Weka kura yako hapa,"Kati ya Kigoma na Rukwa" wapi kumepiga hatua kimaenendeleo?

buhange

JF-Expert Member
Oct 23, 2011
505
110
Ndugu wana JF Kumezuka ubishi mkali sana hapa mtaani, kwamba kati ya Mkoa wa Rukwa na Mkoa wa Kigoma, wepi wanahaki ya kutamba kifua mbele kwamba wanawazidi wenzao kimaendeleo ktk kada zote? KURA YAKO TAFADHARI...Chaguo lako lisisimamie ktk upendeleo wa asili unakotoka.
 
Mkuu, inawezekana swali langu hili hapa JF likawa limebeba maana ndogo sana kutokana na upeo wangu huu mdogo, ila mpaka nimefikia uamzi wa kutupia uzi huu ni baada ya ubishi mkubwa wa wanajamii hapa mtaani, tena siyo leo tuu wala mara moja. Wanaobishana si wenyeji wa maeneo hayo ila wengi wao wamepita kiashara, kikazi n.k. Wao wanajaribu kutoa tetezi zao kwa vigezo kama Miundombinu, Mzunguko wa biashara, Elimu na hata Uzalishaji mali kwa ujumla. Tunajua kwamba these areas we both Labour reserve zones kwa mjibu wa historia. Sasa kwa maelezo haya mafupi, wewe uonavyo kwa mtazamo wako, wapi ni zaidi ya kwingine? Na kwa nini? Nawasilisha.
 
Vipofu wanapobishania ukubwa wa Tembo wakati wote hawaoni!
 
Naijua mikoa yote miwili na mimi si mwsnyeji wa huko ila nimebahatika kuweko huko kote kwa kipindi cha miezi 12 iliyopita. Opinion yangu ni kwamba Kigoma iko juu kiuchumi
 
Yote ni mikoa yenye wananchi mafukara ila Kigoma kuna afadhali kuliko Rukwa.
 
Me naona Rukwa angalau japo wote hali mbaya lakini Rukwa ina hatua kidogo
 
Mimi ni mwanaRukwa ruka slogan yetu wakati mkoa unaanzishwa pia nimewahi kukaa kigoma kwa muda wa wiki mbili kwenye project ya NGO flan. In short tuache ushabiki Kigoma ipo juu kwa Rukwa tena kwa umbali mkubwa sana.Angalia from Mwandiga to Manyovu mpaka Burundi ni lami pia barabara nyingi za mkoa wa Kigoma pale mjini zimeunganishwa kwa lami but Rukwa kuna barabara ya lami ya 10 km kutokea kwenye ule ubao ambao umeandikwa karibu Sumbawanga mpaka kwa mkuu wa mkoa. Pia fursa za biashara kati ya Rukwa na Kigoma bado Kigoma wapo juu ingawa waha ni wabishi kwa asili lakini wafipa ni wakarimu na waungwana
 
Rukwa kwa umri wake naipigia chapuo. Kigoma ni mkoa mkongwe ukilinganisha na Rukwa.Tangu enzi za akina "Dr, Livingstone, I presume?" ndo uilinganishe na Rukwa...?
 
Ndugu wana JF Kumezuka ubishi mkali sana hapa mtaani, kwamba kati ya Mkoa wa Rukwa na Mkoa wa Kigoma, wepi wanahaki ya kutamba kifua mbele kwamba wanawazidi wenzao kimaendeleo ktk kada zote? KURA YAKO TAFADHARI...Chaguo lako lisisimamie ktk upendeleo wa asili unakotoka.
afadhali kigoma kuna maendeleo kidogo,pale kuna vivutio vya utalii ambavyo vimeleta maendeleo pale
 
Ndugu wana JF Kumezuka ubishi mkali sana hapa mtaani, kwamba kati ya Mkoa wa Rukwa na Mkoa wa Kigoma, wepi wanahaki ya kutamba kifua mbele kwamba wanawazidi wenzao kimaendeleo ktk kada zote? KURA YAKO TAFADHARI...Chaguo lako lisisimamie ktk upendeleo wa asili unakotoka.

hivi kigoma chakula kisha panda bei maana nilikuwepo huko miaka ya 2000 mpka 02 hivi na lami yao moja tokea stesheni mpaka ujiji na kipande chengine toka mwanga katubuka mpka mwandiga..
 
duuh! Kigoma au Rukwa?? Me nafikiri kura yangu imeharibika sababu sijaifika huko!
 
Rukwa kwa umri wake naipigia chapuo. Kigoma ni mkoa mkongwe ukilinganisha na Rukwa.Tangu enzi za akina "Dr, Livingstone, I presume?" ndo uilinganishe na Rukwa...?
Enzi unazozungumzia kulikuwa hakuna mikoa ya Kigoma, Rukwa wala Tabora. Kulikuwa na Western Province, makao yake Tabora. Mikoa ya Kigoma, Rukwa na Tabora yote ilimegwa kutoka Western Province mara baada ya Uhuru, ndo maana Tabora ilionekana imeendelea kuliko Kigoma na Rukwa ingawa kwa sasa Tabora i hoi zaidi
 
Kama unawashindanisha kwa uchawi na ushirikina sawa, ila suala la maendeleo HAMNA KITU.

Labda niwatetee watani zangu Waha, si kosa lao, ni funza wametafuna miguu mpk ubongo umenock
 
Back
Top Bottom