Weka hapa Tiba asilia ulizowahi kutumia na zikakusaidia, mimi zangu hizi hapa

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
3,811
11,744
Muhimu: Uzi huu hauhusishi matatizo ya nguvu za kiume, tayari kuna uzi wake maalum jukwaa la mapenzi

Huu ni uzi spesho wa mirejesho yetu tuliowahi kutumia tiba asili na zikatusaidia, yaani sisi ndio tuwe mashuhuda sio kukopi ma kupesti humu.

1. Nilikuwa nakula samaki ghafla kimfupa kikanikomea kwenye koo, nilijaribu kukohoa kwa nguvu lakini wapi, kuna rafiki yangu alikuwa mtu wa kanda ya ziwa akanipikia ugali mgumu, niliambiwa nipige tonge zile kubwa bila mboga yoyote, Tonge la kwanza tu mfupa ukateremka nikabaki nashangaa na nilimshukuru sana, nilikuwa nimepanga niende hospitali ila rafiki alinisaidia.

2. Funza kwenye kidole anaesababisha kidole kivimbe na maumivu makali, maumivu yalikuwa makali sana, nilienda hospitalini wakaniambia kucha itolewe, niliwaambia hakuna tatizo ntakuja, ulifikiri nilienda !! nikiwa natafta njia mbadala nikaambiwa na dada flan kaishi bush utotoni kwamba dawa ni kuvaa ndulele / turatura / ndura / nyanya pori, yaani unaichuma unaikata juu na chini iwe kama pete alafu unaivaa iishie ile sehemu yenye mdudu, ule utomvu ni sumu kwa mdudu yule, yaani ukiivaaa atahangaika sana mpaka afe ila nawe mda huo chamoto utakiona, akifa maumivu yanaisha na kidole kinakuwa na usaha, unakitoboa huhisi maumivu yoyote yale, unakamua usaha wote.

3. Kwikwi - hii dawa yake ni kunywa maji, ama upate uwoga mfano utishiwe umeiba kitu, kuna nyingine ni sugu sijajua wanatibu vipi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

20 Reactions
Reply
Top Bottom