Week end ya pekee kwa kinamama wa tanzania kufurahi

Ndachuwa

JF-Expert Member
Mar 8, 2006
6,269
4,569
Ni week end ya pekee kwa kinamama wa Tanzania baada ya Mh. Anna Makinda kuchaguliwa kuongoza Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mara ya kwanza. Ni week end ambayo haitakaa ifutike katika historia ya Tanzania kwani hapatakuwepo mama mwingine zaidi ya Mh. Anna Makinda kuwa mwanamama wa kwanza kushika wadhifa wa spika. Ni mategemeo yangu kuwa kunzia mtoko wa leo (Ijumaa) jioni mpaka Jumapili kwa furaha mliyonayo kinamama wallet za waume zenu hazitafunguliwa muwapo kwenye sehemu za starehe. Onyesheni uwezo wenu kwa kutulisha na kutunywesha angalau week end hii tu kudhihirisha furaha mliyonayo baada ya mwenzenu kuukwaa uspika.

Mimi namtakia Mh. Anna Makinda afya njema aweze kuliongoza Bunge letu lifanye vizuri kazi yake ya kusimamia serikali kwa miaka mitano ijayo
 
alishindwa alipokuwa waziri, bado akiwa na nguvu with sharp mind, akiwa kibibi hivi ataweza? si bora wangempa vicky kamata ijulikane ni bora liende tu.
 
Hapa nazungumzia mwanamama wa kwanza kuwa spika. Evaluation itafanyika baada ya muda kupita
 
Sion faida kubwa kiasi cha kuwajaza furaha wakinamama wikend yote bila kuuona uwezo wake sababu aweza kuwa balozi mbaya na kuwaharibia wengine ila angeteuliwa kuwa waziri ktk wizara fulan nyeti labda wangefurahi kwa matumain ya kusaidiwa lkn bungeni sjui anwasaidiaje?
 
wala kinamama hawajafurahi hata chembe , sio kila mwanamama kuwa mtu fulani wa kwanza inawaamaze wanawake, sana sana watasikitika kuona hoja muhimu zenye maslahi kwao na watoto wao zinapotupwa mbali na mwanamama mwenzao.
 
Hivi bila kupewa fursa ya kufanya kitu unaweza kuonyesha uwezo wako? Mimi bado naoni kitendo cha mwanamama kukabidhiwa kusimamia mhimili wa Bunge ni jambo linalofaa wanawake wote kujipongeza.
 
wala kinamama hawajafurahi hata chembe , sio kila mwanamama kuwa mtu fulani wa kwanza inawaamaze wanawake, sana sana watasikitika kuona hoja muhimu zenye maslahi kwao na watoto wao zinapotupwa mbali na mwanamama mwenzao.

Unaonekana umekata tamaa hata hajaanza kazi. Mpeni muda aonyeshe uwezo wake, akishindwa wananchi wa jimbo lake watakuwa wa kwanza kumwadhibu 2015
 
1.Wanawake walio wengi hawapendani kwa hiyo inawezekana isiwe siku ya kufurahia kama unavyofikiria. 2. Wanawake hawaishi sayari nyingine ni hii hii na hakuna namna ya kumtenganisha mwanamke na mwanaume kwa hiyo
Anachoweza kufanya Makinda kiwe kizuri au kibaya kina madhara kwa jamii na siyo jinsia. Tahadhari ni akianza kupigana na mafisadi anaweza ishia pabaya kama 6. Ana uhuru wa kuchagua. Namtakia kila la kheri katika kuchagua
 
......Kwa kweli nimefurahia huyu mama kuwa spika wa kwanza mwanamke kwa Tanzania, Mungu amsaidie kuongoza bunge salama.
 
Back
Top Bottom