Weka hapa Tiba asilia ulizowahi kutumia na zikakusaidia, mimi zangu hizi hapa

Mkuu, kila siku sukutua na chumvi, bumba mate mazito yenye chumvi sukutulia eneo lenye jino bovu. Unasukutua unatema mate (chumvi ibakie mdomoni) utasukutua HADI ile chumvi uliyoweka mdomoni iishe.

Hii ni mjarabu kabisa bila rongo rongo.

Hata jino likikuuma litulize kwa hiyo style
shukrani sana boss
 
Muhimu: Uzi huu hauhusishi matatizo ya nguvu za kiume, tayari kuna uzi wake maalum jukwaa la mapenzi

Huu ni uzi spesho wa mirejesho yetu tuliowahi kutumia tiba asili na zikatusaidia, yaani sisi ndio tuwe mashuhuda sio kukopi ma kupesti humu.

1. Nilikuwa nakula samaki ghafla kimfupa kikanikomea kwenye koo, nilijaribu kukohoa kwa nguvu lakini wapi, kuna rafiki yangu alikuwa mtu wa kanda ya ziwa akanipikia ugali mgumu, niliambiwa nipige tonge zile kubwa bila mboga yoyote, Tonge la kwanza tu mfupa ukateremka nikabaki nashangaa na nilimshukuru sana, nilikuwa nimepanga niende hospitali ila rafiki alinisaidia.

2. Funza kwenye kidole anaesababisha kidole kivimbe na maumivu makali, maumivu yalikuwa makali sana, nilienda hospitalini wakaniambia kucha itolewe, niliwaambia hakuna tatizo ntakuja, ulifikiri nilienda !! nikiwa natafta njia mbadala nikaambiwa na dada flan kaishi bush utotoni kwamba dawa ni kuvaa ndulele / turatura / ndura / nyanya pori, yaani unaichuma unaikata juu na chini iwe kama pete alafu unaivaa iishie ile sehemu yenye mdudu, ule utomvu ni sumu kwa mdudu yule, yaani ukiivaaa atahangaika sana mpaka afe ila nawe mda huo chamoto utakiona, akifa maumivu yanaisha na kidole kinakuwa na usaha, unakitoboa huhisi maumivu yoyote yale, unakamua usaha wote.

3. Kwikwi - hii dawa yake ni kunywa maji, ama upate uwoga mfano utishiwe umeiba kitu, kuna nyingine ni sugu sijajua wanatibu vipi.

Kuna mdudu huwa anasababisha kidole kuuma na kuvimba pia,,,,huyo mdudu ni nani? Au tetenasi?kuna jamaa zangu wawili walifariki kisa kuwa na huyo mdudu vidoleni,,
 
Mkojo wa asubuhi kwa matatizo ya meno.

Nilikuwa napata matatizo ya meno mara nyingi, nikashauriwa kusukutua na mkojo wa asubuhi,

Baada ya hapo nikapona hadi leo
 
Kuna mdudu huwa anasababisha kidole kuuma na kuvimba pia,,,,huyo mdudu ni nani? Au tetenasi?kuna jamaa zangu wawili walifariki kisa kuwa na huyo mdudu vidoleni,,
Huyo dawa yake ni ndulele unakamlia hapo kwa kidole huska mambo yanakuwa bambam
 
Mkojo wa asubuhi kwa matatizo ya meno.

Nilikuwa napata matatizo ya meno mara nyingi, nikashauriwa kusukutua na mkojo wa asubuhi,

Baada ya hapo nikapona hadi leo
Matatizo gani ya meno ?? Meno kuwana rangi mbaya ? Wala meno kuuma
 
Hapana ipo, ila umwekee kipindi hafahamu nenda kwenye banda la kuku kama unafagia chukua baadhi ya kinyesi cha kuku kilichokauka vizuri kisage kiwe unga kirainike hasa kisha muwekee kwenye bia anayokunywa ila hakikisha hajui baada ya hapo atatapika sana na kuichukia harufu yyte ya pombe
Kama ana mke anayenyonyesha pasipo yeye kujua " Kamua maziwa na umuwekee kwenye pombe". Hutajuta japo utajuta atakapokuwa anatapika. Hatarudia tena.
 
Jamani anayefahamu dawa ya tumbo la wanawake linalouma upande wa kushoto chini ya kitovu au daktari wake. Msaada tafadhali.
 
Kuna mti. Mmoja utomvu wake niliuweka kwenye fresh woond siku 2 tu
 
Mimi naombeni nisaidieni mtu anayejua dawa ya kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa mwanamke sijui ndo kuongeza nguvu za kike

tumia Ndizi+ Maziwa fresh+ Karanga + Vijiko 4 Vya Asali

Hakikisha unavisaga kwenye blender ili uweze kupata mchanganyiko mzuri, hapo itakuwa Tayari Sasa Kwa matumizi, tumia ndani ya week 2 kutwa mara tatu utakuja kunishukuru
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom