Wema Sepetu atupwa lupango

Naona hatimaye huyu Wema kaachiwa lakini kana ubangi bangi fulani. Watu wanaosema kumwombea fine..Lakini pia kuna kuvuna unachopanda..anataka kuonyesha kuwa anajua sana kupenda midume, mapenzi ya diazini hiyo ndiyo yalompelekea kuvunja kioo cha Kanumba na sheria ipo ili kutoruhusu mikanganyiko ya vurugu kupitia mapenzi uchwara...

WAZAZI..waache uchuro hapa, kuna asilimia zao nyingi kumfanya hivyo anavyoishi na anavyoonekana..Katika ustawi wa jamii yetu, Maombi yana sehemu yetu na utashi wetu na maamzi yetu yanayo sehemu ambayo inachangia...
 
This is called the "Naomi Campbell" complex, by which diva and their wannabes totally leap out of reality and operate under an utopian existence in which they are some Queen Bee, aka Baduism or "The Miseducation of Lauryn Hill".
 
It seems as if kila mchangiaji hapa anaamini kuwa huyu mtoto amefanya hilo alilofanya kwa kuwa tu 'amechanganyikiwa'. Hivi kuna anayejua sababu halisi haswa iliyopelekea yeye kutenda kosa hilo? Kuna mambo yanatokea kwenye maisha ya kila siku ambayo yanaweza kuku push ukajikuta unafanya mambo ambayo hata hukutarajia!
 
Kiboy cha Wema
i31_Wema1.JPG



Source:Michuzi
 
It seems as if kila mchangiaji hapa anaamini kuwa huyu mtoto amefanya hilo alilofanya kwa kuwa tu 'amechanganyikiwa'. Hivi kuna anayejua sababu halisi haswa iliyopelekea yeye kutenda kosa hilo? Kuna mambo yanatokea kwenye maisha ya kila siku ambayo yanaweza kuku push ukajikuta unafanya mambo ambayo hata hukutarajia!
Ni mchanganyiko wa mapenzi na wivu...
 
Mbona kama anajipu shingoni! isijekuwa alikuwa amening'ínizwa huko segerea. Lakini haya maurembo ya kutizama upya. Haiwezekani Lundenga achukue watoto wa watu then waishie kuharibikiwa hivi, ona ule msururu wa bwana mkubwa wote wanaconnection na huyu manju.

Nadhani tuweke kila mshiriki angalau awe na shahada moja na ajira ya kueleweka na apewe guarantee akitoka huko aendelee na ajira yake badala ya kuwaacha wakizurura hovyo. Ukienda Zain Vodacom Tacaid Baclays Bank kunawashiriki wazuri tu ambao wanaweza shiriki huo ulimbwende kwa muda then wakarudi kibaruani kwao.
 
Miss Tanzania wa zamani Wema Sepetu atupwa lupango Dar

wemasepetu.jpg


MISS Tanzania wa mwaka 2006, Wema Sepetu na mwenzake, Asha Jumbe, wakazi wa Tabata Senene jijini Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni wakikabiliwa na tuhuma ya kuharibu mali.

Akisoma hati ya shtaka hilo, Mwendesha Mashtaka Inspekta wa Polisi, Nassoro Sisiwahy mbele ya Hakimu Mfawidhi Emillius Mchauru alisema kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Januari 29 majira ya saa 3:00 usiku maeneo ya Magomeni Mikumi, Dar es Salaam.

Nassoro alidai kuwa siku ya tukio hilo watuhumiwa hao waliharibu kioo cha mbele cha gari aina ya Toyota Rav 4 yenye namba ya usajili T.993 ASD.

Mwendesha mashtaka alidai kuwa kioo cha gari kina thamani ya Sh 1,000,000 mali ya Stephen Kanumba.

Hata hivyo, watuhumiwa hao walikana shtaka hilo na walipelekwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya Sh 500,000, wadhamini wawili, mmoja awe mtumishi wa serikalini.

Awali, mtuhumiwa wa kwanza alikuwa ana mdhamini, lakini cha kushangaza alipofika mahakamani hapo alidai kuwa alikuwa amesahau barua zake kwenye gari.

"Mheshimiwa hakimu naomba nikachukue barua za kumdhamini kwani nimezisahau kwenye gari nilipoitwa mimi nikaja bila kuzichukua, "alisema mdhamini wa mtuhumiwa wa kwanza

Baada ya muda kupita hakimu Mchauru alisema, "Yaani mahakama imsubiri mtu aenda nyumbani kuchukua barua za kumdhamini mtu, kesi hii naiahirisha hadi hapo itakapotajwa tena Machi 18".

Source: Mwananchi

Inasikitisha, lakini kama tuonavyo kwa hawa macelebrity macho, mijicho yapo kwao, nafikiri alitaka kuigiza yale ya marehemu Left Eye. RIP

Pole sana Wema, ni kukomaa kimaisha.
 
Yaani mama yake anamsihi aingie ndani ya gari ili ampeleke home ..ila bado Wema anang'ang'ania yule jamaa??? tena mbele ya wazazI????

Mengine aibu mno!!

Au anakula unga??
 
Ina maana Kanumba alikuwa mpenzi wake harafu akamumwaga ndio ikamtia hasira au ni vipi?
Ni kama hivyo, kwani kesi yenyewe ni ya kuvunja kioo cha gari la Kanumba, Well mwanamke/mwanaume akifikia hatua hiyo kwa mpenzi wake mara nyingi ni kutokana na wivu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom