Weka tabia za Kiswahili hapa, ambazo ni tofauti na wenzetu wa Magharibi (Wazungu & Wamerekani)

TAI DUME

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
8,854
23,103
Ijapokuwa kwasasa dunia ni Kama Kijiji kutokana na utandawazi lakini bado sisi Waswahili bado tunaendekeza baadhi ya vijitabia ambavyo ikitokea siku ukabadilisha mazingira ukaenda kuishi ughaibuni utapata tabu Sana. Mfano:

1. Uswahilini tumekuwa na kajitabia ka kujivunga kula ukikaribishwa chakula ugenini mpaka ubembelezwe bembelezwe ndio ujidai basi nitakula kidogo tu, mwisho wa siiku unamaliza poti zima peke ako. Aisee kwa wenzetu usiposema una njaa utaishia kuwaona wenzio wanajipashia chakula Cha kumtosha mwenyeji tu huku wewe ukiishia kuungurumisha matumbo kwa minyoo ya njaa.

2. Uswahilini tuna kijitabia Cha kutokuwa straight kwenye kumkukatalia mtu Jambo ambalo huwezi kumfanyia kwa kuogopa utaonekana mbaya au nawewe siku ikiwa na shida hautasaidika. Yaani kumwambia mtu no hiyo hela siwezi kukupa kwa sababu wewe NI mvivu au Sina nishida. Yaani mtu atuzunguuka ili tu asionekane mbaya. Kwa wenzetu huitaji hata sekunde kupewa jibu lako. Just "No I can't lend you some money because last time you were staborn in paying me back". Na inakuwa imeisha hiyo, ukimaindi poa ukielewa poa.

3. Kushindwa kumwambia ukweli mtu aliyekuja kukutembelea bila appointment kwamba una ratiba nyingine. Hata Kama unaharaka zako tunaona vibaya kumwambia Mgeni aondoke coz wewe unaratiba nyingine. Utabaki unamsikiliza mpaka aamue kuaga mwenyewe. Au ukithibutu kumwambia aondoke utaanza na misamaha kibao utafikiri wewe ndio mwenye makosa.

Kwawenzetu Kama huna appointment Cha kwanza mlangoni tu utaulizwa "what are you doing here?" Hata Kama unasharura atakuambia sahivi natoka njoo muda Fulani. Inakuwa imeisha hiyo mtu anafunga mlango anakuacha nje.

Vipo vijitabia vingi Sana ambavyo kwa namna moja au nyingine vinapelekea tuonekane ni watu tusiojielewa au vinatuchelewesha kwenye uchumi wa Kati mkuu.

Toa uzoefu wako hapa.

Kawoli.
 
1) Hivi tabia za wanawake kwenda kwenye "VIGODORO/BAIKOKO" hivi wenzetu magharibi wanazo?

2) Na tabia ya kutembeze "DAFTARI ZA MICHANGO" ya harusi, usipo changia basi unasuswa na jamii nzima, wenzetu magharibi pia wanazo?
Wana Strip Clubs kule, nadhani ndio vigodoro vilivyo advance,

Hata michango wanachangishana, sema kidijitali, Kama Go Fund Me n.k
 
1) Hivi tabia za wanawake kwenda kwenye "VIGODORO/BAIKOKO" hivi wenzetu magharibi wanazo?

2) Na tabia ya kutembeze "DAFTARI ZA MICHANGO" ya harusi, usipo changia basi unasuswa na jamii nzima, wenzetu magharibi pia wanazo?
Hiyo namba mbili kwakweli inaweza vumilika kwenye misiba. Lakini huku kwetu eti mtu mke wa kumgonga yeye anatuchangisha ndugu, majirani na marafiki? Utafikiri nasisi atatuazima mke siku moja moja. Kwawenzetu haiko hii.
 
Hiyo namba 1 umenikumbusha tulienda ugeni sehemu msosi ukaandaliwa akaja mama mmoja tukamkaribisha akawa anadai ameshiba tukamwambia anawe ili aonje japo tonge mbili sio vizuri kugoma hata kuonja.

Baada ya kunawa alikula mpaka tukashiba tukamuacha anaendelea tu kula.
 
Kutembea sehemu mbalimbali duniani, na ukawa na uwezo mzuri wa ku observe tabia za watu, basi utajua kuwa tabia za kibinadamu hazitofautiani sana.

Hizo zinazoitwa tabia za ‘Kiswahili’ hata kwenye nchi za Kimagharibi zipo na ninaziona kila siku.
 
mkiwa bar hata kama ni demu wako mna share the bills lakini kibongo bongo haiwezekani mi nilikua na demu wangu mzungu Ireland huko tumeenda kula vyombo siku iyo nikashangaa anakomaa na yeye alipe aisee nilishangaa badae nikazoea
 
mkiwa bar hata kama ni demu wako mna share the bills lakini kibongo bongo haiwezekani mi nilikua na demu wangu mzungu Ireland huko tumeenda kula vyombo siku iyo nikashangaa anakomaa na yeye alipe aisee nilishangaa badae nikazoea
Si kila mtu!

Wapo wengi tu ambapo wanaume ndo hulipia kila kitu!
 
Kutembea sehemu mbalimbali duniani, na ukawa na uwezo mzuri wa ku observe tabia za watu, basi utajua kuwa tabia za kibinadamu hazitofautiani sana.

Hizo zinazoitwa tabia za ‘Kiswahili’ hata kwenye nchi za Kimagharibi zipo na ninaziona kila siku.
Wapo wanaosema kuwa kinachofanya nchi za watu weusi na weusi wakose maendeleo sio kuwa wamezidiwa akili na wazungu, ila ni culture, je kama culture zetu ni sawa, akili zetu ni sawa , kinachosababisha weusi wasiendelee ni nini?
 
🤣🤣🤣 nimekumbuka tabia ya mshua wangu mkubwa kama ulikuwa waenda kwake bila appointment imekula kwako..anakuacha getini na uso umekushuka..😂😂😂..

Mbaya zaidi mkewe alikuwa na tabia anatoka mkoani bila taarifa hata ikiwa usiku mkubwa vipi hamfungulii mlango anakuja kulala home...😔😔😔 Sii poa hata kidogo.
 
Wazungu na wamarekani ndio huongoza kwa umbeya wa kimataifa wa kujadili na kuingilia Mambo ya ndani ya nchi zingine ikiwemo kuwapiga na kuondoa viongozi wao

Kwenye umbeya wa kimataifa ulaya na Marekani wanashika namba moja
Hii naina ni swala la kisera zaidi kuliko kuwa vijitabia katika household basis.
 
Back
Top Bottom