Wema hawajalizaliwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wema hawajalizaliwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mutekanga, Aug 25, 2009.

 1. M

  Mutekanga Member

  #1
  Aug 25, 2009
  Joined: Aug 26, 2007
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tuliwacheka wahenga kwa kuwauza ndugu zetu utumwani. Mpaka sasa tunajiuliza kama kweli walikuwa na akili timamu. Sisi tumekwenda zaidi! Vizazi vijavyo, vitatushangaa sana, si kama vile tunavyowashangaa wahenga, hapana - sisi hata mifupa yetu itafukuliwa na kuchomwa moto.

  Ujinga huu wa kukitanguliza chama badala ya Taifa, kutanguliza tumbo badala ya taifa, kuuza rasilimali zote, kutoa fedha ndani ya nchi na kuzichimbia ulaya, kununua shahada za wapiga kura, kupindisha ukweli, ukabila na udini, ni mambo ambayo yataonekana kinyaa na kichekesho mbele ya vizazi vijavyo.

  Ni kweli wema hawajazaliwa. Viongozi wetu wanataka kuendelea kutawala, hata wale walioondolewa kwa kashfa kubwa ,bado wanataka kusafishwa ili wawe Zuma wa Tanzania. Ni mambo ya kusikitisha kabisa. Wanayaangalia matumbo yao, badala ya kuliangalia taifa letu. Tukianza kupigana, wao na familia zao watakimbilia walikoficha vijisenti vyao.

  Tafakari.
   
 2. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #2
  Aug 25, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  Mkuu Mutekanga,

  I can see your reflection! Wema washazaliwa, we cannot recycle the same guys, ni wakati wetu kuamka... Wakati wa kuandika na kutekeleza, wakati wa kutekeleza yaliyoandikwa na tuliyopania kufanya... Maamuzi sahihi yanawezekana 2005-2015... Ni miaka 10 ya kufanya mabadiliko makubwa, mabadiliko ambayo hawatapenda yatokee lakini haina budi kutokea!

  Daima mimi niliwazia muongo huu mmoja, kuwa muongo wa mapambano ya kifikra na kuelekea mapambano halisi ya kulipeleka taifa letu palipo pazuri zaidi ya tulipokuwa kabla.
   
 3. Mganga wa Jadi

  Mganga wa Jadi JF-Expert Member

  #3
  Aug 25, 2009
  Joined: Mar 12, 2008
  Messages: 278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Wema ni wengi mno wamefunikwa na wingu nene la ufisadi uliojengwa ndani ya udini, ukabila , uchama. Inahitajika vita nyingine ya kujitolea mhanga kwa ajili ya ukombozi wa nchi yetuinayoliwa na wachache wanaojiona wajanja.

  Mwema ni mimi na wewe na tupo hai ni lazima tu-act sasa la sivyo historia itatuhukumu.
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Aug 25, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Ukiangalia haraka haraka wema ni wengi kuliko hao wabaya na ukiangalia wabaya wenyewe ambao wametushika maskio yetu hata 50 hawazidi lakini tumekubali wenyewe kuuza uhuru wetu ambao baba na babu zetu waliupigania kwa mkoloni leo hii tumegeukwa na wale ambao tuliwaamini kuwa watatuongoza na kutupeleka pale tunapo taka na kujipatia maendeleo.
   
Loading...