Wekeza pesa kidogo kidogo upate gari ya ndoto yako

Habari ya Majukumu wana jukwaa?

Baada ya kupokea maoni kutoka kwa wadau wetu na wateja wetu mbali mbali, hatimae tumeamua kukubaliana na ombi la kuwekeza pesa kidogo kidogo kwa kati ya miezi 3- miezi 24 kwa anayehitaji kumiliki gari lakini hana pesa ya kulipia kwa pamoja.

Wajibu wa Mteja kwa huduma hii
1. Mteja anawajibika kusaini mkataba kwa ajili ya huduma hii
2. Mteja anatakiwa kua na shahidi ambae ni ndugu ambae tutatakiwa kumrejeshea kiasi kitakachokua kimewekwa iwapo mteja atafariki dunia kabla ya kukabidhiwa gari
3. Kutunza taarifa zake za kibenki kwa kipindi chote atakachokua akiwekeza

Wajibu wa Kampuni
1. Kuhifadhi pesa ya mteja mpaka itimie kama ilivyokusudiwa
2. Kumsaidia mteja kuchagua gari nzuri iliyo katika ubora na kumshauri kulingana na kipato chake
3. Kusaini mkataba wa makubaliano ya kupokea pesa za mteja kila mwezi mpaka zitakapotimia kwa dhumuni la kumuagizia gari

Faida za Huduma Hii kwa mteja

1. Itakulazimisha kutimiza ndoto yako ya kumiliki gari kwa kua utalazimika kupunguza matumizi mengine kwa mda ili utimize hili
2. Kujengewa nidhamu ya matumizi bora ya pesa yako na utaratibu wa kujiwekea vapaumbele
3. Hautahusika kuongeza pesa iwapo thamani ya dola itaongezeka


Usalama wa pesa yako
1. Kimomwe Motors ni Kampuni ya kitanzania iliyosajiliwa na inayofanya kazi kwa sheria za nchi yetu
2. Tunasaini mkataba wa kutunza pesa zako
3. Ndugu yako wa karibu atasaini mkataba kama mrithi wako na shahidi iwapo utafariki dunia kabla ya wakati sahihi
4. Hakutakua na gharama nyingine za ziada
5. Kimomwe Motors imedhamiria kua kampuni kubwa ya kwanza ya Kiafrika ya uagizaji wa magari kwa Africa Mashariki na kati ndani ya miaka michache ijayo hivyo usalama wa pesa ya mteja ni jambo la kwanza litakalotuwezesha kutimiza malengo hayo

N.B: KUHUSU KUSHUKA NA KUPANDA KWA DOLA
Iwapo dola itapanda au kushuka, mteja hatotakiwa kuongeza au kurejeshewa kiasi chochote kwa sababu tutatumia thamani ya dola wakati tunasaini mkataba

Kwa maelezo zaidi na ufafanuzi kuhudu huduma hii na nyinginezo waweza kutupigia sim namba 0746267740 au fika ofisini kwetu Magomeni Mapipa

KIMOMWE MOTORS: SAVE MONEY SAVE TIME
Vipi Bajiaj nikiagiza mpaka inafikia hapa pamoja na ushuru na kila kitu itanikamua kama kiasi gani au hamhusiki nazo ?

Na je, utaratibu wa ugomboaji wa Bajaj na pikipiki bandarini ni sawa na magari ?
 
Kwa hii mpaka mkononi bei gani?
IMG_3385.JPG

BILA BIMA
 
Watu wamesepa na hela za kwenda Hijja sembuse huyu anaejidai eti wekeza kidogo-kidogo. Halafu taarifa za mteja za benki wewe muuza magari unataka za nini?
Shukrani kwa mawazo yako. Nadhani kuna sehem hujanielewa vizuri.... Kwa faida yako na faida ya wengine, huduma ya kuwekeza sio biashara yetu kuu, biashara yetu kuu ni mtu anahitaji gari anakuja na cash tunamuagizia anapata gari yake maisha yanaendelea. Hii ya wekeza tumeianzisha kama sehem ya kujali na kusikiliza maoni ya wateja ambao hawana uwezo wa kulipia pesa kwa mara moja hivyo wanahitaji miezi kadhaa kujichanga, na kwa sababu kuihifadhi pesa mpaka itimie ni ngumu hivyo tumekubali kubeba hilo jukumu la mtu kulipia kidogo kidogo kwa mda usiozidi miezi 24 akitimiza lengo lake tunamuagizia gari yake.

Hakuna mahali tumeomba taarifa za Bank za mteja katika maelezo hapo juu, kilichomaanishwa ni kua mteja ana wajibu wa kuhifadhi kumbu kumbu za deposits atakazokua akiweka kwenye akaunti yetu ya kampuni lengo likiwa ni kuhakikisha hesabu zetu na za mteja zinafanana

Natumai umenielewa vizuri boss wangu
 
Vipi Bajiaj nikiagiza mpaka inafikia hapa pamoja na ushuru na kila kitu itanikamua kama kiasi gani au hamhusiki nazo ?

Na je, utaratibu wa ugomboaji wa Bajaj na pikipiki bandarini ni sawa na magari ?
Hatuagizi bajaj boss wangu. Kuna mawakala wa Bajaj hapa Dar es Salaam vizuri uwatafute hao watakusaidia zaidi
 
Nimependa sana huduma yako, binafsi nina imani na nyie sana, kwakuwa nina ndugu yangu mshafanya nae bihashara mara mbili sasa.
Nitawatafuta hili niwekeze mdogo mdogo.
 
Nimependa sana huduma yako, binafsi nina imani na nyie sana, kwakuwa nina ndugu yangu mshafanya nae bihashara mara mbili sasa.
Nitawatafuta hili niwekeze mdogo mdogo.
Shukrani sana kwa ushuhuda mzuri huo boss. Karibu sana na tutafurahi kukuhudumia
 
Hawa waagiza magari wengi wao wezi na sababu kuu ni ujinga wa Watanzania.
Mtu anatumia smartphone ila anashindwa tafuta gari mtandaoni.

Hawa jamaa kama Crown ya 2004 GRS180 kuagiza hadi mkononi ni 10.5mil ila wao wanakuuzia kwa 14.5mil.

Wameongeza zaidi ya 4mil.

IST pia hivyo hivyo ukiiagiza inafika kwa 10mil na point wao wanaongeza 1 mil hadi 2.

Zaidi watakachofanya ni kuchezea speed o meter
 
Back
Top Bottom