Weka hapa wazo lolote la Kiuchumi ambalo likitekelezwa litasaidia nchi yetu

DENLSON

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
944
1,252
Niwaombe watanzania na wote wenye mapenzi mema na taifa letu kutoa mawazo yao ambayo yakitekelezwa au kuboreshwa yatasaidia:
  • Kuinua uchumi.
  • Kutengeneza ajira mpya.
  • Kukuza biashara.
  • Kuanzisha bishara.
  • Kuvutia wawekezaji.
  • Kuongeza ukusanyaji wa kodi/mapato.
  • Kuboresha miundombinu.
Mawazo sio lazima yatekelezwe leo au kesho, lakini kupitia hapa wafanya maamuzi wanaweza kuona na hata kama ni maiaka 10 ijayo kwani bwawa la umeme si wazo la 1980 huko na liantekelezwa leo 2021.
 
kuna wakati mwenzetu JF alitupia mchango muhimu sana; nadhani Madam President Samia Hassan akifanyia kazi haya, basi nchi hii itaweza kusisimua mifumo yake ya uzalishaji.
Karibu kwa rejea

 
Niwaombe watanzania na wote wenye mapenzi mema na taifa letu kutoa mawazo yao ambayo yakitekelezwa au kuboreshwa yatasaidia:
  • Kuinua uchumi
  • Kutengeneza ajira mpya
  • Kukuza biashara
  • Kuanzisha bishara
  • Kuvutia wawekezaji
  • Kuongeza ukusanyaji wa kodi/mapato
  • Kuboresha miundombinu
Mawazo sio lazima yatekelezwe leo au kesho, lakini kupitia hapa wafanya maamuzi wanaweza kuona na hata kama ni maiaka 10 ijayo kwani bwawa la umeme si wazo la 1980 huko na liantekelezwa leo 2021.

Niwaombe watanzania na wote wenye mapenzi mema na taifa letu kutoa mawazo yao ambayo yakitekelezwa au kuboreshwa yatasaidia:
  • Kuinua uchumi
  • Kutengeneza ajira mpya
  • Kukuza biashara
  • Kuanzisha bishara
  • Kuvutia wawekezaji
  • Kuongeza ukusanyaji wa kodi/mapato
  • Kuboresha miundombinu
Mawazo sio lazima yatekelezwe leo au kesho, lakini kupitia hapa wafanya maamuzi wanaweza kuona na hata kama ni maiaka 10 ijayo kwani bwawa la umeme si wazo la 1980 huko na liantekelezwa leo 2021.
Serikali kuu na TAMISEMI waache kuagiza magari mapya...kila department itumie same vehicle Kwa miaka 10..Kwa mfano..gari la waziri,naibu,mkuu wa mkoa ,Katibu mkuu,wakurugenzi wa idara,DC,ded na maafisa wa vyombo vya dola wasibadirishe magari mpaka wanayoyatumia yatimize miaka kumi kwenye docket zao..na pesa itakayookolewa iwekezwe VETA na Sido kuwawezesha vijana wa kitanzania kupata ustadi na nyingine iwekezwe kwenye kilimo cha biashara..pia nashauri nafasi ya DC na DED iunganishwe na kupata strong organ itakayosaidia kusukuma maendeleo huko Chini.
 
Wapunguze kodi ya maroli ya mzigo na mchanga ili kufanikisha uraihisi wa kusafirisha bidhaa kutoka mashambani vitu havitaozea huko maporini kwa magari mabovu tunayokodi huku yaliyo bora yakipeleka mafuta Congo hata mitambo kama concrete mixer au magari ya taka wafikilie kiwango cha kodi upya maana magari mengi ya taka mikoa mingi nimeyaona nayo ni taka pia..
Ikiwezekana wapunguze kodi kwenye landcruiser hizi za utalii ili kuinua ubora wa magari kwa wageni hiyo Kodi wataipata baada ya kuongezeka kwa wageni kwa kutumia hayo magari na wamiliki kununua mafuta...
 
Niwaombe watanzania na wote wenye mapenzi mema na taifa letu kutoa mawazo yao ambayo yakitekelezwa au kuboreshwa yatasaidia:
  • Kuinua uchumi.
  • Kutengeneza ajira mpya.
  • Kukuza biashara.
  • Kuanzisha bishara.
  • Kuvutia wawekezaji.
  • Kuongeza ukusanyaji wa kodi/mapato.
  • Kuboresha miundombinu.
Mawazo sio lazima yatekelezwe leo au kesho, lakini kupitia hapa wafanya maamuzi wanaweza kuona na hata kama ni maiaka 10 ijayo kwani bwawa la umeme si wazo la 1980 huko na liantekelezwa leo 2021.
Tutumie mfumo wa malipo ya lisaa kwenye ajira zote tuachane na huu wa malipo baada ya siku 30....
 
Vijana wengi wapewe maarifa ya kisasa ya ufugaji, kilimo, Na ufundi Na kuwepo Na namna ya kuwawezesha/ kuwasaidia kuanzisha shughuli hizo pindi wamalizapo masomo
 
Serikali ijikite katika kufanya Tanzania kuwa moja ya mataifa duniani yenye wajenzi bora kabisa, ( hii ifanyike BILA KUDHALAU FANI NYINGINE), Kwa kuanzia;

1. Iliunde upya shirika la nyumba la taifa (NHC) ili lijikite katika kutengeneza nyumba za kuishi, shule na majengo mengine yaliyo bora kwa gharama nafuu. Hii inawezekana!

2. Ilifufue shirika la MECCO ili lijikite, kwa kuanzia, kutengeneza barabara za mitaani na mifumo ya maji ya mvua.

3. Itenge na kupima maeneo sahihi ya kujenga miji mipya yenye kushirikiana na miji ya sasa kila mkoa.

4. Itenge fungu la fedha (kwa mkopo au kutoka bajeti ya maendeleo, n.k. ) ilikuanza ujenzi wa miji iliyopangwa na yenye kiwango kwa kupitia NHC na MECCO, TANESCO, TTCL n.k.

Ujenzi holela usinamishwe mara moja, ni hasara kwa taifa.

5. Lengo ni kuhakikisha Tanzania yote imejengwa kwa mpangilio.

  • Nyumba zinazotengenezwa ziuuzwe/zipangishwe kwa wananchi.
  • inawezekana kuwa na nyumba bora kwa gharama nafuu kwa kuwa;

a. Madirika husika yatanunua material ya ujenzi kwa wingi na hivyo kuwa na nguvu ya kupata kwa bei ya chini.

b. Lengo halitakuwa kupata faida kubwa, ila itakua kuhakikisha pesa of nayowekwa kwenye mradi haipotei au kupungua thamani.

n.k.

Faida za kufanya hivi.

1. Maisha bora kwa wananchi kwa kuwa na makzi bora.

2. kwa kuwa huu utakua ni mradi mkubwa wa nchi nzima, na endelevu, utaleta ajira nyingi zilizo rasmi. Ajira wakati wa ujenzi na kwa kupitia ukarabati endelevu.

3. Sasa italeta ulazima wa kuanzisha au kuboresha viwanda vinvyotengeneza vifaa vya ujenzi.

Ikiwa ni pamoja na kuchimba chuma na kutengeneza bidhaa zake kama nondo, misumali n.k.

4. Wananchi wasio na fani za ujenzi, mf walimu, madaktati, wakulima, n.k. watajikita katika kuwa wazuri katika kazi zao ilikuweza kununua/kupangisha nyumba bora, ukilinganisha na hali ya sasa ambayo wanalazimika kujua ujenzi ili wasimamie ujenzi wa nyumba zao ambazo nyingi zinakua chini ya kiwango.

kumbuka ni ndoto ya karibu kila mmoja wetu kumiliki nyumba bora, je sote inabidi tuwe wajenzi?

5. shirika kama Posta litaweza kusambaza huduma mpaka majumbani, kwakuwa miji ikipangwa ni rahisi kuweka anuani za nyumbani. Mashirika mengine kama ya mawasiliano na usafiri n.k yatafaidika pia.

5. kama taifa tutaluwa uwezo mzuri wa kijenzi, na kwakuwa tumezungukwa na nchi ambazo hazijajengwa kwa mipangilio mizuri, basi tunaweza kujenga na huko kwa faida. Pia tutauza vifaa vya ujenzi huko pia.

6. Huko mbeleni MECCO itaweza kutanuka na kujenga barabara kuu na madaraja n.k.

7. kwa kujenga wenyewe bila kumtegemea mchina, mkorea n.k Tutakuwa chimbuko la kumnyanyua mtu mweusi ambaye kwasasa anadharailika duniani kama mtu maskini na asiyejiweza kiakili kama wengine. Kwa hali ya sasa tunamtegemea sana mchina kwa ujenzi..

tujue kwa wazungu walijenga kwao, wachina wamejenga kwao, tusiwe tofauti, na sisi tijenge kwetu.

8.n.k
 
Niwaombe watanzania na wote wenye mapenzi mema na taifa letu kutoa mawazo yao ambayo yakitekelezwa au kuboreshwa yatasaidia:
  • Kuinua uchumi.
  • Kutengeneza ajira mpya.
  • Kukuza biashara.
  • Kuanzisha bishara.
  • Kuvutia wawekezaji.
  • Kuongeza ukusanyaji wa kodi/mapato.
  • Kuboresha miundombinu.
Mawazo sio lazima yatekelezwe leo au kesho, lakini kupitia hapa wafanya maamuzi wanaweza kuona na hata kama ni maiaka 10 ijayo kwani bwawa la umeme si wazo la 1980 huko na liantekelezwa leo 2021.
Hili nitakaloandika hapa halihitaji kuchukua muda Mrefu kutekeleza na huu ndiyo Muarobaini wa kupaa kiuchumi:

1.Kilimo:

Kwa,mazingira tuliyoko,Tanzania inapaswa iwe na itambulike kama BANK YA CHAKULA KWA AFRICA NZIMA NA sehemu nyinginezo Duniani.

Serikali:

Ijenge Miundo mbinu *(Silos)integrated kiasi kwamba wakulima wanaweza kufungua account za Mazao kwenye SILOS.

KWANZA muundo huu utaondoa kabisa tatizo la post harvest losses na pili Wakulima watauza mazao kwa faida kwa sababu hayauzwi kwa pressure zitokanzo na kuharibika kwa Mazao hayo.

That shall be called a food Bank model.

Serikali jengeni hii miundombinu na kuendesha ktk muktadha wa PPP.

WAKULIMA wanachama wanatafutwa kama mteja wa Bank anavyofungua account....

2.Upper hand kwenye mazao ya Biashara **(Subsidies kwa wakulima wanaoachieve high grade)

3.livestock.....Modernization...
-Acquaculure-Heavily invested. .

4.Industrialization........

Light

Heavy....

Ebu chukueni hizo kwanza...
 
Suala kodi (ushuru) wa uagizaji magari uangaliwe upya yatupasa tujiulize hizi bei tumepanga wakati tumelewa au tulikuwa usingizini?!

Muuzaji anakuuzia milioni5 halafu ushuru unalipa million 15!..
Tupunguzieni ushuru na ulipwe walau asilimia 10 ya bei ya gari husika na pia ikiwezekana ulipwe kwa utaratibu wa mwaka1 kama ilivyo kodi ya mapato kwa mtiririko wa kila robo ya mwaka, hapo sasa kila gari ambayo ushuru haujakamilika inafungwa king'amuzi kuifatilia kama ilivyo gari zinazobeba mizigo ya transit au zile za mikopo ya benki.

Kwa utaratibu huu TRA na kodi za mafuta zitaongezeka mara nyingi zaidi kuliko sasa Hays masuala ya kusema gai chakuvu hatuoni mabadiliko yaliyofanyika hasa kwa gari ndogo bado used ndio zimetawala kwa àsilimia kubwa.

