Wema Sepetu adai kuwa mama yake amemtia aibu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wema Sepetu adai kuwa mama yake amemtia aibu!

Discussion in 'Celebrities Forum' started by ngoshwe, Jul 1, 2012.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Jul 1, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145


  [​IMG]
  Wema Isaac Sepetu na mama yake, Mariam Sepetu hawapo vizuri tangu yale mahojiano aliyoyafanya mzazi wake huyo runingani wiki mbili zilizopita akiwachana marafiki wa staa huyo mkubwa wa picha za Kibongo


  Akizungumza na mtandao wa Global publisher katika mahojiano maalum juzi Alhamisi , Wema alisema kuwa hawezi kusahau siku mama yake alipofanya ‘intavyu' kwani aliposikia anaaza kutiririka ilibidi aipigie magoti runinga akiiomba inyamaze akidhani inamsikia.

  "Kwanza sikuwepo wakati mama anafanya intavyu ‘so' sikutarajia kama angezungumza vitu vya namna ile.
  "Ni kweli mama yangu kama mzazi alikuwa na kila sababu ya kunizungumzia, alikuwa na uchungu na mwanaye sawa! Lakini ‘mai mom' alipitiliza."  "Nadhani kuna vitu vilitakiwa kuondolewa kwa sababu mara baada ya kuzungumza, hali ilikuwa mbaya sana kuanzia kwenye mitandao ya kijamii na hata dada yangu alinipigia simu nikamweleza nilivyojisikia vibaya."


  KANITIA AIBU!
  "Nilijua mama kanitia aibu lakini nikajikaza kwa sababu utakumbuka ndo' kwanza nilikuwa kwenye maandalizi ya uzinduzi wa filamu yangu ya Super Star.


  "Nilikaa kimya, nilijifanya kama hakuna kitu chochote kilichotokea lakini si unajua lazima moyo utakuuma tu hata kama ukijifanya kusahau.


  "Baada ya kuona nipo kimya, siku iliyofuata alinitumia meseji mbaya na ninazo lakini hadi leo sikumjibu."  TUNAWEZA KUSEMA ALIKUDHALILISHA?
  "Yaah…ukweli hali haikuwa nzuri. Meneja wangu Martin (Kadinda) alimpigia mama na kumsisitiza mwaliko niliokuwa nimempa wa kuhudhuria kwenye uzinduzi wa filamu yangu lakini amini usiamini mama yangu hakuhudhuria. Kwa upande wa baba naye hakufika lakini alinipa sababu za msingi kabisa nikamwelewa na pia alikuwa akifuatilia kila kitu kwa kuchati na dada yangu kwani alijua niko bize."  VIPI KUPELEKWA KWA WAGANGA?
  "Sijui mama alipata wapi hiyo kitu ‘coz' sijawahi na wala sijui mambo ya waganga kama alivyozungumza yeye."  NISAMEHENI SANA
  "Kwa yeyote aliyeguswa na mama kwa namna yoyote, naomba anisamehe sana."

  http://freebongo.blogspot.com/2012/07/wema-sepetu-adai-kuwa-mama-yake-amemtia.html#_   
 2. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2012
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  haya mapya tena, mama na mwana hawaishiw drama, huyo wema angemchukuwa na mama yake kwenye izo filamu zake aigize naye maana naona anaweza sana.
   
 3. Raiamwematz

  Raiamwematz Senior Member

  #3
  Jul 1, 2012
  Joined: May 9, 2012
  Messages: 104
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Je mama ake alimwambia nini zaidi?? hebu aliye na news atukumbushe, maana mimi hili sakata lilinipita, nilikuwa pori!!!
   
 4. k

  kisukari JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2012
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,760
  Likes Received: 1,050
  Trophy Points: 280
  wangemalizana wenyewe private,kwa vyovyote vile,yule ni mama yake.sio kila kitu mpitie kwenye media
   
 5. BantuGirl

  BantuGirl Senior Member

  #5
  Jul 1, 2012
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 157
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wema unamshushia mama yako heshima, usingepeleka kwa waandishi wa habari....
   
 6. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #6
  Jul 1, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Wema muulize Kanumba yuko wapi sasa, keshaomba ubalozi wa nyumba kumi huko aliko naye alianza sokombingo kama hizi na mzazi wake.
   
 7. salito

  salito JF-Expert Member

  #7
  Jul 1, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,365
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  yaan sina computer tu ningekugonga like...
   
 8. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #8
  Jul 1, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  So sad kwa Wema, alitakiwa amalizane na mamaye nyumbani si hadharani, angekubali yote tu jamii imuelewe hivi, lakini si kumsema mamaye, though huyu mama alikera sana.
   
 9. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #9
  Jul 1, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Akimaliza hii drama, mama arudi aseme kuwa amesikitika kuwa mwanae kamkana. Yaani wasiiachie media ipumue, wera wera!
   
 10. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #10
  Jul 1, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  bibi yake wema sijui yuko wapi,kuja kusema mama wema kamdhalilisha hakumfunda kutumia ushirikina kwa mjukuu wake..lol
   
 11. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #11
  Jul 1, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Upuuzi mtupu.
   
 12. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #12
  Jul 1, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  sasa kama 'katengenezwa' mama yake asiseme????
   
 13. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #13
  Jul 2, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280

  Nashanga!
   
 14. J

  John W. Mlacha Verified User

  #14
  Jul 2, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  mama alisema nini?
   
 15. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #15
  Jul 2, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Mama alisema amemtengeneza Wema, akimaanisha kuwa Wema kashazurulishwa sana kwa waganga so ana Kinga...

  Mama shirikina toto nalo shirikina yaani full ushuzi.
   
 16. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #16
  Jul 2, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Nashauri Mama kwenye movie awe Mganga....
  Ili atuonyeshe jinsi ya kumtengeneza...
   
 17. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #17
  Jul 2, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280

  Ndege wafananao huruka pamoja...
  Mama Gagulo...
  Mtoto Sidiria...
  Zote nguo za ndani
   
 18. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #18
  Jul 2, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Hajamsema wala kumchamba...
  Kamuanika tu mchana kweupeee...shuuuh
   
 19. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #19
  Jul 2, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280

  Hah hah haaaah sasa tumsubiri yule mshambenga ambaye yuko radhi kufa akimtetea Mwana wema.
   
 20. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #20
  Jul 2, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,539
  Likes Received: 10,461
  Trophy Points: 280
  Tatizo mama wema anatafuta umaarufu uzeeni.!
   
Loading...