Wema na huruma zangu zimeniponza, sasa najuta!

Mimi nilimkopesha dada mmoja 150k, imepita miezi hajarudisha. Sasa hivi kaniblock simu zangu zote. Binadamu si wema kabisa. Kudaiwa sio dhambi kwa nini usipokee simu kiungwana tu.
"... kudaiwa sio dhambi, kwa nini usipokee simu kiungwana tu"

Hilo ndilo la kuuliza, na kaku block kwa sababu ulikuwa unamsumbua sana au? Ni baada ya muda gani mlikubaliana atarudisha?

Pia ulijuaje kama ameku block?
 
Pole kwa changamoto, umeshawahi kusikia 'nguvu ya akili?', kinachokutesa sio 900K, kinachokutesa ni akili yako inayokuambia kwamba 'huenda umetapeliwa', na kwamba 'hakuna fedha zingine zaidi ya hizi 900K', na akili yako inatumia muda mwingi kujikita kuwazia 900K yako, wakati akili yako inapaswa iwazie mikakati mingine ya kutafuta hela (zaidi) na kusahau hiyo 'iliyopotea' . Iambie akili yako kwamba, bahati mbaya hii hela imepotea', chukulia kama umetumia na imekwisha, kwani kupoteza 900K ndio mwisho wa dunia?! ' Msamehe na move on na maisha yako, utashangaa 900K itarudi (sio kutoka kwa uliyemkopesha) bali itarudi kwa mtindo mwingine, tena zaidi.

Ushauri wa bure
Siku nyingine mtu akiomba umkopeshe fedha, kama huna hakika kama atarudisha USIMPE, toa sababu zozote zile uzijuazo lakini usimpe, na hata ukiamua kumpa basi mpe kiwango ambacho hata asiporudisha haitakuathiri
Ahsante, nimebarikiwa na huu ushauri wako sana
 
Hakuna kitu kibaya kukopesha mtu kwa kumpa mpaka akiba yako, iliwahi nitokea aisee nilijuta.
Sasa anakuambia hivi, "najua hii ndiyo akiba yako ila nitarudisha tu, nafahamu ndiyo hela ya mwisho ila nikopeshe tu".

Huwa ving'ang'anizi sana, na hata wakipata hela huona tena hasara kulipa deni. Kifupi watu wa namna hii hawana huruma, wabinafsi na wana tamaa.

Dawa ni kuwa na macho makavu na katili
 
Mkuu, ukitaka upoteze ndugu na marafiki basi uwe na tabaia ya kukopesha, vizuri unapo msaidia mtu fedha fanya kama umempa na usihesabie kama unafedha yako...Kukopa bora akakope kwenye Taasisi zinazotoa mikopo...Huwa inauma sana hasa unapo tarajia utalipwa halafu mtu halipi, mbaya zaidi wengine hawawezi kudaidai hasa Kwa mtu ámbae mnaheshimiana
Ni kweli. Ila ukiwa na utu hutosahau deni, mbaya zaidi kuanzia 500k TZS. Mbona wanapopata shida hawasahau shida zao?

Nafikiri hufanya makusudi tu.
 
Binafsi sikopeshi mtu yoyote hapa duniani. Labda nimsaidie tena kiwango nitakachoamua mimi.

Dunia ina mabilioni ya watu uwaache wote unifuate mimi? Nakujibu tu sina. Na kama una shida na ni rafiki yangu nakupiga tafu ila sio kukopesha. Yanayokopesha ni mabenki na taasisi nyingine za mikopo na kuna vigezo , masharti, riba na mikataba.
Ni sahihi, aisee wengi tunafanya vitu hivi kienyeji sana.
 
Pole sana mkuu.
Siku zote usikopeshe pesa yako ya akiba/malengo.
Hivyo kama ilikua ni akiba hukupaswa kumkopesha.

Pia uwe unatoa 25% tu ya kile kiasi mtu anachokuomba usipende kutoa kiasi chote mtu anachomba kukukopa. Kwa mfano huyo jamaa yako uliyempa 900K ulipaswa umpe 225K tu.
 
Alikuwa anang'ang'ania mno, pamoja na kujua kuwa sikuwa na hela nyingine.
 
Tenda wema uende zako.. ulichokosea mkuu umetenda wema alaf umekaa hapo hapo.. pole sana
Ni sawa kwa kiasi fulani, ila hii ilikuwa ni kama business, kukopesha sidhani kama ni kutenda wema.
 
"... kudaiwa sio dhambi, kwa nini usipokee simu kiungwana tu"

Hilo ndilo la kuuliza, na kaku block kwa sababu ulikuwa unamsumbua sana au? Ni baada ya muda gani mlikubaliana atarudisha?

Pia ulijuaje kama ameku block?
Wala sijamsumbua. Nimejua baada ya kuwa simu zangu haziendi lakini nikipiga kwa simu nyingine inaita. Hata messege za whatup haziendi pia lakini kwa simu nyingine inaonyesha anazisoma. Mwenyewe aliniambia baada ya wiki 2 atarejesha. Toka January hadi leo. Nilimuandikia messege kwa simu nyingine nikamuambia, shida huwa haziishi, na kwenye hii dunia huwezi jua nani atakusaidia. Ishi kwa uaminimu na hata siku moja jaribu usiwe chanzo cha makasiriko ya watu. Sitakuja kukudai hiyo hela, kama unaona ni haki yangu utanilipa kama unaona sio stahiki yangu powa. All the best
 
Pole sana kiongozi lakini nina imani anakukusanyia pesa yako..
Miezi imepita na simu hajibu? Hata kama hajapata ila si ku mute. Hiyo ni dalili ya kutokuwa muungwana na sio ustaarabu. Ni jeuri na kibri.
 
Wala sijamsumbua. Nimejua baada ya kuwa simu zangu haziendi lakini nikipiga kwa simu nyingine inaita. Hata messege za whatup haziendi pia lakini kwa simu nyingine inaonyesha anazisoma. Mwenyewe aliniambia baada ya wiki 2 atarejesha. Toka January hadi leo. Nilimuandikia messege kwa simu nyingine nikamuambia, shida huwa haziishi, na kwenye hii dunia huwezi jua nani atakusaidia. Ishi kwa uaminimu na hata siku moja jaribu usiwe chanzo cha makasiriko ya watu. Sitakuja kukudai hiyo hela, kama unaona ni haki yangu utanilipa kama unaona sio stahiki yangu powa. All the best
Na hajakujibu wala kukutafuta tangu ulipotuma hiyo msg yenye kuumiza moyo? Duh!
 
Wala sijamsumbua. Nimejua baada ya kuwa simu zangu haziendi lakini nikipiga kwa simu nyingine inaita. Hata messege za whatup haziendi pia lakini kwa simu nyingine inaonyesha anazisoma. Mwenyewe aliniambia baada ya wiki 2 atarejesha. Toka January hadi leo. Nilimuandikia messege kwa simu nyingine nikamuambia, shida huwa haziishi, na kwenye hii dunia huwezi jua nani atakusaidia. Ishi kwa uaminimu na hata siku moja jaribu usiwe chanzo cha makasiriko ya watu. Sitakuja kukudai hiyo hela, kama unaona ni haki yangu utanilipa kama unaona sio stahiki yangu powa. All the best
Binafsi naamini silaha kuu ya kwanza ya kuyapiga maisha ni UAMINIFU. Aisee bora ushinde njaa ila linda sana UAMINIFU wako.
 
Back
Top Bottom