Wema Sepetu: “Niliposema watu waliniona mjinga lakini sasa Jokate kaumbuka”

Nyundo Kavu

Senior Member
Dec 6, 2011
186
85
Siku chache zilizopita, Wema Sepetu ambaye alikuwa mchumba wa Diamond kabla hajabwaga manyanga alilalama kwenye vyombo vya habari kuwa Jokate ameingilia penzi lake kwa msanii huyo, tuhuma ambazo miss huyo namba 2 aliziruka kwa kusema anasingiziwa.

"Si alikuwa anakanusha, sasa yako wapi?" Jane Swai, mchangiaji wa blogu (jina kapuni) alihoji wakati akitoa maoni yake kuhusu habari ya Diamond kutangaza rasmi kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na msichana huyo mwenye kidoti cheusi usoni na kwamba haoni mwingine wa kumpa penzi lake.

Wakati Jokate akisakamwa kwenye mitandao, Uswahilini nako hali si shwari ambapo dodoso nyingi zisizokuwa na uthibitisho wa kutosha zimekuwa zikitolewa kwamba mwanadada huyo kabla ‘kudeti' na Diamond ameshatoka na msururu wa wanaume wengine.

Wachache kati ya wanaume wanaotajwa mitaani na ambao Jokate amekuwa akikanusha vikali kutoka nao kama alivyokuwa akikana kwa Diamond ni Hashim Thabeet, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA' na Ambwene Yesaya ‘AY.'

"Jokate ni msiri lakini ameshatoka na (anawataja mastaa hao waliopo paragrafu ya juu) na hata …(anamtaja kijana mmoja ambaye baba yake ana wadhifa mkubwa serikalini) naye ametembea naye, hata mzee… (anamtaja mfanyabiashara maarufu nchini) ameshapita, ni vema awe wazi kuna siku ataumbuka," alidai Julieth John, mwanamitindo anayefanya shughuli zake jijini Dar es Salaam.

Siku chache tangu Diamond aanike kile kilichokuwa kikifichwa kati yake na miss huyo namba 2, mchumba wake wa zamani, Wema alitoa kauli hii: "Niliposema watu waliniona mjinga lakini sasa Jokate kaumbuka."
Jokate kwa upande wake amekuwa kimya.

Miss Jokate - Global Publishers
 
heshima kwako sukari ya warembo itageuka kuwa shubiri ya warembo.dunia ni hii na waendao ni viumbe.
 
Hakuna aliyemwona mjinga, ispokuwa watu walidharau kwa sababu ni story ya kijinga.
Hakuna na haja ya kupiga kelele, angetambaa tu.
 
Sio tu mjinga basi hajui anataka nini maishani mwake au anadhani watu wako after utoto na ujinga wao???watoto au limbukeni??
 
hii hadithi inathibitisha kwamba Jokate ni smart, mwerevu, mwenye staha, na bora kuliko Wema. So Diamond amefanya uamuzi sahihi.
 
Kama naona anguko la Diamond hivi.....kuna watu wanakula pesa kwa ajiri yake....huyu dogo angeachana na hawa mastaaa au angekuwa anakula kimya kimya na kuto wapa nafasi wanahababri...kuingilia mambo yake ya ndani...apige kazi ili aake kwenye game muda mrefu.
 
Kidume yupi ungekuwa kwenye position ya kulamba Wema usingepiga?? Position nyingine inakujia ghafla ya kupiga Jokate usingekula......????? Diamond watembezee ni wakati wako, ni msimu wako....
 
kweli malipo ni hapahapa duniani,auaye kwa upanga nae atakufa kwa upanga.thn ktu kngne celew hv hawa mastar hawawezfanya mambo kwa cri hadi mefia zjue.big ip steve r.i.p ulikuwa unafanya kimyakimya
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom