Weledi wa "Spin doctors" wa CCM!

Allen Kilewella

Verified Member
Sep 30, 2011
13,459
2,000
Katika eneo ambalo CCM iko vizuri sana ni kwenye eneo la Propaganda.Ingawa hakuna jambo la maana ambalo CCM wanafanya kwa nchi yetu, lakini ni mafundi wa kutengeneza propaganda kuonesha kwamba chama chao kinatekeleza kila wanachoahidi na kuonesha kwamba vyote vinavyoshindikana ni kwa sababu vyama vingine vinazuia vitu hivyo kufanyika.

Kila wakati ni lazima lizushwe jambo nje ya mkondo Mkuu kuwatoa watu kwenye jambo la msingi la kitaifa. Bahati mbaya kabisa kwa sasa vyama vya upinzani kwenye eneo hilo wamekuwa ni dhaifu sana na kuachia shughuli hiyo ifanywe na wanaowaunga mkono mtandaoni.
 

Rich Pol

JF-Expert Member
Oct 11, 2013
7,832
2,000
CCM kitaendelea kutawala miaka yote mpaka kitakapotokea chama cha siasa chenye upinzani wa dhati kuongoza nchi, na siyo wapiga deal wakiongea hili leo kesho wameshalisahau
 

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
30,777
2,000
Kwa anayefahamu muundo na shughuli za CCM ni wazi ataelewa kuwa utekelezaji wa Ilani ni kipaumbele cha kwanza kabisa...mengine yanafuatia.

Tatizo la Upinzani ni kutokuwa serious na kukosa jambo jipya kwa wananchi ambalo halijawahi kuahidiwa na CCM.

Upinzani unatuhadaa kwamba utayabadilisha mambo ingawa Hawana na hawajaonesha njia mpya yoyote na badala yake wanakasirika kuona CCM inatatua yale yalikuwa yanawapa cha kusema.

Kwa sasa upinzani unaathiriwa na hasira za kuona kile walichotamba nacho kwenye majukwaa kimepokwa na CCM.

Mbaya zaidi tamaa ya upinzani kuingia madarakani kwa njia zote zisizo halali imeonekana wazi wazi....Yaani upinzani ulikuwa radhi kuitoa kafara au kuachana na vita ya ufisadi ili tu impate fisadi wanayeamini angewaingiza madarakani...na hili ndio limekuwa tope lao kuu...na hawana msaada....

Bado upinzani wa kweli ambao ulitabiriwa na baba wa Taifa haujatokea.
 

Allen Kilewella

Verified Member
Sep 30, 2011
13,459
2,000
CCM kitaendelea kutawala miaka yote mpaka kitakapotokea chama cha siasa chenye upinzani wa dhati kuongoza nchi, na siyo wapiga deal wakiongea hili leo kesho wameshalisahau
Umesahau mwenyekiti wako alisema hatachagua wapinzani kwenye serikali anayoiongoza na leo hii anafanya nini? Umesahau wabunge wa CCM walivyokuwa wanazitetea sheria mbovu za madini lakini leo hii wanalalamika kwamba tunaibiwa na wawekezaji?
 

nkongu ndasu

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
22,567
2,000
nchi yetu itaendelea kuwa masikini mpaka kiama kwa staili ya viongozi tunaowachagua hasa kutoka ccm.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom