Wengi hamfahamu tulipotoka kabla ya matumizi ya plastiki kutamalaki

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,266
Miaka ya 1960 baada ya uhuru mpaka miaka ya 1970 bidhaa za nyumbani kama mafuta ya kujipaka yalikuwa yanafungwa katika vifungashio vya glass.

1575255103559.jpeg

Kuna wakati bidhaa za nje hazikuingia kabisa Tanzania. Tanga kulikuwa na kampuni ilitengeneza mafuta ya ngozi yalijulikana kama Asher’s Petrolium Jelly. Huwezi kuyakinganisha na Vaseline lakini yalitufaa na yalizashalisha ajira.

Mafuta ya kula yalifungwa kwenye makopo.

1575255418920.jpeg

Yaliuzwa kwenye maduka ya ushirika. Kila ushirika ulikuwa na duka lake. Ushirika wa wazee, wakina mama, walimu nk. Bidhaa ziliratibiwa na RTC ambako pia mauzo yalifanyika.

Ni baada ya milango ya biashara kufunguliwa awamu ya pili ndiyo tulianza kuzoea vitu kuwepo kwenye maduka ya watu binafsi bila kibali.

1575255773341.jpeg
 
Bidhaa nyingi za zamani ziliandikwa kiingeleza hata kama zimetengenezwa Tz je sababu ni kuwa watu walikuwa wameelimika au?
 
Daah, tumetolka mbali!!
Hio SUPA GHEE, tulipata mdada wa kazi naye akajua ni siagi ya kuweka kwenye mkate. Salama yetu mdogo wetu wa mwisho alimuona ndio akamshtua; tatizo dogo na akili zake za kitoto alimcheka sana dada wa watu na kumtania.
 
MKUU NASIKIA HATA KONDOM YA ZAMANI ILIKUWA INATENGENZWA KWA KUTUMIA UTUMBO WA NG'OMBE ULIOOSHWA VIZURI😂😂😂
Najua unatania lakini kondomu hazikuwepo kwa wingi. Zilikuwa chache sana na hazikuwa zinapatikana kwa urahisi. Mtu akiwa na kondumu angeweza kufanya maonyesho na kutoza watu fedha ili waiangalie.
 
Daah, tumetolka mbali!!
Hio SUPA GHEE, tulipata mdada wa kazi naye akajua ni siagi ya kuweka kwenye mkate. Salama yetu mdogo wetu wa mwisho alimuona ndio akamshtua; tatizo dogo na akili zake za kitoto alimcheka sana dada wa watu na kumtania.
Kipindi kile tan-bond iliungia mboga kama mafuta. Si kwa kutokujua ila hakuna mafuta unatumia ulichonacho. Lipstick zilikuwa eye shadow.
 
Najua unatania lakini kondomu hazikuwepo kwa wingi. Zilikuwa chache sana na hazikuwa zinapatikana kwa urahisi. Mtu akiwa na kondumu angeweza kufanya maonyesho na kutoza watu fedha ili waiangalie.
Miaka ipi hiyo Mkuu?
 
Kweli mimi ni babu sasa ndio nimeanza kushtuka picha ya vitu hivo vyote nimeshatumia na mpaka sasa sijaoa aisee niombeni mungu nitakufa nikiwa mhuni nini
Swala la ww kuweka bayani mwanamke wako unataka maombi ya nn ?
 
Back
Top Bottom