Weekend story: Bad wives

duuuh! bonge la story aiseee.........wewe mwanamke hakuna usichokijua
 
America The Land Of The Free! The American Dream.

I dont know what i was thinking, but America was nothing as i expected. Kwanza nilikuwa sijawahi ku fly hata short routes, afu mara ya kwanza ni kafly na Ethiopian airways to Adis Ababa, Afu na ku connect mpaka New York. Aaaaaaaaaaahhhh! Ni masaa mengi sanaaa usisikie. Nimefika new york mwili wote unaumaaaa. Mda mwingine watu wanaona ugumu kurudi kwao, pengine wanaiwaza hii safari inawachoshaaa kabisaaa.

Bwana we, nimeingia newyork city, picha likaanza, kwanza pale pale airport nimeinhia chooni sioni cha kuflashia, nikasema shughuli, ngoja nitoke ki vampire, ile nanyanyuka mzigo ukaji flush. Daaah! Nimetoka naona mabomba ila sioni kkoki jamani mambo gani. kuna mpopo alikuwa anadeki vyoo. Nikamuulia excuse me how do i get the water. Mpopo yuko WHAT? Mi nimekaza WATER ile kibongo bongo T lazima isikike. Hanielewi kabisaa. Nikawaza ina maana hiki kimombo hakiombi hata mma jamani. Ikabidi nimuoneshee kunawa mikono.

Akacheka kwanzaaa. Akaniambia put your hand there. kuweka maji hayooo. Nilivozoea nikajua mambo ya sensor. Ila ushamba ulikuwa mkubwa. Joey akaja kunipokea, na kunipeleka chuo. Hiko chuo cha kata sijui hata sielewi na vile vyuo vya bei rahisi aka basi. who cares, it is America baby. Hostel akasema it is very expensive akanipeleka getto, apartment siko kwenye bronx kabisaaa, afu apartment moja tuna share wa 4. Nikauliza jamani hamna gangstars huku nisije pigwa risasi nikaambiwa hamnaaa. Ila pia sio salama sanaaa.

Siku ya 2 Joey kuja akaniambia kazi ishapatikana, it is America baby no kukaa buree, ni kupiga mzigooo. Kazi yenyewe kuosha vyombo, sasa bora wenzangu mmoja anatoa makombo na kuvi load kwenye dosh washer, mi ndo navitoa kwenye dish washer, nashika maji masaa kibao. Mmmmhhh!

Joey simuoni kabisaaa, yani tunaonaa kwa kubeep. Kumuuliza kisa anadai anafanya kazi 4. Tena yeye msaada wake umeishia hapo ashaniingiza America, nikizembea na kufanya ndivo sivo America itanishinda nitaenda kuomba deportation. Ada, kodi vyote juu yangu. Maisha yalikuwa magumuuu hatari. Chuo kikanishinda nachokaa sanaaa. Nikaacha chuo mwenzangu niwe napiga kazi mda wote. Na kilichokuwa kinanibana mi visa yangu hairuhusu kufanya kazi kabisaaaa. so kila kazi wananikatalia, nikisema nafanya kwa nusu hela, wanakubali basi nazidi kujiumiza.

Kazi ya vyombo mikono ikaanza kuoza si ipo kwenye glopes siku nzima ndani ya maji, nikaiacha nikiwa sina kazi hapo. Joey aligomba sio kidogooo. Yani utafikiri nimeua mtu. Afu toka jimefika hajwahi kulala hata siku moja, anasingizia ana kazi nne. Nilivoavha kazi nikamkomalia mda unaoenda kwako nipeleke hata nikuone basi hapo kwako mi mda wote niko freee, anazunguka mbuyu tu, hanipeleki wala hataki kusikia hio habari.

Hela zenyewe kunipa ikawa shidaaa kweli kweli ananisimanga hatari, nikamkumbuka Amar sio kidogo jinsi hela zake nilivokuwa natumia kwa nafasi. Yani nachukua tu navotaka. Na Joey kunisimanga kuliniuma sanaa sababu yeye alichezea sana hela zangu well za amar na sikuwahi kumsimanga hata mara moja.

Siku kama Mungu tu akaiweka simu juu ya meza akawa katoka nje nikasema nichungulie picha, si ndo jikakuta picha zake za harusiiii, mi nilitegemea labda kama kuoa kamuoa head girl, walaa kamuoa mzungu mnene hatariiii. Wale mabongeeee. Na wana mtoto. Kumbe hafanyi kazi 4 wala nini, kaolewa na mzungu anawahi nyumbani kumpikia mkewe. Mxiuuuuuuu.

Alivorudi nikamuulizaa, basi ndo kufunguka kuwa huyo mzungu kamuoa sababu ya makaratasi, hampendi sijui nini. Mzungu mnyanyasaji balaaaa, anampa cha moto sio kidogo. Kwanza chumbani kafukuzwa analala sebuleni, mzungu akikasirika anamuita negro, blood monkey. Alafu anamfanyisha kazi zote za ndani, sio kwa ubaya lakini, manake kulikuwa na maid mchina, sasa analipwa hela ndefu, maana huyo mzungu kwao Texas wana uwezo kinomaa, Tamaa zake Joey akasuggest sababu yeye kazi hana, basi afanye kazi za huyo mchina, mchina aondolewe afu alipwe yeye hio hela. Mkewe akakubali, tatizo likaja baba mkwe, kusikia hio akagoma, akasema joey is family kwanini alipwe, if he can help out in the family to save cost its good then, sababu anakula tu bureee sijui nini. Ndo basi tenaaa.

Mzungu choo hashei na mtu, kisa tu hawajui kutumia choo kistarabu, Joey na mwanae wanatumia choo chao na yeye chake. Afu she is nagging all day and night. Katumikaaa sio kidogo. Hela anazonipa ana bana bana kwenye groceries. Mmmmmhhhh! Nikaona hapa nimepatikana, shule nishaacha, sijui tu nirudi bongo, manake hapa pashakuwa pagumu. Bongo Amar hayupo nitaishije, ngoja nikomae.

Sababu najua kushona na kusuka, nikaanza kuwasuka wasichana wa mule ndani bure. Nasuka rasta za hatariiii , weaving ku bond, sanasana rasta. Nikaanza kupata jina kidogo kidogo. Nakula vichwa napata hela ya maana. Nikanunua cherehani, nikaanza kushona vitenge, naweka etsy na ebay. Nakula oda hatari. Nikiwa sisuki, nashona, utanitaka. Ila mwili ndo unakwa unaumiaaa, maana akzi za mkono ukilala nanhela ina lala. Ikumbukwe mwili wangu dhaifu sanaaa, niliumwa sanaa udogoni sasa nilivoupigisha kazi non stop ikawa kama nimechokoza nyuki.

Nikaanza kuumwa sasa, vitu havieleweki kabisaa. Hela zote nilizopanga nihame pale down town n7tafute sehemu nzuri nikaanza kujiuguzia, Joey nae hana msaada wowote zaidi ya kuni drive hospital. sasa nikirudi naumwa sina hata mtu wa kuniangalia, inabidi niwalipe wale wadada waniangalie kwa masaa, huduma yenyewe ikawa hivo hivo tu. Joey mda wote kabanwa na mkewe. Hali ikawa inazidi kuwa mbaya. Siku Joey akaja na HG kuniona, jinsi nilivokuwa naumwa sikuweza kuwaza kwamba bado wanawasiliana au vipi, after all its America watajijua. Nikamsikia tu HG anamwambia Joey unatakiwa umpeleke hospitali, usipompeleka atakufa, si unaona hali yake mbaya sanaa. Joey anasisitiza nampeleka. Anaambiwa na HG kwa sepcialist , hospital ya private. Analalamika hana bima, mi mwenyewe na bima ya mke wangu, hela nitatoa wapi kama ngese.
Jioni hali ndo ikawa mbaya kabisaa nikaanza kuhisi roho inatokaaa kabisaaa. Nikawasikia wale wasichana wenzangu wanaambiana huyu anakaribia kufa, sasa kesho bwana wake akija amtoe hapa ama sivo jioni tunachukua tunaenda kumtelekeza nje ya hotel huko afie huko huko. akifa humu itakuwa soo si mnajua watu wengine hatuna makaratasi ya kuishi humu, watakuja polisi hapa itafanyika uchunguzi biashara hio haitakiwi kabisaaaa.

Hapa la msingi kesho mchana tunamkokota mpaka mjini tunamtelekeza huko huko akifa huko atajijua mwenyewe. Roho ikaniumaaaa. Nafia nchi ya watu, sina hata wa kunizika, naenda kutupwa barabarani. kweli America sio sehemu ya kujivunia. Wazazi wangu watabakia kungoja mtu arudi arudi kumbe nishaoza kitambo sanaa. Nililia usiku huo. Wakawa wanaambiana kasikia nini tulivosema tunaenda kumtupa, ndo mkomae jamani kesho tunaenda kumtupa Sidney, kesho kutwa tusipokomaa mnaweza hata kunitupa mimi, ndo maisha sasa tufanyaje mnadhani.

Asubuhi nikaamka na nguvu kweli, wanasema mtu kabla hujafa ile siku ya mwisho unapata nafuu kabisaa uage, na kufanya yako manake jioni Israel ndo anatia timu tenaaa. Nikaweka airtime kuongea na Joey kumwambia wanaenda kunitupa hukuu help me out, do something. Joey yuko mi sina pa kukupeleka sasa nifanyaje, namwambia nipeleke hata kwa mkeo, pleaseee. Joey kagomaa. yuko tu im sorry, i am really sorry. Nikazidi kumuona kama senge tu, sasa mi naenda kutupwa sorry itanisaidia nini.

Nikapiga nyumbani, nikaongea na maza, akauliza unaendeleja nikamwambia nimepona nimeanza tena kusuka, nipe mzee niongee nae, mzee nikachana tu kila huku, huku hali yangu mbaya sanaa, wanaenda kunitupa mchana hivooo nikafie barabarani, hamna jinsi, hela hamna, afya yangu imekuwa mbaya sana, sasa i guess this is goodbye, ukiona sipigi simu ujue tayari huku ujue mambo yashakuwa si mambo. Utatafuta njia za kidiplomasia kumuelekeza bi mkubwa kuwa mwanae ndo basi tena hukuuu, ili asije kukaa anasubiri mtu aliekufaaa. Mzee alilia kwa nguvu, ukiona mwanaume analia kwa kwikwi ujue yamemfika, anauliza kwani shingi ngapiii zina takiwa huko niuze nyumba nije. sasa akiuza nyumba wataishi wapi. Nikamwambia ni mipango ya Mungu uwe tu na amani. Nika kata simu.

Imefika mchana wakaja sasa kunipeleka huko mjini, wenyewe wananiambia tumechanga hela tunakupeleka hospitali ukapate msaada kuna Dr. mjini tunakupeleka, nikasema sawa. Sasa nifanyaje, bora kwenda mwenyewe kwa amani wangeweza hata kuniziba hewa au kunipiga au kuniwekea dawa nizimie ndo wanipeleke kinguvu. Nikachukua kibegi changu, nikawa nakokotwa mpaka mjini. Wengine wanaliaaa kimya kimya machozi tu yanawatoka, wengine kwa kwikwi. Mmmoja akasema mi kesho naenda kuomba deportion nirudi nyumbani siwezi kufika hali hii. Mwenzie anamwambia unaweza usiumwe, haya maisha tu kila mtu na bahati yake. Tukafika kwenye park wakaniambia subiri hapa pumzika, tunakujaaa. Nikajua ndo kimojaaa.

Nimekaa nikaikumbuka ile namba alionipa Amar, nishakubali tu moyoni kwamba mimi ndo basi tenaaa, nikasema tu ngoja nimuage Amar he was nice to me at a point in time. Nikaipiga ile namba kingereza tu kile nikajua huyu mbongo zis na zat nikamuuliza tu naomba namba ya Amar, akasema Amar huyu hapa ongea nae, kuongea nae, maneno yakaniisha. Kumbe yuko USA mda wote huo, mi nateseka yeye yupo hapa hapa. Nikawaza kwanza leo nakufa itasaidia nini kunungunika. Nikamwambia Amar mi nakuaga nakufa leo, akashtuka unajiua au? Unajuaje unakufa, nikamwambia tu nimeumwa upyaaaa, sasa wenzangu wamekjua kuniweka hapa park huku Missour hali ni mbaya sanaaa. Just wanted to say goodbye. Akaniambia we nenda polisi mi nakuja huko polisi. Nikamwambia karatasi zime expire, chuo niliacha siwezi kusaidiwa na authorities, mi ndo nakaa hapa nife, kwaheri. Nikakata simu. Alipiga ile simu mpaka ikaisha chaji ikazima. Nikafumba zangu macho nangoja kurudisha namba.

Kigiza kikaanza kuingia, mara nikasikia mdada ananiita Sidney, kumbe HG, nikashangaa, nikamuliza umejuaje niko hapa akasema Joey alinimbia watakuja kukutupa leo, sasa ndo nikawaomba waniambie walipokutupa wakaniambia. Twende nyumbani. kukweli kufa nilikuwa tayari ila kufa mwenyewe nilikuwa naogopa hatari. Nikajikokota hivo hivo mpaka kwenye gari.

Kufika kwake anakaa uzunguni kwa wazungu, kuzuri, sasa yule ndo alikuwa anaishi Amrican dream. Akanipeleka chumbani. Baadae nikazima sikumbuki kilichotokea nastuka, nasikia wanagombana na mzungu kabisaa kwa tonation yake atakuwa wa London, anamwambia "I cant believe you brought an illegal imigrant who is dying in our home, you know what that means? when shs dies he we are in big trouble for housing an illegal imigrant and you know this country. Her friends were wise to damp her, so should we, i dont want her here by the time i come back. You wanna help her fine, help her but not in my facking house. Take her to your church or something." Mmmmmmh nikajifanya bado nimezima nisije kutupwa tena.

Akaja nesi akasema huyu anatakiwa apelekwe kwa specialist. HG anamwambia nesi hana karatasi hawezi kupelekwa kokote, just help her. Nesi akafikiria akasema kuna Dr. Myahudi mwenzangu, alikuwa expert huko Israel sasa huku hajapewa vibali kabisaa, Ila anajua sanaa ni very good dr. na sio expensive labda aje amuangalie tuone atamsaidiaje. HG yuko sawa sawa kabisaaa.

Nikamuomba nesi simu aiweke kwenye charger, nikawa nasikia inaitaaaa nguvu ya kuichukua sinaaaa. Nikazimia kabisaaa tena.

ITAENDELEA.
 
hapo sydney solution kumpigia amar though he is sturbbon atleast he loves the dumb girl but cannot axept the fact of kupelekeshwa..... ila chondechonde america sikanyagi bila helaaa... tna saiv yuko trump ndo bac kabisaaaaa
 
Lara1 mama tunakusubiri huku Maana sasa ni SAA saba ati fanyaga manuva basi hakijaiva ama ndo cheleachelea.
 
Back
Top Bottom