Wabunge wetu waache ubinafsi kwenye kutunga hizi sheria na pia mamlaka husika zijitahidi kutunga miswada rafiki kwa sisi wananchi wa chini na si kutazama watu wa level fulani, mkigusa jamii ya chini kwenye wengi huku ndio kwenye pesa na hata kanuni zenu za kodi ziko namna hiyo jamii ya chini ndio kubwa sasa ni wakati wa kufanya mabadiliko ya kutugusa huku moja kwa moja.
 
Mfumo wa vyama vingi ufutwe, muda mwingi unatumika kujadili ujinga
Mambo ya siasa na vyama yafutwe kabisa. Tuwe tunachagua viongozi kuanzia mtaa/kijiji, kata na wilaya kwa kufanya usaili/interview. Kwenye wilaya kuwe na ofisi ya DED na ofisi zingine za umma (ambapo watumishi wanapatikana kwa usaili).
 
Dreamliner moja iliyopaki ni sawa na matreka elf 10 mapya na vifaa vyake tena kwa cash, Kama ni kwa mkopo unapata trekta elf 50 za horse power 75.Trekta moja ulima heka 25 kwa siku kwa speed ya kivivu. Trekta moja utoa ajira kwa vijana 100.
So badala ya dreamliner moja iliyopaki kutoa ajira kwa watu 30 zingekuwa ni trekta zingetoa ajira milioni 5 za moja kwa moja achilia wategemezi wao.Ajira zote zilizonunulia ndege zingenunua trekta laki moja ambazo zingetoa ajira milioni 12 nchi nzima.Ndege ugusa wachache,kilimo ugusa wote.Kama Malaysia waliwekeza kwenye michikichi tu ndo wanailisha dunia mafuta ya kula na bado awajalijaza soko. Soko la mazao ya kilimo duniani ni kubwa hata KILA mtu alime tza hatutoweza kulijaza.Hela zilizotupwa kwenye ndege tilioni moja tungepata matreka laki 2 yangeajiri vijana milioni 12 zingemaliza tatizo la ajira nchini kwa kuwekeza kwenye kilimo mkakati na zingesharudi ndani ya miaka 3 tungepata pesa tosha za kigeni kukamilisha miradi yote bila kutegemea kukopa.Kupitia kilimo tu tungekuwa uchumi wa kati.Kama wakoloni wao waliweza maliza tatizo la ajira nchini why tunashindwa?Tangu Uhuru bado atujapata kiongozi sahihi mwenye uchungu anaeguswa na ugumu wa maisha ya watz,zaidi ya kuyafanya maisha yazidi kuwa magumu.Kwann watumishi wasipewe misamaha ya Kodi Ili wajinunulie magari binafsi kuliko kuwa na utitiri wa magari ya serikali ambayo hayazalishi,hayana faida ni hasara kwa mlipa Kodi V8 moja tu ni sawa na matrekta 10 mapya na jembe zake hapo ni sawa na ajira elf 1.
Tuendelee tu kuwalaumu mabeberu juu ya kushindwa kwetu aliyetupa Mali alitunyima akili.
 
Mambo ya siasa na vyama yafutwe kabisa. Tuwe tunachagua viongozi kuanzia mtaa/kijiji, kata na wilaya kwa kufanya usaili/interview. Kwenye wilaya kuwe na ofisi ya DED na ofisi zingine za umma (ambapo watumishi wanapatikana kwa usaili).
True hata mawaziri waombe Kazi na sio kuteuliwa.
 
1. Wajenge masoko ya kimataifa kwenye mikoa ya mipakani kama Kagera, Mbeya, Songwe, Kigoma etc. Na yawe kama EPZ. Lengo ni kuwa nchi tunazopakana nazo zisifuate bidhaa Dubai au China bali kwenye masoko hayo.

2. Waruhusu wakulima kuuza mazao kokote watakako na waruhusu wanunuzi wa mazoa kutoka nje ya nchi bila urasimu.

3. Wajenge irtigation schemes.

4. Warahisihe kupata passport, kigezo kiwe NIDA tu.

5. Nchi ianze kuzalisha chuma.
 
Back
Top Bottom