Weekend story! BEN 10

Nani mwingine ameyaelewa maombi ya Ghost kwa Mungu, Yaani nimecheka mno eti Mungu nakujengea makanisa na kusomesha yatima wako na kuuza unga kidogo tu LOL.

Story za Lara1 ukidhani hii ndo the best of all akileta nyingine ana outdo unajikuta kila story ni best ukilinganisha na nyingine. Personally nishachoka kumsifia fanani apambane na hali yake tu sa hivi.
 
Najua mshapata upande mmoja wa story yangu ya kufumaniwa! Nasisitiza msomaji huo ni upande mmoja tu! Na umeletwa kwa lengo la kunichafua na kuninyongonyeza! Na kunifanya nionekane sina thamani, wala sina maana yoyote!

Mwanzo kabisaa niliolewa out of fear na stigma huenda bikaishia peke yangu! Maana kasumba kasumba hizi! We kataa wanaume wa maana, wanapoteaga hawa! Utakosa hata wa kukupa mambo! We jitie mchagua sanaa! Mwisho utachagua koroma!

Hizi tantalila zikaniingia nikajikuta tu nipokwenye kona nalazika kufanya mamuzi magumu! Moyo haujaridhia ila jamii ndo imenoshika kidete! Maana ilifika stage mashosti wote wameolewa! Kila mtu anaenda kwake kupika! Yuko busy na mume wake! Nikasema hapa sina namna! Sina ujanja! Kuendana na kasi hiisina budi kuolewa! Liwalona liwe!

Kipindi hiko huyu mume wangu kubwa la maadui alikuwa malaya mbwa! Alikuwa na pesa kama yote! Na mimi i was doing more than okay! Nilikuwa nishakuwa head wa idara! Na napokea pesa nzuri! Nishajenga, nishanunua Prado! Kibongo bongo naweza sema nishamaliza kila kitu! Bado tu kuolewa na kuzaa!

Nilikuwa na challange moja! Kila mwanaume anaekuja anakuja kimaslahi! Siku mbili nyingi ashaanza umatonya! Na mimi jamani niwe muwazi kufuga mabwana sio zangu kabisaa kabisaa! Hata paka simfugi mie itakuwa bwana? Thubutuuuuuuu! Bwana akianza tu vizinga kanikosaaa!

Sasa huyu mwakitombile ndo ikawa na nafuu! Japo sasa file lake ndo chafu chafu halifai! Ila financially he was doing more than well! Ana kampuni zake mwenyewe! Na pesa anazo! Na familia yake pesa ipo! Hata akikupa ofa ya outing ni Dubenga, siku ingine Tokyo! Sio mambo ya kitoto!

Watu wananikumbusha mama chamba sanaaa! Chamba mpaka utoke na mavi! We mkaka mzuri, pesa anayo,unachotaka kitugani? Umalaya umalaya kitu gani baba ako mzazi mwenye malaya vile vile ukichunguzakama unabisha muulize mama yako mzazi! We pishana na fuko la pesa kwenye maandamano uone kama atakosa mke!

He was nice to me, and treating me nice! Nikakubali niolewe! Alivokuwa maloveee kipindi chote cha harusi ungemjua sasa? Mpaka kuchagua nguo huyu hapa! Sijui nini huyu hapa! Zikafanyika sherehekama zote! Nikajipa moyo sijafanya makosa!

Maisha yakawa ya kawaida mwanzo! Upendo upo upo kishkaji! Nikazaa watoto wa 3 still we were going strong! Baada ya hapo kurudi ndo saa 5! Ukimuuliza anakwambia nisinywe na washkaji! Kwanza nakuoa nakunywa! Itakuwa sasa! Usinipangie!

Inapita miezi mwanaume hakushikiiii! Hachokozi mechi! Mimi sinyoi na yeye hanyoi! Misitu ya Amazon na Congo! Ukiuliza sababu hamnaaa! Hamna ugomvi useme umuombe mtu msamaha hamnaaa! Imetokea tu!

Ukiulizakwawengine wanakwambia wembe ni ule ule! We mwezi tu hajakugusa mie nina miaka mi 3! Haki nakuapiaaa! Kaka angu yuleee! We mbona una nafuuu kubwa sanaaa! Ndo ndoa hio! Nawaulizasasa wenzangu mnajiburudishaje? Mzee ndo hanihitaji sasa genye zangu nafanya vipi! Naambiwa mtu mzima HAPANGWI! Jiongeze!

Watu hawakupi majibu ya moja kwa moja! Nikawaulizaau niombe talaka yangu? Wakasema alafu? Mitoto mi 3 utampelekea nani? Hio ramani ya kuzimu tumboni nani ataihitaji, na hizo nyama zilizolegea je? Papa hio imepitisha watoto wa 3, kama valuation of assets tunasema SCARP VALUE! We ndo basi ushafeliii! Na huo ndo ukweli! We bana hapo hapo! Acha kuwa postive! Think of your mother! She stayed with pops not because she loved him, she had no where to go na nyie! Overtime nafsi itakomaaa! Utazoea!

Nawaa!bia hapana aisee! Why do we have to end up like this? Mmmmmmh! Wanaguna! Wanakwambia huko nje kumebadilika! Sio kama ulivokuacha! Sahivi hata wewe ukimtaka kijana umlipe wewe! Umgharamie ndo aingize kojoleo lake akojoe! Ama sivo uibe mabwana za watu, na wakikumata wenywe topaz za uso tu kukuhusu! Bora uendelee kumbembeleza mumeo akufanye hivo hivo hata kwa kungangania!

Think on the bright side! Unajitamba mbele za watu una mume! Umepata wa kukustiri! Una familia! Watu wakiongea familia fyoko fyoko unayo pia! You basically have it all on the outside! Japo u ajua on the inside you have nothing! Who cares? Either way life facks us all!

Nawaambia huyu bwana hawezi kuwa ankaa miezi yote hii hana mwanamke uko nje! Lazima ana mwanamke nawaambia! Naambiwa unauliza majibu! Pigia jibu mstari funga kitabu! Ukisema ukichokonoe utayapata mazito kuliko unayotafuta! Unaweza kukuta mumeo hana wanawake hukonje ila ndo yeye mwenyewe anageuzwa mwanamke! Mwana kulitafuta mwana kulipata! Tuliza mishono mitatu hio lea watoto hao!

Nikaanza kuongea na mume wangu kidiplomasia? Nini tatizo? Nini kimebadilika? Mbona hakuwa hivo! Kama nimekukosea nisamehe! Anasema unapenda sanaa drama! Na mapenzi ya tamthilia! Sisiwazazi sahivi! Tushapita huko! Mara unapenda mapenzi ya kugeza sanaaa!

Nawauliza wenzangu nini kimebadilika! Wananiambia kilichobadilika ulikuwa kijana sasa ni mzee! Afu ubataka upewe wzifa wa vijana! Heheheeee! Kama mazuri vile! Nikambembeleza Mr! twende counseling! Marriage councelling! Akagoma kabisaa! Anasimamia ndoa haina tatizo tatiP ni mimi napenda drama!

Nimevumilia ndugu msomaji miaka kama mi 3! Wa 4 nikaja kufuma sms! Ana mwanamke afu kamjengea nyumba huko Kitunda kubwaa, nzuri hatariii! Nikamsaka huyo mwanamke mpaka nikamjua! Afu mtu mzima sasa! Ana watoto wa 4! Baba tofauti! Hana uzuri wowote ndugu msomaji! Anauza cafe ya chakula! Mama lishe apande juu kidogo!

Niliumiaaa sanaa moyo! Niliumia sanaaaa! Nikaanza kumchatisha kama mkaka nipo bank! Namba si ninayo! Akajaa haraka haraka! Akanielekeza mpaka hapo caffe! Nikaenda! Nikamuangaliaaa! Nikamtumi sms acha kutembea na waume za watu! Nitakitia ki cafe hiko kiberiti! Akajibu mumeo atanifungulia ingine kama alivonifungulia hii! Jeuriii ndugu msomaji! Navowaambia jeuri hamjamjua kabisaa!

Nikapata ujasiri wa kumuuliza kwani mume wangu unampa nini lakini? Akajibu hata nikikwambia jeuriya kumpa hiko nachompa unayo? Nikamuuliza nini unampa acha kuzunguka! Akajibu Matakoz! Mpe na wewe kama unaona rahisi atatulia kwenye ndoa kama maji ya mtungi heheheeeyaaaa!

Nikaona napoteza tu mda! Bwana nilimshika mashati si kidogo! Nikamwambia naondoka na wanangu! Akasema ukiondoka namuha!ishia humu ndani kama unataka kutukomoa bora tu ubakie! Nishakwambia nilipitiwa nitajirekebisha! Nikajipa matumaini anajitutumua tu ila atajirekebisha!

Kweli lileshangingi aliachana nalo! Manake likawalina ni text naona unaloga sanaa siku hizi kuniharibia! Sijui unalala na mganga! Heheheee! Nikajua ashaachika! Nikamjibu cha kuazima hakistiri wowoo! Asharudi nyumbani. Na matusi tukawa tunafanya kama kawaida! Upendo ukarejea!

Miezi mi 3 mingi! Ratiba zikarudia pale pale! Nikajaribu kujua anatembea na nani? Sikuwezakujua kabisaa! Nikakata tamaa! Nikawa nimejikalia nasononeka tu! Nikaja kupenyezewa anatembea na ndugu yake! Wa mbali ila udugi wa kuvuta manati upo! Nikamuuliza akaniambia wewe ni pumbavu kabisaa! Nikatembeee na ndugu yangu ili? Hata kama umaluuni ndo nimekosa kabisaaa kiasi hiko? Hataaaaa! Haiwezekani! Nikamuamini asilimia 100. Ikaja baadae kujulikana tena na mume wa huyu ndugu! Ilikuwa aibu ya kufungia mwaka ndugu msomaji! Alirudi nyumbani mikono nyuma!

Akaanza kutembea na binti wa 18 yrs! Msomaliiiii! Kadogo kakorofiiii Alshababu wa kike! Huyu ndo hajifichi kabisaa! Anawambia wanangu yeye anti! Mwambieni mama yenu anti anawasalimia! Kwanza sikutaka kufanya nae ligi sababu ni mdogo sanaa! Ningeweza kumzaa kama ningeamuaga kuzaa na miaka 16! Afu design nishachokaaa! Najua akitoka huyo ataokota mwingine! Nikakubali tu matokeo!

Akamtia mimba yule msomali akampangishia! Akawa ndo mke mdogo tena! Miminavumilia tu ndugu msoaji! Moyo ukawa u ejaa sumu! Sumu kaliii! Mpaka nikaanza kuumwa pressure! Watu waka ipeleka kwe ye maombi! Maombi yalinisaidia kusamehena kurejesha amani na pressure ikaisha kabisaa!

Nimezunguka makanisa mengi sanaa! Mpaka kufika kwa pastor! Pastor mara ya kwanza nawaona na mkewe kiukweli walinivutia! Anajua thamani ya mke! Anampa mkewe nafasi! Wanavosema apatae mke kapata kitu chema basi anavokienzi sasa! Mwanaume ndo yule!

Akaanza kunipa huduma! Wanangu wako boarding wote, Mr ndo vasco da gama! Nikamjaza mimi single mother! Huku na huku tukaanguka dhambini! Mkewe aliistukia! Na mimi sikuachia sababu na mimi nporwa mume natulia! Nabebewa mume natulia! Na safari hii mwenye mume atulize kitenesi!

Kama biliwaza danger ya fumanizi labda upande wa Mozah! Sio mume wangu! Maana ashanichoka na kunisusa kabisaakabisaa! Sikuwaza kwamba mimi kuchepuka kutamtoa roho kiasi kile! Sikuwahi kuwaza! After all the cheatings nilizomkamata sikutegemea angenivua nguo kiasi kile! Tuna watoto wakubwa! Uzuri wako nje! Na aliwahonga gazeti wamsanue pastor sanaa mimi wafunike funike! Hata sura yangu haikutoka! Wala kazini hawakijua! Still it was inhuman!

Yeye akanipa talaka akajua kanimaliza! Mimi nikaenda mahakamani kufungua kesi rasmi ya talaka na tugawane mali! Hapo kwenye kugawana mali palimvuruga sanaaa! Akakimbilia kwa paroko tusuluhishwe ndoa za kikristo hazina talaka! Paroko akaniandikia wito mara 3 wa kuitwa parokiani! Sikwenda! Akamtuma mwenyekiti wa jumuiya! Nikamwambia nimeokoka sahivi so automatically sio kondoo wake!

Mimi nimeweka wana sheria law firm! Na pendekezo langu nipewe 80% ya mali na custody ya watoto! Nika sight kuzaa nje kwamba kaoa mtu mwingine kiserikali ana ishi nae! Akaona kesi imemkalia vibaya! Akaja kidiplomasia! Anasisitiza watoto watoto! Akaomba msamaha hasira tu! Akaomba anipe mali kiduchu tuyamalize kishkaji! Nikamwambia tukutane mahakamani! Mchaga alidataaaa!

Mlokole kiukweli baada ya tukio alisikitisha sanaa! Mozah alimfukuza nyumbani! Kumbe nyumba wanayoishi ni ya Mozah! Nikampa pesa akapange hoteli ya gharama! Ananiambia siwezi kurudi madhabahuni naomba nitafutie
mtaji wa biashara yoyote!

Msomaji kama mjuavyo sifugi mabwanaa mimi!Kila sms akituma anaomba pesa! Kama mimi ndo nimemzaa vile! Alinichosha sio kidogo! Nifanyie hiki nifanyie kile! Like seriously! Utetezi wake siwezi kupanda madhabahuni! Nikamwambia inaweza kupanda vizuri sanaa! Akasema siwezi gazeti limesambaa nchi nzima!

Nikamwambia kwani mbona wenzio wanasimuliaga nilikuwa jambazi! Nilikuwa kibaka, nilikuwa jela ndo wokovu ukanijiaaa! Na waumini tunatoa Amen za kutoshaa tu! Sasa wewe utasema Nilikuwa Mzinzi, muasherati kasingiziwa! Nikafumaniwa na mke wa mtu, na kuandikwa gazetini! Tafuta gazeti la tarehe flani na mwaka flani utaniona front page! Lakini bwana kaniletea wokovuuuu! Haleluyaaaah! Sasa nahubiri neno! Mbona Amen zitakuwa za kutosha tu?

Anajitetea pale, shida yake asifanye kazi aishi kwa mgongo wangu! Aaaah subutuuuuuuu! Nikaona hatuelewani! Nika mblock! Akawa hana pa kunipataaa kabisaaa! Atanipatia wapi mie mtoto wa mjini? Kama Mozah ndo alikuwa anmfuga ni Mozah huko huko sio mie! Kabisaaa!

Woga tu ndugu msomaji ndo ulikuwa unanirejesha nyuma! Kesi yangu inanguruma! Nikaanza kutongoza vikaka vya bank! Hawa njaa kali! Nikampata mmoja! Kimuonekano ana njaaa na nilitegemea ana njaa! Lakini nimeanza kutoka nae hakuwahi kuniomba kitu! Labda mimi kwa nafsi yangu ndo nimpe!

