Wema Sepetu atupwa lupango

GP

JF-Expert Member
Feb 5, 2009
2,049
160
kuna habari kwamba yule miss TZ 2006, Wema Sepetu ameanza kuchanganyikiwa. Wiki iliyopita alimfanyia fujo mpenzi wake wa zamani ambaye ni msanii wa maigizo nchini Steven Kanumba na kuvunja vioo vya gari lake.
inasemekana kwa sasa mrembo huyu anatumia kilevi aina ya Bangi na wazazi wake wameshamshindwa wanamwachia Mungu tu.
 
bado mtoto,anahitaji kukua...its a disgrace kwakweli.
huyu binti naamjua personally,baada ya kuukwaa u-miss,she made a 360 degree
U-turn
 
Amekosa guidance,

Tushimnyooshee kidole...haya mabo huwakumba wengi! Tumwombee Mungu abadilike awe mrembo wa sura na tabia!
 
Mmh isije kuwa kapata ile mail ya Liumba na wanawake aliotembea nao,mana naye yumo kwenye list.kama ni kweli hakuna atakayepona mana hiyo list inatisha jamani
 
Miss Tanzania wa zamani Wema Sepetu atupwa lupango Dar

wemasepetu.jpg

MISS Tanzania wa mwaka 2006, Wema Sepetu na mwenzake, Asha Jumbe, wakazi wa Tabata Senene jijini Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni wakikabiliwa na tuhuma ya kuharibu mali.

Akisoma hati ya shtaka hilo, Mwendesha Mashtaka Inspekta wa Polisi, Nassoro Sisiwahy mbele ya Hakimu Mfawidhi Emillius Mchauru alisema kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Januari 29 majira ya saa 3:00 usiku maeneo ya Magomeni Mikumi, Dar es Salaam.

Nassoro alidai kuwa siku ya tukio hilo watuhumiwa hao waliharibu kioo cha mbele cha gari aina ya Toyota Rav 4 yenye namba ya usajili T.993 ASD.

Mwendesha mashtaka alidai kuwa kioo cha gari kina thamani ya Sh 1,000,000 mali ya Stephen Kanumba.

Hata hivyo, watuhumiwa hao walikana shtaka hilo na walipelekwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya Sh 500,000, wadhamini wawili, mmoja awe mtumishi wa serikalini.

Awali, mtuhumiwa wa kwanza alikuwa ana mdhamini, lakini cha kushangaza alipofika mahakamani hapo alidai kuwa alikuwa amesahau barua zake kwenye gari.

"Mheshimiwa hakimu naomba nikachukue barua za kumdhamini kwani nimezisahau kwenye gari nilipoitwa mimi nikaja bila kuzichukua, "alisema mdhamini wa mtuhumiwa wa kwanza

Baada ya muda kupita hakimu Mchauru alisema, "Yaani mahakama imsubiri mtu aenda nyumbani kuchukua barua za kumdhamini mtu, kesi hii naiahirisha hadi hapo itakapotajwa tena Machi 18".

Source: Mwananchi
 
KABINTI HAKO BADO KASHAMBA DIZAINI!hizo mambo watu hawafanyi siku hizi.ukisema kanakua utakuwa unakapendelea!
 
Na Kuruthum Ahmed

i240_wemabc1.jpg

MISS Tanzania wa mwaka 2006, Wema Sepetu (pichani hapo juu) na mwenzake, Asha Jumbe, wakazi wa Tabata Senene jijini Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni wakikabiliwa na tuhuma ya kuharibu mali.

Akisoma hati ya shtaka hilo, Mwendesha Mashtaka Inspekta wa Polisi, Nassoro Sisiwahy mbele ya Hakimu Mfawidhi Emillius Mchauru alisema kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Januari 29 majira ya saa 3:00 usiku maeneo ya Magomeni Mikumi, Dar es Salaam.

Nassoro alidai kuwa siku ya tukio hilo watuhumiwa hao waliharibu kioo cha mbele cha gari aina ya Toyota Rav 4 yenye namba ya usajili T.993 ASD.

Mwendesha mashtaka alidai kuwa kioo cha gari kina thamani ya Sh 1,000,000 mali ya Stephen Kanumba.

Hata hivyo, watuhumiwa hao walikana shtaka hilo na walipelekwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya Sh 500,000, wadhamini wawili, mmoja awe mtumishi wa serikalini.

Awali, mtuhumiwa wa kwanza alikuwa ana mdhamini, lakini cha kushangaza alipofika mahakamani hapo alidai kuwa alikuwa amesahau barua zake kwenye gari.

