mwana wa Tanzania
Member
- Nov 27, 2019
- 35
- 145
Nimeona tafsiri potofu/uelewa finyu kuhusu Kauli hiyo ya BASHIRU, Msingi wa kauli hiyo ni dhana ya kitaaluma ya INCUMBENCY ADVANTAGES inayotumika katika Political Science.
Chanzo cha tafsiri hio POTOFU inaweza kuwa uelewa hafifu wa dhana ya INCUMBENT ADVATANGE au inafanyika maksudi ili kupata manufaa ya kisiasa.
Nikiri wazi kwamba
1. Mimi ni mmoja wa Wanafunzi wa DKt BASHIRU ambapo nikiwa UDSM nasoma Shahada ya kwanza ya Sanaa katika Katika Siasa na usimamizi wa Umma alinifundisha Kozi inayohusu nadharia za masuala ya Uchaguzi.
2. BASHIRU amekuwa too academic kwa kutumia nadharia za kitaaluma jambo ambalo limechangia umma kwa sehemu kubwa kutoelewa ipasavyo ujumbe aliokusudia kuutoa
Katika taaluma ya Political Science, INCUMBENT is the current holder of an office or position usually in relation to election . Kwa tafsiri isiyo rasmi INCUMBENT ni anayeshikilia Ofisi au nafasi mara nyingi katika Uchaguzi.
INCUMBENCY ADVANTAGE
katika taaluma ya Sanaa ya Sayansi ya Siasa maana yake ni FAIDA au NAFUU inayopata Chama kilichopo Madarakani dhidi ya visivyo madarakani (Vyama Vya Upinzani).
NINI HASA BASHIRU ALIKUWA ANAMAANISHA?
Kwamba CCM kama vilivyo Vyama vingine kote Duniani vilivyopo Madarakani kina nufaika na faida ipasavyo na fursa ya kuwa Madarakani kwa kubuni na kusimamia miradi mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo SGR, Kufufua Shirika la Ndege, Afya, Elimu n.k ambayo inajenga imani ya Wananchi kwa Chama hicho katika kukipigia kura kwenye Uchaguzi.
Hivyo basi ni SAHIHI kusema CCM haitumii vyombo vya DOLA PEKEE kuendelea kubaki Madarakani bali na taasisi zingine zote za Umma.
Pia itakuwa ni SAHIHI kwa Vyama visivyo Madarakani mfano Chadema, ACT Wazalendo vikishika Dola kuitumia Kushinda au kuendelea kubaki Madarakani ili mradi vinafanya hivyo kwa mujibu wa Kanuni, taratibu na Katiba.
Hata hivyo HASARA ambayo huikumba Chama kilichopo Madarakani ni kushindwa kufikia matarajio ya Wananchi au kutotekeleza ahadi ilizotoa kwa Wananchi ambapo kwa Vyama visivyo Madarakani inakuwa faida kwake.