Wengi hawajui kama simu za zamani zinaweza kutumika kutengeneza vitu vingine | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wengi hawajui kama simu za zamani zinaweza kutumika kutengeneza vitu vingine

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Bikra, Aug 6, 2009.

 1. Bikra

  Bikra Senior Member

  #1
  Aug 6, 2009
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 103
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wateja wa NOKIA Tanzania wametakiwa kuzipeleka simu zao za zamani ambazo hawazitumii kwenye ofisi zao za Dar es Salaam katika mpango wa Nokia wa kurudisha simu zilizotumika na kuongeza kiwango cha kuzirecycle simu za zamani.
  Kwa mujibu wa utafiti wa NOKIA, watu watatu kati ya wanne duniani hawafikirii kabisa ku-recycle simu zao huku karibu ya nusu yao hata hawajui kama inawezekana ku-recycle simu zilizotumika.

  Utafiti wa NOKIA ulihusisha kuwahoji watu 6,500 katika nchi 13 duniani ikiwamo Nigeria ambayo iliwakisha soko la Afrika. Utafiti huo ulifanywa na NOKIA ili kujua mwenendo wa wateja wa simu kuhusu kurecycle ili kuusaidia mpango wa kampuni hii wa kurudisha simu zilizotumika na kuongeza kiwango cha kuzirecycle simu za zamani.

  Tanzania ni moja kati ya nchi ambazo watumiaji wake wengi hawafahamu kama inawezekana ku-recycle simu zilizotumika kitu ambacho kinaendana na matokeo ya utafiti wa NOKIA.

  “Watu wengi hawajui kama simu hizi zinaweza kuwa re-cycled. Na wengi hawajui namna ya kufanya re-cycling. Nokia inamrahisishia mteja kwa kumpa taarifa kupitia mpango wetu wa Kurudisha Simu kama huu tunaoushuhudia leo. Tunataka kila mtu atambue wapi ataweza kupeleka simu zake za zamani,” alisema Nicholas Maina, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa NOKIA Kanda ya Afrika Mashariki.

  Utafiti umeonyesha kuwa kama kila mtu kati ya watu bilioni 3 wanaomiliki simu wangerudisha simu angalau moja tu, itakuwa sawa na kuokoa tani 240,000 za malighafi ya kutengenezea simu na hivyo kupunguza athari za kimazingira hasa mabadiliko ya hewa. Malighafi tani 240,00 ni sawa na kuyaondoa barabarani magari milioni 4 ambayo yanatoa hewa chafu inayoathiri mazingira.

  Matokeo ya utafiti yanaonyesha pia kuwa pamoja na watu wengi kuwa waliwahi kumiliki wastani wa simu tano, chache sana zinakuwa re-cycled zinapokuwa hazihitajiki. Ni asilimia 3 tu ndo walisema wamere-cycle simu zao wakati asilimia 44 walisema wanazitunza nyumbani tu. Wengine walisema simu za zamani wanaziwapa ndugu na jamaa zao.

  Dunia kote, asilimia 74 ya watumiaji wa simu waliohojiwa walisema hawafikirii ku-recycle ingawa asimia 72 walikiri kwamba kufanya hivyo kuna faida kwa mazingira kwa. Majibu hayo yalifanana karibu katika nchi zote. Maina alisema hadi kufikia asilimia 80 ya simu za NOKIA zinaweza kuwa re-cycled na baadhi ya malighafi zinaweza kutumika kutengenezea bidhaa nyingine kama vile birika za kuchemshia maji, benchi za kukalia kwenye sehemu za mapumziko, vifaa vya kuzibia meno na hata kifaa kama saxophone na vifaa vingine vya bati vya muziki.

  Kati ya asilimia 65 na 80 ya simu moja ya zamani huweza kutumika kwa kazi nyingine na sehemu iliyobaki kama vile plastiki, hutumika kuwasha moto wa kuyeyushia sehemu za simu. Vifaa vingine hukusanywa pamoja na kubanwa na huweza kutumika katika ujenzi wa barabara au majengo. Kati ya nchi zilizofanyiwa utafiti, India iliongoza kwa kuwa na watumiaji wa simu wasiojua kama inawezekana ku-recycle simu ikiwa na asilimia 17 tu ya wanaojua, Indonesia asilimia 29 na nchi zilizokuwa na ufahamu mkubwa ni Uingereza ikiwa na asilimia 80 huku Finland na Sweden zikiwa na asilimia 66.

  NOKIA imeandaa maeneo ya kukusanya simu ambazo hazihitajiki katika nchi 85 duniani kote, mpango ambao ni mkubwa wa kujitolea katika sekta simu ya mkononi. Kwa Tanzania wateja wa NOKIA wanaweza kupeleka simu zao za zamani ambazo hawazitumii kwenye ofisi za Authentic-Harbour View Mall zilizopo mtaa wa Samora na Midcom Service Centre bara bara ya Alihassan Mwinyi.

  “Tunaitikia wito"
   
 2. Mlaleo

  Mlaleo JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2016
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 9,862
  Likes Received: 3,309
  Trophy Points: 280
  Zishasahaulika hizo Simu... Siku hizi zinaitwa Tochi kwa Jina Maarufu hata Lumia haijulikani sana
   
Loading...