Mwenyewe kwa kujisikia tu rohoni mwangu nikampatia MarkX, nikampangia na appartment niwe najiachia huko! Mtu wa bata sanaaa! Na mimi watoto wakubwa sina majukumu basi tunajiachia wote sanaa sanaaa! Burudaniii! Watu ofisni wanaongea, lazima waongeee si unajua jelousy, ila sisi hatuna habari!

Siku tunatoka kwenye bata akawa ana search station nikasikia kama sautinaijuaaa! Nikamwambia acha hapo hapo! Ilikuwa Wapo Radio! Nikasia " Mimi nilikuwa mzinzi tena muasherati kweli kweli, nishafumaniwa na mke wa mtu na picha kusambaa magazetini ila leo Nawtangazia wokovuuuu! Ameeeen! Ameeeen! Yesu huyuhuyu alieniokoa mimi mkaribishe kwenye maisha yako! Haleluyaaah! Ameeen! Za kutosha kabisaa!

ITAENDELEA!
 
ahahahahahahahhahahahahahhahahhaahah hakyanani mi nilikuwa mzinzi sanaa! muasherati sanaa! lakini nimeokoka now!
AHHAHAHA hii confession mbn huwa siioangi kwenye TESTAMONIES!
 
Jkk
Episode 1! MAAMUZI MAGUMU!

Nimtongozeee nisimtongozeee! Atanionajeee ndugu msomajiii? Mambo ya ben 10 haya anayaweza mama Dai. Kwanza mtoto mdogo, akinishushua nafanya vipi unadhani ndugu msomaji. Kwanza anawapenda wasichana wadogo wa umri wake. Bora nijistiri mieee. Kwanza star kila mtu anamtaka. Mambo ya kutongoza wameumbiwa wanaume.

Ila mtoto anaonekana fundi sanaa yule, kwanza mashairi yake ya wimbo wa Iokote anapatia mpaka dhambi sasa. Msumari kwa nyundo nikugonge, ikiwa kwa juu chini naizamia! Balaaa tupu. Kiukweli moyoni kaniingia si masihara.

Huyu mtoto sikuwahi kumuona hata siku moja, nilisikia wimbo wa Iokote nikauliza nani kaimba huo wimbo? Maana sio kwa utamu huo, balaaa! Nikaja kujua ni kitoto i was disapointed a lot. Lakini kila niksikiza wimbo anavoimba kama hataki unanivurugaaa balaaa! Msomaji ushawahi kumpenda mtu hakujuiii?

Nikaamua kuomba ushauri kwanza kwa shoga angu Moza. Moza si mtu mzima sanaa kiumri ila kimajukumu ni mtu mzima, ana watoto wa 3, hajawahi kuolewa ila ashaishia na baba watoto zake wa 2 na wote akashindwana nao. Sahivi anaishi peke yake na wanae. Moza kwao ndo boss kubwa, anasikilizwa balaa, na amelea wadogo zake wote. Na ndo anaendesha familia.

Moza ni mambo mengi sanaa, ila kubwa nalomsifu ni jasiri sanaa, tena sanaa. Kwenye kudream big Moza ndo mamba yao. Kama humjui unaweza dhania hana akili vizuri. But she is the dog when it comes in moving mountains. Napenda ushauri wake cause kama mimi katoka chini sanaa. Na sasa yupo juu sana ila hana dharau kabisaa.

Nilimpigia akaniambia niko Kempisky dogo njoo, nikaenda na kumkuta na Mama lakee, huyu mama lakee kazaa na mtu mkubwa sanaa hafanyagi chochote ni kula bata 24/7 na kuspend baaasi. Nikamueleza da moza nina shida ya ajabu. Akanidaka dogo kama unaazima pesa azima tu usitukate stimu, million 5 au 10? Nikasema sio pesa. Wakanikata jicho mwana knyoko.

Nikajieleza mie mwenzenu kuna msanii nampenda. Wanapendaaaa mambo ya chiniii balaaaa, mambo ya kufukunyuana ndo mpango mzima kwako. Wakanidaka juu juu msanii gani? Nikasitaa kuona aibu. Wakajiwahi au Mond bin Laden,nikawaambia under ground tu. Wakaniambia kaimba wimbo gani? Nikajizoa zoa kuwatajia Iokote.

Mama lake akazama kwenye I phone X, akau ugoogle! Akasema balaaaa! Huyu mtoto Hans stone ni nani? Akagoogle, akasema ndo maana. Huyu mtoto wa marehemu Banza, ila katamuuu. Sema nini nakuachia huyu nishakula kuku siwezi kula mayai yake. Hii kazi fanyaaa. Kazi ya uhakika kabisaa hii. Nikapata moyo kumuuliza nafanyaje?

Mama lake akanikata stimu, nikikutongozea mimi nitakudanganyaa nitamla mwenyewe, shetani langu liko jirani mno. Hamna cha kuku wala mayai, nitafagia tu. We jiongeze. Unatongozwaje geuza upside down. Akaendelea kuperuz peruz, akasema mbona mchafu mchafu bado? Mmmmmh! Sidhani i
A sijui.

Moza akaingilia, sahivi pesa ya kutembea na mwanaume wa ndoto zako unayooo, usijibaneee. Throw him few cash, atajaaa. Wana njaa sanaa hao. Maisha mafupi, umebahatika kuzishika mdogo fanya yakupendezayo moyo wako. Its okay to have adictions. Mambo ya uchafu kwani midosho chi town bei gani? Mpendezeshe mwenyewe, afu uzuri wa mwanaume mdogo una mcontrol kwa remote. Mi point yangu do what makes you happy hasara roho tu.

Nikajiongeza nika m dm nimependsana kazi zako, mimi dada yako shabiki yako sanaa. Ukihitaji chochote niambie. Feel freee. Nikawa nangoja kwa hamuuu. Majibu positiveee. Ikiingia notification roho inanienda mpocompoco, nikifungua nakuta Mange has posted new post. Damn! Nangoja tena.

Ikapita wiki bila bila. Nikakata tamaa kabisaa. Moza akaniuliza kwa whatsup Uturuki lini hio? ulikapata kale katoto? Nikamwambia uturuki bado bado ila kwa dogo mambo oves tu. Akasema ngoja, yule si yupo management ya Hanscan, mama lake anamjua tuchukue namba yake umuendee whatsup. Dakika 10 nyingi whatsup hio hapo namba. Ila nakushauri usirembe wewe nenda tu direct, andaa fungu kama laki 5, au maliza M kabisaa mwambie mpige show pesa yako isiende bure mazee.Nikamwambia sawa dada.

Nilikaa na namba wiki nawaza pa kuanzia sipatiii. Nikaamua kumfata mtabe wa hizi kazi shoga angu Linda, yeye anatongoza wanaume sana tu, ila matajiri. Kina Mo hivi ndo kazi yake mjini. Mzuriiii. Hatumii nguvu sanaaa. Muonekano unambeba. Nikamfata kwake ananimbia ana mpango wa kumtongoza mtoto wa Bakhresa. Ndo mipango yake siku zote na atampata. Ukiacha uzuri analoga sanaa.Tena sana.

Hakufurahishwa na swala langu, akaniambia mbona so cheap? Fine you wanna date a star awe basi na hadhi, about that life.Kama mimi nikiwa bored napiga sana show na calissah and he is worth every dime i pay him.sasa hiki kitoto kiko oves sanaa. Kina njaa sanaa. Tena sanaa. I dont know, kipendacho roho hula nyama ilio oza.

Nikamuuliza sasa unanisaidia au vepe? Akasema namba yake si unayo? Money Talks! Tuna humo 30,000 kila wiki, usijitambulishe wewe nani wala unataka nini. Nikimpa mwezi nampendelea atajileta mwenyewe utachinja kiulaini.

Nikamwambia Linda mi nataka anipende, iwe relation sio kama biashara ya kuuza na kununua binadamu! Akanikata jicho. Akasema anza kutambaa ndo utembeee. Usitake kupaa kabla hujakaa. Hio stage one akujue wewe nani na una lipi jipya. Mengine tutaendelea ukifaulu bigginer course.

Nikarudi nyumbani, kabla sijalala nikatuma 100,000 kwa line yangu ya magumashi. Hakuna cha asante wala nini. Ijumaa tena nikatuma 100,000. Mwendo huo huo kama ijumaa 5 hivi. Ikaja text nani mwenzangu? Falasi kweli, mpaka imefika 600,000 ndo anauliza nani mwenzangu?Sikujibu.

Akaja whatsup, samahani wewe nani? Unatuma pesa kila ijumaaa. Au unakosea? Nikajibu wala sikosei! Mimi shabiki wako, dada yako. Kuwa na amani, vikubwa vya balabuu, ila nikipata kidogo nakuwezesha mdogo wangu au nakosea. Akawaka hapana dada hukosei, nashukuru kwa support yako. Tuko pamoja.

Sikushoboka mpaka Ijumaa nikamjaza 100,000 kama kawaida. Akaanza kunitumia za sahivi dada? Dada unaendeleaje? Ama kweli Linda kiboko. I am not cheap. Sikujitokezaa.wala story nae sina. Kabisaaa. Siku hio akaniambia dada nina stress naweza kukupigia nikamwambia HAPANA. Sipendagi ujinga mimi.

Akaja kuniambia, dada unanisupport sana niambie chochote kuhusu mziki wangu. Sababu ya support yako nimeanza kuwa uncommfortable. Ni mwema sanaa kwangu. Niakmjibu hio video uliofanya na Mau sana mbaya is so cheap kingese, ukitoa wimbo wako usifanye video under budget kama hio. Akajieleza vyuma vimekaza hata Mond haendi South kwa Godfather tena.

Nikiwa uturuki nikamuuliza unavaa viatu size gani? Akasema 43. Nikapasuka jordans OG kama pair 5.Nikamnunulia na jeans na tshirt za hatari.Nikampa bodaboda apeleke studio. Jioni akaniuliza sister umeniletea zawadi? Nikamwambia umezipendaaa? Katoto kamejaaa. Uzuri wa vitoto unaona innocense yao kabisaaa. Sio mikonki master.

Akaniambia wimbo wangu upo tayari nataka tukutane nikusikilizishe wewe unipe maoni yako kabla sijautoa. Nikawaza sanaaa. Nikarudi kwa Mama lake, ananiambia we ushafeliii na huo ndo ukweliii. Huyo ahsakufanya dada tenaaa. Kuja kupeana tena sahau. Muite kwako mfiriganeee mambo yaisheee. Moza akasema hapana keep it going like a game tuone mwisho mtaishiaje, nimependa hili muvi lenu. Usiende kusikiliza. Ili asikujue wewe nani wala unataka nini.

Mama kubwa anachombeza, mchezo wa kuhonga huu sio mzuri kabisaa. Ni kama kula nyama ya mtu, ukianza huachiii ngooo. Kuanza ni mgumu ila ukikukolea basi unaanza kuufuja u aweza jishtukia unamhonga mpaka kaka yako kmjaribu tu. Heheheheeeeee!

Akaja kuniambia dada nina shida ya 200,000 samahani lakini. Nikatuma 500,000 nikamuuliza zitakutosha au niongeze? Akasema zinatosha dada asante. Mmmmmmmh! Na badoooo! Akakumbushia mambo ya kunisikilizisha wimbo. Nikawa njia panda.

ITAENDELEA KESHO.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimelitafuta hili goma nikajua nitakuta limependeza!
Fanani mbona unatufanyia hivi lakini!?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom