Weka gari yako ya umeme itakayompoteza Lucid Air!

Mad Max

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
23,079
63,136
Hii Lucid Air kutoka Lucid Motors, USA, ni chuma na nusu aisee, especially kwa wadau wa executive sedans.
2022_Lucid_Air_Grand_Touring_in_Zenith_Red,_front_left.jpg

Naikubali katika sekta zote tatu kuu, muonekano, technology na performance!

GIMS_2024,_Le_Grand-Saconnex_(GIMS0087-2).jpg


Kwa muonekano, chuma inavutia sana, kuanzia nje na ndani. Imekaa kistylish na kisasa ukifananisha na sedans nyingi za class yake, ata Model S, Tycan na sedans za EV kutoka Ujerumani zinakalishwa.
2023_Lucid_Air_Touring,_rear_7.23.23.jpg


Technologically, chuma inakuja na ADAS yao inayoitwa DreamDrive, ambayo ina sensors karibia 32 ikiwemo camera 14. Vyote ivyo ni kusaidia katika autonomous driving assistance.
Lucid_Air_Dream_edition,_IAA_Open_Space_2023,_Munich_(P1120054).jpg


Chuma pia ina active suspension, panoramic sunroof, executive rear seats, na wapenzi wa audio kuna speaker system 29, zikija na noise cancellation, utachagua rim size 20 au 21, na seat ya mbele unaweza kuadjust mara 22 pia ina ventilation na massage.

Performance
Hii chuma ni moja ya quickest EV Duniani, inakuja na option ya motor mbili, tatu au nne (kwahiyo utachagua RWD au AWD), na horsepower zinafika hadi 1300 kutegemea na model na range hadi kilometa 800+!!
Lucid_Air_Electric_Drive_Unit_and_Battery.jpg

Base level ya Lucid Air inatumia battery la 88 kWh ambayo ni RWD, inayotoa 430 hp na range ya 653 km wakati Lucid Air Dream Edition Performance inatoa 1,111 hp na ina acceleration ya 0-100 kph ya 2.5 sec, na inaweza kufika top speed ya 378 km/h.
Lucid_Air_Chassis_-_center_and_rear.jpg


Pamoja na kwamba gari ni high performance, kali na ipo quick, ila ni very efficient pia. Mfano, Lucid Air GT ina efficiency ya 0.16kWh/km (approximately sawa na 55 km/L)!

Bei tusiongelee sana ($70,000 unapata Tesla Model 3 hapo mbili) lakini ni moja ya best kama sio namba 1 EV nnayoiona ni kali.

Weka yako tuone!
 
Back
Top Bottom