Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,597
- 215,268
Kabla ya Uhuru wakati Tanganyika ikiwa katika uangalizi wa Uingereza, kuna binti wa Kiingereza alikuja Tanganyika baada ya kumaliza mafunzo yake ya udaktari huko kwao.
Daktari Mkuu katika Hospitali ya kanisa alikopangiwa alikuwa raia wa Australia na yeye akawa Msaidizi wake. Siku moja akiwa kazini alimpokea mke wa mwalimu wa kijijini pale akiwa mjamzito. Mama yule alikumbwa na mauti wakati wa kujifungia lakini aliacha mtoto wa kiume
Habari za kifo cha mke wake zilimuumiza sana mMwalimu. Daktari Muingereza alimshauri amuachie mtoto yeye ashughulikie mazishi ya mke wake. Daktari alimuacha mtoto hospitali akiangaliwa na manesi. Baada ya mazishi Daktari alishajenga muungano na mtoto yule. Alimuomba mwalimu amlee mtoto yule aliyefiwa na mama.
Baada ya Uhuru, daktari alirudi kwao Uingereza. Alimuacha mtoto akiwa na miaka saba. Alimtafutia shule ya boda nzuri na kumpeleka. Alilipa ada ya mwaka na mahitaji mengine. Alipofika kwao, baada ya kupata ajira aliendelea kumtunza yule mtoto
Daktari alipoolewa na kupata watoto, aliwafahamisha watoto wake kuwa wana kaka mkubwa Tanzania. Watoto waliandikiana barua. Yule mtoto alifika mbali kielimu na kuwa mmoja wa viongozi wanaoaminika serikalini. Aliamua kulea watoto yatima kwani anafahamu kama asingepata msaada wa malezi asingefika hapo alipo.
Ndugu wanatembeleana na watoto wao wanajiona ni ndugu. Daktari alitengeneza keki isiyooza.