Welcome William John Malecela!

Status
Not open for further replies.

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
Naona kuna memba mpya mwenye majina ya W. J. Malecela. Natabiri atakuwa William John Malecela, kama ni yeye napenda kumkaribisha jamvini.

Tunatarajia mengi toka kwako mkuu
 
Kwa heshima na taadhima pamoja na unyenyekevu mkubwa, ninaomba kujiunga na forum hii na wananchi wote ndani ya huu uwanja. Mimi ni Mtanzania mwenzenu na ni mwananchi mzalendo pia, ninaomba kuja hapa tushirikiane kuliendeleza taifa letu kwa kutoa maoni na michango kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu changa.

- Jina langu ninaitwa William J. Malecela, anwani yangu pepe ni malecela(at)msn.com na namba yangu ya simu nyumbani ni 1-914-664-1518, na pia namba yangu ya mkononi ni 1-914-473-1033, ninamkaribisha mwananchi yoyote kuwasiliana na mimi wakati wowote ule.

Kwa hayo machache, naomba nimalize kwa kusema haba na haba hujaza kibaba, maendeleo ya taifa huletwa na mawazo ya kimaendeleo ya wananchi wa taifa lile bila ya kujali ukubwa au udogo wao kitaifa na huanzia popote pale hata hapa kwenye hii forums.

Ahsanteni sana ndugu zangu.

Wenu

William J. Malecela.
 
Last edited by a moderator:
karibu sana Jamvini hapa na naamini unayo mengi ya kutushirikisha na kujifunza kutoka hapa jamvini.

Karibu Malecela Junior
 
Ndugu malechela na wengine --- unapotoa namba ya simu na email yako hadharani kama hivi ulivyofanya wewe ndugu malechela chochote kikitokea kutokana na wewe kutoa mawasiliano yako hadharani jf haitohusika mawasiliano hayo --- members tuwe makini sana na contacts zetu kwa faida zetu na jukwaa zima na jf

usiku mwem a
 
Karibu sana jamvini. Ujio wako naomba usipelekee kumpoteza yule mwana JF
Maarufu kwa jina la 'efuemiesi'.

Yule keshatuaga na kwamba sasa anaiendea hatua nyingine. Yaweza kuwa ndio mwanzo, si unajua tena?
Karibu Malecela
 
.

Kwa hayo machache, naomba nimalize kwa kusema haba na haba hujaza kibaba, maendeleo ya taifa huletwa na mawazo ya kimaendeleo ya wananchi wa taifa lile bila ya kujali ukubwa au udogo wao kitaifa na huanzia popote pale hata hapa kwenye hii forums.

Ahsanteni sana ndugu zangu.

Wenu

William J. Malecela.

Ukiondoa jazba, haba na haba ndio itajaza kibaba!
 
Jazba nafikiri keshaziondoa wakuu.....na ile ya kutaja taja majina na kujifanya kujua member itakwisha......otherwise tupo pamoja 2010.....msituletee tshit za jinja nataka tetron bana....
 
Kwa heshima na taadhima pamoja na unyenyekevu mkubwa, ninaomba kujiunga na forum hii na wananchi wote ndani ya huu uwanja. Mimi ni Mtanzania mwenzenu na ni mwananchi mzalendo pia, ninaomba kuja hapa tushirikiane kuliendeleza taifa letu kwa kutoa maoni na michango kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu changa.

- Jina langu ninaitwa William J. Malecela, anwani yangu pepe ni malecela@msn.com na namba yangu ya simu nyumbani ni 1-914-664-1518, na pia namba yangu ya mkononi ni 1-914-473-1033, ninamkaribisha mwananchi yoyote kuwasiliana na mimi wakati wowote ule.

Kwa hayo machache, naomba nimalize kwa kusema haba na haba hujaza kibaba, maendeleo ya taifa huletwa na mawazo ya kimaendeleo ya wananchi wa taifa lile bila ya kujali ukubwa au udogo wao kitaifa na huanzia popote pale hata hapa kwenye hii forums.

Ahsanteni sana ndugu zangu.

Wenu

William J. Malecela.

Vipi wewe ni mmoja miongoni mwa Royal famili ya Mzee J Malecela ( CCM )? umarufu mzee tinga tinga
 
Bwana Malecela,

Uliyoyasema yote kimsingi ndiyo msingi wa JamiiForums.Tunaamini katika uwazi. Sielewi kwa nini unatoa personal information. Kama mwanachama mpya, hujatueleza kwa nini sisi wanachama wa siku nyingi tukutafute wewe. Kwa nini wewe unataka majadiliano zaidi katika personal contacts? Kuna ajenda gani ambayo haiwezi kuongelewa hapa kwenye forums hata ihitaji personal contacts?

Je kuna kitu maalum unataka kujadili? Au kuna mpango unatayarisha? Ingekuwa vizuri ukatupa sababu ya kueleweka inayosababisha utake personal contact.

Forums zetu zinatoa umuhimu mkubwa kwa anonimity, na kutokana na majadiliano yanavyokwenda watu wana haki ya kuwa concerned kuhusu usalama wao.Kwa nini watu wasiamini kwamba wewe ni agent wa CCM unayetaka kuchukua namba za simu na majina ya watu?
 
anatoa simu za marekani wakati mwenyewe yuko bongo,bwaa ha ha ha haaa
 
yhst-20539724291135_2046_0

- Hapa nipo pamoja na Mwenyekiti wa CCM na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa J. K. Kikwete.
 
Bwana Malecela,

Uliyoyasema yote kimsingi ndiyo msingi wa JamiiForums.Tunaamini katika uwazi. Sielewi kwa nini unatoa personal information. Kama mwanachama mpya, hujatueleza kwa nini sisi wanachama wa siku nyingi tukutafute wewe. Kwa nini wewe unataka majadiliano zaidi katika personal contacts? Kuna ajenda gani ambayo haiwezi kuongelewa hapa kwenye forums hata ihitaji personal contacts?

Je kuna kitu maalum unataka kujadili? Au kuna mpango unatayarisha? Ingekuwa vizuri ukatupa sababu ya kueleweka inayosababisha utake personal contact.

Forums zetu zinatoa umuhimu mkubwa kwa anonimity, na kutokana na majadiliano yanavyokwenda watu wana haki ya kuwa concerned kuhusu usalama wao.Kwa nini watu wasiamini kwamba wewe ni agent wa CCM unayetaka kuchukua namba za simu na majina ya watu?

Mkuu Kiranga
Heshima mbele, hapa JF tunaamini watu kuwa na mawazo huru ili mradi hawavunji taratibu zilizowekwa hapa jamvini. Wapo wanachama kadhaa ambao wanatumia majina yao halisi na wala sina haja ya kuwataja. tafadhali tujifunze kuheshimu utashi na hiyari za wanachama wenzetu.

Itavutia zaidi huko mbele ya safari kama kila mmoja wetu atakuwa muwazi kama alivyo mwanachama mpya William J. Malecela na wale wengine ambao wanatumia majina yao halisi kwani wanaonesha kuwa wao si waoga. ninamsifu William kwa kwenda mbali zaidi kwa kuweka na kontakti zake zote na picha juu kuondoa shaka zaidi kwamba yupo tayari sasa kufikiwa na mtu yeyote. Ikiwa unaona unahitaji kujificha tafuta kadi umpigie au nenda Penny Talk or CallTanzania.com.

Hongera na karibu mwanachama mpya Bw. William J Malecela.
 
Pundamilia,

Sijakataa uwazi (nimeusisitiza, rejea bandiko langu hapo juu) wala kutoheshimu matakwa ya mwanachama.

Nilitaka kujua zaidi ni kipi kinachosukumia personal contact ambacho forum hii haiwezi kukifanya? Nikatoa dukuduku kuhusu usalama.

Maswala yangu hayajajibiwa na wewe wala bwana Malecela mwenyewe.Maswali haya hayana lengo la kumvunjia mtu heshima, ila kama mtu ana heshima zake anaweza kuyajibu na kuhakikishia watu kwamba anazo heshima zake.Ni moja ya mambo tunayojivunia hapa JF, kwamba hakipiti kitu bila kuchambuliwa kwa kina.

Ningefurahi kama ningepata majibu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom