Tetesi: Weka hapa Taarifa Muhimu,toka mitandao mbalimbali ya kijamii

NI MTAZAMO TU

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
1,203
998
Mimi toka Muungwana blog nimeona hii.

MWANASOKA bora wa dunia, Cristiano Ronaldo ameamua kuondoka Real Madrid baada ya kuwaambia wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya Ureno nia yake, kwa mujibu wa taarifa kutoka Hispania.

Mustakabali wa Ronaldo Real Madrid haueleweki kutokana na mshambuliaji huyo kusema hana furaha kufuatia kesi ya kukwepa kodi Hispania, Pauni Miklioni 13. Ameionya klabu hiyo ataondoka iwapo atatiwa hatiani.

Na gazeti la la Marca la mjini Madrid limesema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 atafanya hivyo baada ya kuwaeleza wachezaji wenzake wa timu ya taifa mipango yake.

Ronaldo kwa sasa yuko Urusi na kikosi cha Ureno kwa ajili ya michuano ya Kombe la Mabara Confederations kujaribu kurudia mafanikio yao ya Euro 2016 nchini Ufaransa.

Nukuu katika gazeti la Marca inasema kwamba Ronaldo amewaambia wachezaji wenzake: "Ninaondoka Real Madrid. Nimefanya maamuzi. Hakuna kurudi nyuma.'

Paris Saint-Germain ikitajwa kama klabu ya kwanza ambayo mchezaji huyo anaweza kujiunga nayo, inatarajiwa kuanza rasmi kuifukuzia saini ya Cristiano Ronaldo kama mshindi huyo wa Ballon d'Or nne ataondoka Real baada ya msimu mzuri akiiachia taji la La Liga na Ligi ya Mabingwa.

Manchester United ingependa kumrejesha nyota huyo Mreno huyo Old Trafford, lakini kwanza wanatakiwa kuchunguza baada ya taarifa ya kufanyika kikao cha siri kati ya wakala wa Ronaldo, Jorge Mendes na Rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi mjini Cardiff mchana kabla ya fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Inafahamika Mendes amemuambia Al-Khelaifi juu ya matatizo hayo yanavyozidi kukuwa na amemuahidi kuendeleakuwasiliana kupeana taarifa zaidi.

PSG imekuwa ikimfukuzia mwenye umri wa miaka 32 kwa miaka sasa itakuwa tayari kutumia kiasi chochote cha fedha ili kumpata Ronaldo.
 
Hana jipya huyo faza,man united tunahitaji damu changa zenye kiu ya mafanikio
 
Kutoka wasafi WhatsApp:
Raia nchini Afrika Kusini waadhimisha miaka 41 tangu mauaji ya wanafunzi weusi na polisi weupe wa ubaguzi wa rangi.

Wanafunzi weusi walikuwa wanaandamana katika kitongoji cha Soweto jijini Johannesburg mnamo mwaka 1976 kupinga lugha ya Afrikaans kutumika kama lugha rasmi katika shule .

Kipindi hicho serikali ilikuwa chini ya watu weupe,polisi waliwaua wanafunzi hao waliokuwa wanaandamana kwa risasi .

Wanafunzi wengi waliuawa na idadi kamili ya waliouawa haijulikani .

Hafla mbali mbali kote nchini zimeandaliwa na serikali na upinzani ishara ya heshima kwa wanafunzi waliojitoa mhanga kipindi hicho.
 
MWANDISHI WA MAKALA ILIYOSABABISHA GAZETI LA MAWIO KUFUNGIWA
ADAI KUTISHIWA MAISHA NA WATU WASOJULIKANA
TAARIFA INA REPOTIWA KUTOKA DW NOW
 
Back
Top Bottom