Weekend hii ni kinywaji, ni chakula, ni dawa/booster na pia ni Natural Supplement

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,652
14,247
Katika siku za week naipenda sana Jumamosi. Hii huwa naitumia kufanya shopping ya Vegetables na Fruits pia kufanya mapishi au kuandaa juice/smoothie.

Jumamosi hii nlikuja na kitu kizito. Huu ni mchanganyiko ambao binafsi huwa naupenda sana kwa siku za weekend.

1. Tende nusu kilo
2. Maziwa fresh lita moja
3. Ndizi za Kuiva 6 (Napendelea Malinyi)
4. Korosho Robo kilo

Maandalizi

Huwa namenya ndizi na kukata vipande vidogo vidogo na kuweka kwenye Fridge vigande( hii husaidia wakati wa kusaga viwe laini zaidi)

Nachukua tende natoa mbegu then naweka kwenye Blender na kumimina maziwa ambayo nlishayachemsha yakapoa. Nasaga. Then nachukua ndizi na kuweka kwenye blender naongeza maziwa nasaga sana iwe laini.mpaka inakuwa nzito.naweza punguza ili niongeze tena maziwa na korosho.

Hapo ntasaga tena na kuhakikisha imekuwa laini sana.ntaendelea ku dilute na maziwa kupunguza uzito kisha ntaweka flavor ( mara nyingi hupendelea Vanillla) au bila flavor sababu korosho zenyewe pia zina flavor.

Tayari smoothie yangu naichanganya zaidi ichanganyike kwa ku blend humo humo kwenye blender.

Inakuwa nzito kiasi nitakacho.napenda sana nzito ya kunywa na kijiko.hapo naweka kwenye friji tayari kwa kuliwa.

Faida zake ni nyingi ikiwepo

1. Kuongeza nguvu mwilini
2. Protein kujenga mwili
3. Kuleta hamu ya kula pia
4. N.k

Ni nzuri ila inaweza sababisha uongezeke uzito ikiwa hufanyi mazoezi. Otherwise tumia na fanya mazoezi ujenge mwili vizuri.

NB: MWILI HAUJENGWI KWA MATOFALI HATA SIKU MOJA.
 
Hiyo namba 4 ndiyo ilitakiwa ianze.
Maana shughuli yake si ya kitoto.

Weekend hoyeee
 
Back
Top Bottom