Wema Sepetu: Tafuta wataalamu wa jadi haraka iwezekanavyo.

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
17,370
21,062
Miongoni mwa mastaa wa kike ambao wasipojiangalia watakuwa na mwisho mbaya basi huyu mwanadada Wema Isaac Sepetu anaongoza.

Kiukweli Wema inabidi afanye juu chini atafute wataalamu wa jadi wamsafishie nyota yake maana anazidi kufuja kila kukicha .


Wema kwa muda mrefu amekuwa mtu mwenye mikosi kila atakalolifanya lazima liharibike, mfano kampuni yake ya endless fame imekufa kifo cha mende, vipodozi vyake,app yake na mambo mengi mno yamemdodea .


Tukiachilia mbali suala la biashara, Wema amejaa mikosi mpaka mwilini mwake kuna uwezekano mkubwa hata suala la kizazi amefungwa kimazingara japo yeye anahisi na kukiri tabia yake ya kutoa mimba usichanani mwake ndio chanzo lakini hapana atazame kwa wataalamu huenda kuna jambo limejificha nyuma ya pazia.

Tukija upande wa muonekano Wema amekongoroka mno mpaka inakuwa vigumu kupewa baadhi ya dili kutokana na mwili wake kutokuwa na mvuto tena maana amekuwa kimbau mbau ambaye haeleweki nyuma wapi mbele wapi ukija kwenye sura ndio kabisa uzee unamkaribia.

Kwa hiyo ushauri wa bure aende kwa wataalamu wamchekie nyota yake au kama anaona aibu awaite hata masheikh wamfanyie kisomo angalau cha siku saba mfululizo au siku tatu kikiambatana na swadaka kwa watoto yatima na maskini huenda mambo yake yatakaa sawa kwa idhini ya Allah.
 
Hiyo ni imani kama imani zingine na suala la imani linatofautiana baina ya mtu na mtu.

Huyo Wema uwezekano wa kufungwa kimazingara upo kabisa.
Wema anatia huruma saana, hivi majuzi alienda kwenye kaburi la baba yake akasema pembeni ya lile kaburi asizikwe mtu anataka akifa azikwe pale pembeni ya baba yake mzee izack.
Nkajisemea kimoyomoyo huyu mwanamke kakata tamaa ya maisha kabisa anataka afe tu ijulikane moja.
 
Amegalagazwa sana mpaka amefubaa

Siku moja nikiwa airport nilikutana na jamaa zangu

Tukawa tunapiga story mbili tatu na madreva tax, niliyoyasikia japo sikuthibitisha nihatari sana.

Somehow utowaji mimba ni moja ya viashiria kwamba alitumikisha sana mwili wake.

1. Mtu apandacho ndicho atakachovuna.

2. Uzee nao upo wala haukwepeki
 
Wema anatia huruma saana, hivi majuzi alienda kwenye kaburi la baba yake akasema pembeni ya lile kaburi asizikwe mtu anataka akifa azikwe pale pembeni ya baba yake mzee izack.
Nkajisemea kimoyomoyo huyu mwanamke kakata tamaa ya maisha kabisa anataka afe tu ijulikane moja.
Stress za maisha zinamchanganya, ila uwezekano wa kuwa amechezewa upo asidharau.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom