni maongo wa CCM kuzoofisha Upinzani, 2005 nilikuwa na watoto wangu pale UDSM but hawakupiga kula mana waliambiwa majina yao hayapo kwenye daftari la wapiga kura.

  CCM imeona Mnyika wa Ubungo atashinda lakini hapa wanatengenezea mizengwe hili akose kula za UDSM. 2005 80% ya wanachuo walikuwa namusupport JOhn Mnyika


  NB: JOHN MNYIKA KUWA MAKINI KWA HILI KURA ZAKO ZINAPOTEA
   
Loading...