"Mheshimiwa hakimu naomba nikachukue barua za kumdhamini kwani nimezisahau kwenye gari nilipoitwa mimi nikaja bila kuzichukua, "alisema mdhamini wa mtuhumiwa wa kwanza.

Baada ya muda kupita hakimu Mchauru alisema, "Yaani mahakama imsubiri mtu aenda nyumbani kuchukua barua za kumdhamini mtu, kesi hii naiahirisha hadi hapo itakapotajwa tena Machi 18".

%5Cwemasepetu.jpg

Miss Tanzania 2006,Wema Sepetu na rafiki yake Asha Jumbe ndani ya basi la Magereza watayari kuanza maisha mapya ya rumande baada ya kukosa dhamana kwa shtaka la kuharibu mali.

Source: Mwananchi Newspaper
 
If we have people who believe in God and Pray in JF - then its time to pray for the lady - God changes people - if we pray for her God will change her -

Naamini Mungu anamuwazia mema - na anaweza kumbadilisha akawa dada mzuri tena - siku moja labda - mtumishi - mhubiri wa Mungu - au mwanamke mwema aliye fahari ya mumewe -

LETS PRAY FOR HER - NOTHING IS IMPOSSIBLE FOR GOD

May God comfort her parents, relatives and friends - najua wanaumia wamwonapo mpenzi wao anapotea - :(
 
...Dah, watu wengine wanahitaji 'reality check' ndiyo warudi kwenye mstari. I hope maisha ya lupango yatamnyoosha angalau kidogo huyu 'spoilt brat.'
 
Preacher, nakubaliana na wewe kwa asilimia mia moja.

Mungu ni mwema atamuokoa na kumuondoa katika mahangaiko yote ya dunia.tumuombee ili aweze kuijua kweli. Amen
 
mie nakapenda kweli haka kabinti jamani but kweli kamebadilika sana cku hizi vitabia vya ovyo ovyo...kweli badokana ka ushamba fulani.
 
Criteria za kuchagua ms tz huwa ni nini? they obviously need to be reviewed
 
Hawa ''mstaa'' wetu wa bongo vipi? au hata hizi kashkash wanaziiga kwa wenzetu wa Magharibi ambao kwa wenzetu mazingira yao wakati mwingine yanawalazimu kuwa hivyo? What is the root cause of all these here?
 
mie nakapenda kweli haka kabinti jamani but kweli kamebadilika sana cku hizi vitabia vya ovyo ovyo...kweli badokana ka ushamba fulani.

Kamezidi kuwa na skendo kibao, mwanzoni nilidhani barehe lakini sasahivi kakubwa tu kanapaswa acha upuuzi huu mara moja!
 
If we have people who believe in God and Pray in JF - then its time to pray for the lady - God changes people - if we pray for her God will change her -

Naamini Mungu anamuwazia mema - na anaweza kumbadilisha akawa dada mzuri tena - siku moja labda - mtumishi - mhubiri wa Mungu - au mwanamke mwema aliye fahari ya mumewe -

LETS PRAY FOR HER - NOTHING IS IMPOSSIBLE FOR GOD

May God comfort her parents, relatives and friends - najua wanaumia wamwonapo mpenzi wao anapotea - :(

Sawa lakini mimi sitafanya hivyo kwa ajili ya huyu. Nadhani wana JF waumini m-pray that mafisadi wote warudishe hela zote and not praying for this foolish kid!
 
Sawa lakini mimi sitafanya hivyo kwa ajili ya huyu. Nadhani wana JF waumini m-pray that mafisadi wote warudishe hela zote and not praying for this foolish kid!

Mi nakupa zote mkuu, we ndo umenena
hivi vitoto vinatupotezea muda na appetite ya kudili na mafisadi, au wametumwa na mafisadi ili watupotezee concetration?

Mungu vilaani vizazi hivi
 
The truth huyu binti ana umbo la kuvutia but she is empty upstairs na utoto ndio bado unamsumbua. Si mtu wa kulaumiwa bali wa kuhurumiwa, kuombewa na kusaidiwa. Tatizo lake kubwa ni delayed hormone growth inayofanya ni mwili tuu umekuwa na kupevuka lakini akili bado iko pale pale kwenye utoto, uthibitisho ni sauti yake bado ni baby voice.
Ukweli ni kuwa hajalala lupango, bali ofisa wa zamu atakuwa 'amemsaidia' angalau kulala mahali pazuri hata kama ingebidi kutumia ule msemo 'ukijua kupokea....'
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom