Welcome Aboard to JF Flight

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,810
Ndugu zangu napenda kujitambulisha. Naitwa Muberwa ninaishi Dar es Salaam. Nimefurahi sana kujiunga nanyi katika mtandao huu. Nawatakia majadiliano mema na siku njema.

salamu nyingi ziwafikie popote mlipo

Hi! JamiiForums

My name is John Kitabi, i'm mechanical engineer by professional, i wanted to say hallow to all members of JF and lets exchange ideas for better future

Habari wana jamiiforums?

Naitwa Allen Shembilu na nipo Dar, na ninafurahi kujiunga nanyi kwenye jamii forum hii.

Naamini mmenipokea na naahidi ushirikiano ndugu wana jamiiforums.


Natumaini nyote ni wazima na mnaendelea vema na kazi za ujenzi wa Tanzania. Mimi naitwa S. H. Mnozya, nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu contributions, ideas, analysis and comments za JF. Kimsingi zimekuwa zikinipa changamoto na ninawapongeza kwa kazi nzuri.

Hata hivyo nia na lengo ni kujenga, ili kujenga hatuna budi kujitazama visogoni na kama mmoja wetu hajachana nywele vizuri basi tusisite kumwambie achane. Naamini kuwa ili JF izidi kujijengea heshma na kuthibitisha pasina shaka kuwa ni jamii ya watu mahiri katika kufikiri hatuna budi kuongeza ufanisi katika uchambuzi wa kisayansi.

Nahitimisha kwa kurudia kuwapongeza wanajamii forum wote kwa kazi nzuri.

Nabisha hodi na nawapa heshima zenu Mabibi na Mabwana wa jamii forum. Napenda kujitambulisha kwenu kama MADENGE. Natumai tutazidi kuwa wote humu mtandaoni. ASANTENI

Hodi wanaJF naomba ukaribisho.

Ndugu zanguni wajuvi, wadadisi na wengineo,

Mie ndugu yenu Kiranga cha Ngeda wa viunga vya bandari iso salama, Kiranga wa upande wa Mbwamaji, Kiranga wa Mkuranga,kakae Muamini na mwana wa Fundi Shomvi na Sikudhani binti Muhamedi.

Mara nilivyotoka pande za Msanga Kisiju nikaambiwa ukishangaa maajabu ya Rufiji gari kupita juu ya mto hutafika Utete wala Mpwapwa, zaidi ya hapo maendeleo siku hizi yako huku bandari iso salama kwenye majumba yaliyopandiana, nikachungulia nikaona kweli mnafaudu, hata Mbagala na Charambe tu harufu wanaisikia, na mimi nikaona niombe kugonga hodi hodi mnikaribishe mlionitangulia.Nisambe nimenyimwa maji wakati kisima chatitiri.

Salamu sana kutoka Msanga Kisiju, Kilwa Pande, Kilwa Kivinje, Kilwa Kisiwani, Songo Songo, Somanga, Muhoro mpaka pande za Sala Sala na Mkuranga.Ningewatumia pepeta na mabumunda ya motomoto lakini nimeambiwa humu naweza kutuma picha tu, na mie kamera sina, labda siku nyingine wakija wapima viwanja na midarubini yao ile nitawaomba wanipige picha niiweke muone ninavyofukuzana na ngedere na kima. Sasa niage nikimbilie kuangalia hesabu za minazi maana wakwezi na komba hawakawii kumuadhiri mwenzenu huku. Baada ya hapo mkiniona kimya mjue safari ya Mafia imewadia.

Natanguliza ungo wa shukurani

Kwa leo ni hayo tu,

Wasalaam,

Kiranga cha Ngeda Sangala Kandumbwa



"Welcome aboard to JF Flight... Kijiwe cha Umbea, Fitna, Majungu, Udini, Ufisadi... na kila aina Ya Uzandiki... kuelekea kwenye kila aina ya selfishness.

To participant..., insert any rubish from your brain... Na kuwa tayari kuutetea for any cost... JF... works just like any other Vijiwe vya mitaani...... Kila mtu anajuwa too much... and many member watakuunga mkono na wapo watakuzodoa... if you don't know how to do that... just read as many thread as you can... specially DINI na SIASA na bila kusahau Celebrities Forum... Habari/Hoja mchanganyiko... n.k.

In the event of a sudden attacked by any memberz. Stop screaming to Moderatorz, just swearing a lot... and grab the keyboard, and pull it over your face. If you have a wife and she asked for your help or assistance... Finish marumbano before... assisting her... otherwise she may become your keyboard...! Just write as many utumbo... as you can... you can even use Hoja za nguvu... na ushahidi wa kupandikiza...!

If you are at work... and your boss asked you about kiporo cha kazi ulichokiwacha tangia weekend ya juzi... you have to decide... which one you love more... Job or Jambo... ooops... Jamii... I mean JF...!

After few weeks zijazo utabiri unaonyesha kuwa.... mtakuwa amongs of addicted with JF kama jamaa zangu fulani na fulani hapa...

JF Hakuna Kushindwa ni Kijiwe a.k.a kibanda cha grit sinkerz

Welcome Aboard"
 
Back
Top Bottom