Wengi tunahitaji kujua tafsiri ya 'Breaking news'

i think this simply means the latest hottest news!!!



they say this..............habari zinazotufikia hivi sasa..................
 
Hivi majuzi niliwasikia TBC1 wakiita "Habari Mpasuko"

Hii ya kutaka kutafsiri kila kitu kama kilivyo toka kwenye english na kwenda kwenye kiswahili itatufikisha pabaya. Hii habari mpasuko!!! Hmmmm!....imekaa kiajabu ajabu wangetafuta neno jingine lililotulia.
 
Hii ya kutaka kutafsiri kila kitu kama kilivyo toka kwenye english na kwrnda kwenye kiswahili itatufikisha pabaya. Hii habari mpasuko!!! Hmmmm!....imekaa kiajabu ajabu wangetafuta neno jingine lililotulia.
Tafsiri ya neo kwa neo inaweza leta maana tofauti kwa jamii.Mfano tafsiri FEEDBACK....
 
Hili neno 'Breaking news' nafikiri linatumiwa ndivyo sivyo.
Hakika nakuunga mkono maana ninachojua mimi ni kwamba "Breaking News" ni taarifa ambayo inakuwa ndiyo inatoka wakati ule unapokuwa unawataarifu wana JF ni "LIVE" event japo si lazima tulione kama tuonavyo katika TV. Sasa leo mtu akipata taarifa ya siku nne ama tano zilizopita anaandika "Breaking News" Ni makosa kwa kweli. Kitu kingine taarifa hiyo inabaki hapa JF kwa muda mrefu hata miezi mitatu ama zaidi kwa kichwa cha habari "Breaking News"
Labda tukimuomba Mod awe anafuta neno "Breaking News" baada ya muda kupita, tungeleta maana halisi.
 
...Nyie acheni iwe breaking news hivyo hivyo mkitaka kutafsiri kila kitu mtatoka na maneno ya ajabu...Kifupi ni habari zinazopatikana muda huo huo (live) au zilizopatikana muda mfupi uliopita na kwa vyovyote vile watu zitawavutia kama si kuwastua....
 
Tafsiri ya neo kwa neo inaweza leta maana tofauti kwa jamii.Mfano tafsiri FEEDBACK....


hii kuna mwalimu wetu mmoja kule Galanos enzi hizo alituambia linaitwa Mlishonyuma.Yaani we acha tu,maanake ni direct translation bila breki
 
ebwana hli neno sina hakika kama BAKITA wameshalipatia neno la kiswahili.Nijuavyo ni 'istilahi' katika uga wa habari.
Nafikiri tuwashirikishe BAKITA kusudi watu waache kulitumia visivyo.Kuita 'habari mpasuko' nahisi siyo sawa.sijui....labda 'habari za papohapo', 'habari mpya'
 
Back
Top Bottom